Sitta: Siogopi kushtakiwa kwa kumtetea Mwakyembe

Tofty

JF-Expert Member
Nov 6, 2008
206
13
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema haogopi kupelekwa mahakamani kutokana na kutamka kuwa Dk Harrison Mwakyembe amelishwa sumu, kwak sababu ana ushahidi wa kutosha.

Kauli hiyo ni mwendelezo wa mjadala mzito unaotikisa nchi kwa sasa baada ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, kusema polisi wameandaa jalada la kumpeleka mahakamani waziri huyo kutokana na madai hayo.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Wwaziri Sitta alisema kama Dk Mwakyembe amedai kuwa, ripoti ya daktari wake inaonyesha kuna kitu kwenye ndani ya mifupa kinachochea hali aliyonayo, yeye anapelekwa mahakamani kwa kosa lipi.

Tayari, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda, amemruka Manumba akisema hatambui ripoti ambayo aliitoa kwa waandishi, ambayo inaonyesha Dk Mwakyembe hakunyweshwa sumu.

Sitta akisisitizia kwamba Dk Mwakyembe kapewa sumu, alisema kutokana na hali hiyo yupo tayari kwa lolote katika hilo na kwamba, anasubiri jalada hilo lipelekwe mahakamani ambako ndiko kwenye uamuzi wa kisheria.
“Ukiwa mwanasheria huwezi kuogopa mahakama, mimi ni mwanasheria namba 384 wa Mahakama Kuu.Nimesajiliwa kisheria na natambulika kwenye vyama vya wanasheria. Niko tayari kwa lolote litakalotokea kuhusu hilo na siwezi kuogopa kwa kusema ukweli,”alisisitiza Sitta.

Aliongeza kuwa anachotakiwa kufanya DCI, ni kuwasiliana na viongozi wake wa juu akiwamo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili aweze kuwapa taarifa hizo na kuwasilisha jalada hilo mahakamani.

Sitta alisema licha ya hilo, anashindwa kuelewa kosa linalompeleka mahakamani, ikiwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Mponda amemkana na Mkuu wake wa kazi ( IGP), Said Mwema.

Alisema Dk Mwakyembe mwenyewe ametoa ufafanuzi kuhusu suala hilo na kumwambia DCI alikopata mamlaka ya kutoa tamko kuhusu afya yake,hivyo basi anasubiri jalada hilo lipelekwe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), ili afikishwe mahakamani.

Alisema anachotakiwa Manumba ni kutekeleza kile alichokusudia ili aweze kufanikiwa, kutokana na hali hiyo anasubiri uamuzi huo.

“Ni kichekesho bwana, we unafikiri mimi naogopa kupelekwa mahakamani kwa hili? Hata siku moja... niko kwa ajili ya kusema ukweli, nitasema ukweli daima na wala siogopi kwenda mahakamani, nashindwa kumwelewa huyu bwana, tena muulize Manumba ameshawasiliana na viongozi wangu wa juu maana sheria zinasema anapaswa kuwasiliana nao kabla ya kuwasilisha jalada lake mahakamani,”alisema.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Manumba alikanusha Dk Mwakyembe kulishwa sumu na kwamba, jeshi hilo linakamilisha uchunguzi ili kuwasilisha jalada la kumfikisha mahakamani Waziri Sitta kutokana na kusambaza habari hizo.

Alichokisema Dk Mwakyembe
Mwishoni mwa wiki iliyopita, akitoa tamko baada ya kukerwa na kauli ya polisi, Dk Mwakyembe alisema anapata taabu kuamini kama Manumba na wenzake walisoma taarifa halisi ya matibabu yake au walisoma taarifa ‘nyingine’ na kama waliisoma wenyewe au ‘walisomewa’

“Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa waandishi wa habari, hakifanani kabisa na picha iliyoko kwenye taarifa halisi ya Hospitali ya Apollo inayotamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow (uboho) kinachochochea hali niliyonayo,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:

“Kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua, kukidhibiti au kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi wala aibu: hakulishwa sumu.”

Pia, alitoa sababu kuu tatu za kupinga ripoti o ya DCI akisema:"Kwanza, kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake, unaoendelea katika Hospitali ya Apollo, nchini India, ambako bado sijahitimisha matibabu yangu, pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa “sikunyweshwa sumu” wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu.

Alisema sababu ya tatu ni kitendo cha Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima sasa, halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.

