Sitta: Zitto achana na ndoto za Geita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Zitto achana na ndoto za Geita

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Apr 17, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Na Frederick Katulanda
  Gazeti la Mwananchi

  SPIKA Samuel Sitta jana alimshauri Zitto Kabwe kuachana na ndoto za kuwania ubunge wa jimbo la Geita, lakini muda mfupi baadaye kiongozi huyo wa Bunge akaomba msaada wa sala kutoka kwa paroko ili aweze kushinda uchaguzi kwenye jimbo lake.

  Spika alitoa ushauri huo baada ya Zitto, ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, kuomba kuuliza swali la nyongeza kuhusu mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Geita wakati wa kipindi cha maswali na majibu jana kwenye Mkutano wa 19 wa Bunge unaoendelea mjini hapa.


  Swali la msingi kuhusu mradi huo liliulizwa na mbunge wa Geita Mjini, Ernest Gakeya Mabina, ambaye alitaka kujua kama serikali inatambua kuwa mgodi wa dhahabu wa wilayani humo uko tayari kutoa kiasi cha dola 500 milioni za Kimarekani kwa ajili mradi huo.


  Baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Aggrey Mwanri kujibu kuwa serikali haina taarifa hizo, Zitto, ambaye ameeleza kuwa huenda atalitosa jimbo lake na kugombea ubunge wa Geita, alisimama na kuelezea matatizo ya maji yanavyoisumbua Geita na kuiomba serikali kuangalia uwezekano wa kutoa fedha za kusambaza maji kutoka kwenye matanki.

  "Kwa kuwa mgodi utatoa fedha za kukutoa maji kutoka Ziwa Victoria hadi kwenye matanki, ni vizuri serikali ikatafuta fedha ili ifanye kazi ya kusambaza maji kwenda sehemu mbalimbali," alishauri Zitto.


  Lakini kabla ya kumkaribisha Mwanri kutoa maelezo, Spika Sitta alisema: "Kwanza naibu waziri ningependa kumshauri kidogo Zitto. Naomba uachane na mambo hayo ya kugombea ubunge wa Geita. Ni vizuri ukarudi kwenye jimbo lako."


  Kauli hiyo ya Spika Sitta iliamsha kicheko kutoka kwa wabunge wengine.


  Akizungumzia kitendo chake cha kuzungumzia masuala ya Geita mara baada ya kumalizika awamu ya asubuhi ya Bunge, Zitto alisema suala hilo halina uhusiano na uamuzi wake wa kutaka kugombea ubunge wa Geita na kwamba amekuwa akiamini ni mbunge wa watu wote na kutoa mfano jinsi alivyokuwa mstari wa mbele katika sakata la mgodi wa Buzwagi.


  "Nimekuwa nikitetea Watanzania wote bila ya kujali mipaka ya majimbo, mfano ni wakati nazungumzia suala la Buzwagi. Mimi sikuwa mbunge wa Kahama, lakini nililizungumzia," alieleza mbunge huyo kutoka Chadema.


  Hadi sasa, Zitto bado hajaamua agombee wapi kati ya Kigoma Kaskazini na Geita baada ya kufanya uchunguzi ambao alisema ungetoa picha ya nini afanye kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.


  Uchunguzi wake, ambao alisema ulifanywa na watu wake, ulihusisha majimbo ya Kinondoni, Kahama, Geita, Kigoma Mjini na jimbo lake Kigoma Kaskazini lakini baadaye akasema kuwa ameachana na majimbo matatu na kubakiwa na Geita na Kigoma Kaskazini na kwamba angetangaza uamuzi wakati wowote.


  Baada ya kipindi cha maswali na majibu, Sitta naye alijikuta kwenye masuala ya uchaguzi wakati alipomuombaparoko wa Parokia ya Urambo Mashariki kumuombea dua ili aweze kurudi bungeni mwaka 2011.

  Spika, ambaye amekuwa akidai kuwa mafisadi wanamuandama kwenye jimbo lake na wakati fulani kuomba aongezewe ulinzi, alitoa kauli hiyo wakati akitambulisha wageni waliofika bungeni jana baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.


  Alikuwa akitambulisha kikundi cha wanakwaya 36 kutoka Urambo ambacho kilitembelea Bunge jana kikiwa safarini kuelekea jijini Dar es Salaam kurekodi albamu yao.

  Jamani mwaka huu ni mgumu kweli, kwa hiyo nyinyi watu wa dini mtuombee sana kwa Mungu kwa sababu hali ni ngumu kwetu, alisema Spika Sitta.


  Kwa hiyo mkirudi jamani, mtuombee na mumwambie Baba Paroko Mongela atuombee ili aliyebora apite Urambo Mashariki.


  "Sio lazima mimi lakini atuombee ili aliyebora apite na kuwa mbunge katika jimbo la Urambo Mashariki mkoani Tabora."

  Wakati akiwatambulisha wanakwaya hao wa Kikundi cha Mtakatifu Cecilia kutoka Urambo, Sitta alisema kikundi hicho kinaongozwa na mwalimu kutoka Kenya ambaye anafundisha shule ya kimataifa ya mtakatifu huyo.

  Baadaye akaipigia debe shule hiyo akisema: Jamani sio muwapeleke (watoto) kwenye shule za mjini, hata shule za vijijini kama shule yetu ya kimataifa ya Urambo Mashariki.


  "Halafu, Waziri wa Maji, shule yetu ile ya kimataifa ya Urambo haina maji, kwa hiyo nakuomba ufanye utaratibu wa kutupatia maji."
   
 2. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hivi siku hizi Spika ndiye anaye washauri watu majimbo ya kugombea ubunge au alifanya hivyo kwa Zitto tu?
   
