Siupendi wimbo wa Taifa

Siupendi wimbo wa Taifa

TAI DUME

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
11,352
Reaction score
31,351
ANGALIZO: KAMA HUAMINI KATIKA UWEPO WA MUNGU MWENYE ENZI USISOME

Mungu ibariki Tanzania.
Aibariki mara ngapi? Hivi tunautani na Mungu?! Aibariki ktk nini kilichobaki labda?

Ni nini ambacho mnataka kumsingizia Mungu ambacho alikisahau kukiweka ktk nchi hii.

Mnitajie ni nini ambacho hakiwatoi udenda watu wa magharibi kuhamia hapa. Mungu awabariki na nini tena? Au magunia ya funza na ndoo za kamasi?

Neno lake liko wazi kabisa. "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa ". Maana ake ni kwamba MUNGU anatoa rasilimali tu. Kutafuta maarifa ni kazi na upeo wa mwanadamu.

Mungu hatoi maarifa labda kwa wateule wachache kama mfalme suleimani tena kwa maombi ya upendeleo. Sisi hatuna suleimani hapa. Tutafute namna ya kubadilisha rasilimali ambazo MUNGU ametubariki ili tufaidi baraka zake. Na sio kuendelea kulia lia kupitia wimbo wa taifa.

Mungu anachukizwa na binadamu ambao hawana SHUKRANI. Hapendi unafiki. Ndio maana hatuishi kupigwa na umaskini, magonjwa, ufisadi, risasi zinazokata kona angani, kujiteka na mengine mengi sana.

Tubadilike. Mungu ameshatubaliki. Shetwani wetu ni kukosa maarifa na uzalendo. Tubadili hii nyimbo. Tutengeneze nyimbo yenye kuleta hamasa ya taifa kufanya kazi, kuwachukia wezi wa rasilimali zetu, Kutafuta maarifa lakini bila kusahau walau mstari hata mmoja wa kumshukuru. Vinginevo laana zitaendelea kutuandama vizazi na vizazi.

MUNGU TWASHUKURU KWA BARAKA ZAKO. AMEN
 
Aibariki ipate viongozi waadilifu, wenye upeo mkubwa wa kuweza kusimamia rasilimali za taifa, wasio na ubaguzi, ukabila, udini na ukanda.... Wenye kujali na kuthamini we wengine.... Wasio na chuki, vinyongo, vusasi na kulewa madaraka.... Walio na utayari wa kuwatumikia wananchi kutoka moyoni na si kwa kusukumiziwa
 
Una point Mkuu, wakati mwingine mawazo ya wakati fulani hayawezi kuwa valid ule wakati ukipita. Ni vyema tukafanya tafakari ya mambo mengine pia kama vile bendera ya taifa naona kama rangi zake ziko kishamba shamba sana na ile alama ya twiga (huyo mnyama huko porini wanyama wenzake wanamshika makalio) inabidi akae mamba au jaguar au the lion himself.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom