Sivutiwi kabisa na haya mabeseni ya kuogea (Bathtub)

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,508
99,305
Tumezoea unaoga uchafu unatoka mwilini, sasa ile unaoga afu uchafu unarudi Kwenye maji Yale Yale Ni KERO Sana kiukweli.

Unaharaka zako unahitaji uoge chap chap uende zako afu unakutana na mtihani wa kutumbukia mzima mzima ujiloweke kwanza Kwenye beseni.
Ni kupotezeana muda kiukweli.
 
Ukiona kitabu hukielewi hujaandikiwa wewe. Kwenye picha ulizoweka ipo moja ina shower. Mara nyingi mtu mwenye uwezo wa kuweka bath tub hashindwi kuweka na shower hapo hapo au kwenye kisehemu kingine pembeni. Bath tub sio kwa ajili ya kuoga kuondoa mauchafu yako uliyotoka nayo gereji huko, hio ni kwa ajili ya relaxion baada ya uchovu na stress za siku nzima ndio maana unakuta wengine wanaingia na vitabu au wanalala kabisa.
 
Ameweka hapo na ki champagne anarelax mwenyewe, yuko kwenye bubble bath
 
We hujawahi kuona mtu huku uswahilini kala ugali mkubwa na dagaa wa mwanza.Akishashiba kitumbo ndi!!!unasikia anasema kwa jinsi nilivoshiba hivo natamani nipate beseni kubwa lijazwe maji niingie ndani nitulie.Sasa wazungu ndo wakakuletea hizo madude.
 
Mkuu

Kuna majani huwa yanawekwa kwenye hizo
bathtub ….

Kama una maradhi au stress za tozo zinaondoka…..

Pia yanaongeza umri wa kuishi…..haijalishi

changamoto za tozo, Mgao wa umeme wala maji….

Mwenye kuyajua hayo majani ayaweke hapa…..

Shukrani!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…