 3. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Fuata yanayosemwa na watu wengi kaka zito, ni bora ugombee kwenu kigomaaaaaaaaaaaa mwisho wa reli
   
 4. shugri

  shugri Member

  #4
  Apr 17, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani mbona anakuwa mgumu huweka wazi wapi atagombea?
  Woga wa nini kaka- amua watu waelewe?
  :frown:
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kishachemsha, mwaka huu hapati kitu........... ameleta utoto kwenye siasa............ ngoja wazee wamfundishe siasa.................
   
 6. shugri

  shugri Member

  #6
  Apr 18, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Akili kusema ukweli hata mie nafikiri hicho ndo kitamkuta sasa naona mahesabu yanamshinda aende wapi maana wananchi wa kigoma kaskazini nasikia wamemkasirikia kwa kuwa ametumia muda mwingi dar es salaam kuliko jimboni kwake----

  ukiona mtu anakuwa mgumu kuweka wazi mipango yake ujue mahesabu hayajakaa vizuri!
  Wapi aende kute anaona kunawaka moto!

  Just an observation:target:
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Apr 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu,

  Kwa siku hiyo mimi nilikuwa nafuatilia kikao hicho cha Bunge kwa makini sana na hakika taarifa iliyondikwa hapa imepotoshwa. Sielewi malengo yake haswa.

  Aliyeishauri serikali kuchukua dhamana ya kusambaza maji ni mbunge mwenyewe wa Geita na ndilo lilikuwa swala ama hoja yake kimsingi. Naibu Waziri Mwanri alimjibu mbunge huyo kuwa ombi hilo atalifikisha na ktk swali la nyongeza ndipo Zitto aliposimama kuishauri serikali kuzungumza kwanza na Halmashauri ya wilaya hiyo kupata picha kamili kabla haijachukua hatua zozote..

  Sitta, ambaye binafsi nilimwona kutotumia busara ya kiti chake alirukia na kumkanya Zitto kwa kejeri kwamba Maswala Ya Geita awaachie wana Geita. Hii ni dharau kubwa sana kwani baada ya swala hili tu lilifuata swala jingine ambalo mbunge wa viti maalum aliuliza pia swali la nyongeza ktk swala ambalo halimhusu. Sasa sie;lewi kama utaratibu wa Bunge hauruhusu mbunge kuuliza, kukanya ama nyongeza yoyote isiyohusiana na jimbo lake.

  Kifupi kikubwa nilichoshangaa siku hiyo robo tatu ya wabunge hawakuwepo, viti vilikuwa vitupu kabisa hali kulikuwepo na maswala mengi muhimu sana ambayo yalihitaji mchango mkubwa wa Wabunge..

  Wakuu zangu katika kukaa kwangu hapa Tanzania nimepata darasa zuri sana na hakika kama ilivyokuwa mwaka 2005 kabla ya Uchaguzi uliopita nitarudi tena na makala Inayohusu ile mada nzito isemayo - ili tuendelee tunahitaji nini?..Mwkaa 2005 nilisema tulihitaji kuundoa UFISADI kwanza, haikufanyika na hakika ufisadi ulikuja kuwa mada kubwa Kitaifa hadi leo hi navyozungumza. Sasa basi kwa kuwapa tu dondoo safari hii nasema hivi Ili tuanze hatua ya kwanza ktk mapinduzi ya kijamii safari hii adui mkubwa wa maendeleo ya Tanzania ni CCM -hivyo ndio kusema ili tuendelee tunahitaji kuing'oa CCM madarakani..hakuna cha ziada ama pungufu..

  Kwa nini? - hilo ni somo ambalo nitakuja lizungumzia ktk mada nzima inayowatahadharisha Watanzania wenzangu kuhusu mfumo nzima wa Utawala wa Chama CCM .

  Inshaallah nikipata muda wa kutosha nitarusha hoja nzito ambazo nimezishuhudia mimi mwenyewe ktk utafiti wangu..
   
 8. shugri

  shugri Member

  #8
  Apr 19, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mukandara,
  Unachosema ni kweli ni mara nyingi tuu watanzania huona jinsi spika anavyoudhoofisha upinzani ndani ya bunge hasa kwa kutumia kiti chake kukejeli na mara nyingine kupuuza hoja zinzotolewa. Nadhani hilo linahitaji mjadala wake mwingine kabisa. Kinachoulizwa hapa ni lini Zito ataliambia taifa ni wapi ana mpango wa kugombea maana tumechoshwa kuyumbishwa mara kinondoni, mara geita mara kigoma mjini, tena narudi kaskazini!
  This is a sign of a politician who is only about political power and not committed in bringing cuctainable change in one particular place where he identify himself with!
  Tumechoka watanzania sema unagombea ama la?
  Regards
   
 9. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa rais wetu alishasema huu ni mwaka wa siasa hivyo siasa kama inavyofahamika haina nadharia maalumu (fomula) kila mtu anafanya anavyoona itamsaidia. Kwa Zitto pia naye naona mwendo ni huo huo. Silioni tatizo katika hili kwa sababu mwanasiasa yoyote huishi kwa kupima upepo ikitokea umepima upepo na kuona mambo hayaendi kama ulivyotaraji unabadili mawazo.

  Napendekeza apewe muda kwani muda wa kufanya maamuzi bado na muda wa kufanya hivyo ukifika atatujulisha.
   
 10. shugri

  shugri Member

  #10
  Apr 19, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  But dont u see that is a sing of political stagnation to him.
  Being very popular in a short time considered a hero,
  yet his is stranded and full of fear of just comming clean
  and face the people again!

  Wow i wish to here is campaign- just view on what agle
  will he use this time?

  Atoke vipi?
   
Loading...