Source: Mwananchi
 
Napata hasira sana.huyu Manumba baada ya kupeleka mafisad mahakamani,ambao wanaleta umaskin,anajitumumua kwa mambo madogo,haya akikutwa na atia,inapunguzaje umaskin
shame of them
 
sasa sita wasaidie wananchi na polisi basi kutaja jina la mtuhumiwa kusema tu kalishwa sumu si kumtetea,mshauri ndugu yako swape waandishi ripoti yote kuna wasomi wengi tu wataidadavua, SITA UMEGEUKA KASUKU ANAE KARIRIA MANENO K ALISHWA SUMU,SUMU,SUMU INAWEZEKANA UNASEMA UKWELI SASA KAMA HUENDIBELE ZAIDI YA HAPO TITAKUPUUZA
 
sio kazi ya Sitta kutafuta mtuhumiwa!
 
Sita ng'ang'ania ukweli na akishindwa kukupeleka mahakamani, mpelekeni yeye sasa kwa kulidanganya taifa maana waziri wa afya na bosi wake IGP wamemruka. Pia wapi amepata mamlaka ya kutoa tamko la afya juu ya mh. Mwakyembe?
 
big up mzee sitta

Watanzania tunapenda kujaji kabla ya kusikiliza kesi yenyewe ambayo inataka ushahidi wa kutosha ili kumtia mtu hatiani. Wakati maumba anshutumiwa kaingilia haki ya Mgojwa kwa kusema hakupewa sumu iweje nae Sitta aseme moja kwa moja kwamba kapewa sumu au yeye haingilii haki ya mgonjwa?
Hata kama swala la kupewa sumu lipo je Mwakyembe maadui wake ni hao wanaotajwa kuwa Mafisadi tu na hakuna uwezekan wa mwingine yeyote ambaye ana conflict nae katika nyanja yeyote ile?
Hapa ushahidi wa kutosheleza ndio kitu muhimu. Labda swali kuu liwe ni nani anayeweza kutoa ushahidi wa kutosha ambao utakuwa wa kuaminika?
 
Mtabishana sana. Lakini Mungu anajua ukweli wote!
 
Ushahidi upo ila longolongo kibao,sasa ndo nini kuzunguka ukweli? Sitta shikilia msimamo.
 
sasa sita wasaidie wananchi na polisi basi kutaja jina la mtuhumiwa kusema tu kalishwa sumu si kumtetea,mshauri ndugu yako swape waandishi ripoti yote kuna wasomi wengi tu wataidadavua, SITA UMEGEUKA KASUKU ANAE KARIRIA MANENO K ALISHWA SUMU,SUMU,SUMU INAWEZEKANA UNASEMA UKWELI SASA KAMA HUENDIBELE ZAIDI YA HAPO TITAKUPUUZA

Mkuu unafikiri hata akimtaja huyo mhusika kwa wananchi itasaidia nini wakati mamlaka zinazohusika na sheria zimeshatamka na kugongana zenyewe kwa zenyewe kua Mwakyembe hakulishwa sumu na nyingine zikisema hazijatoa mamlaka kwa dci kutamka hvyo?hii ni sinema ambayo hata mtoto wa darasa la kwanza haitaji muda kuielewa!i will always stand kwy ukweli,na ukweli huo upo kwa dr mwakyembe na hn Sitta
 
Kwa maoni yangu tuache Mh. Mwakyembe augue kwa amani kwani ugonjwa wake hatujawahi kuusikia, angalau mimi sijausikia. Kwahiyo ni ugonjwa ambao tunatarajia mgonjwa anapata machungu makubwa physically na phychologically kuliko mgonjwa wa ukimwi wa leo.

Kama mtu amesema amenyweshwa sumu tarajio langu ni kwa ndugu zake kutaka kujua kama ni kweli na nani kampa sumu. Ni juu ya mgonjwa na ndugu zake na hasa daktari kutoa tamko la kupinga usemi huo. Mtu mwingine hana sababu ya kuingilia usemi huo kiasi cha kukanusha bila ya kujua aina na chanzo cha ugonjwa wa mgonjwa isipokuwa pale atakapo ambiwa ni yeye aliyempa hiyo sumu, hata kuhisi hivyo tu bila ushahidi hapashwi kupinga usemi huo kabla hajasema anahisi analengwa yeye, kwamba hapo sasa anajitetea.

Wengi hatujui idadi ya maadui wa mgonjwa wa kuweza kumpa sumu au kwamba hana adui kabisa wa kumpa sumu. Hata mtu akisema amenywesha sumu sawa au amelogwa ni kawaida ya utamaduni ya mwafirika mtu akipatikana na ugonjwa usio wa kawaida na unasumbua vichwa na ili wapumzike kuumiza vichwa wanasema huyu amelogwa (sawa na amenyweshwa sumu). Tusubiri madaktari wamalize utafiti wao, yaani waseme anaugua ugonjwa gani na chanzo chake. Tumuombee apone.
 
Watanzania tunapenda kujaji kabla ya kusikiliza kesi yenyewe ambayo inataka ushahidi wa kutosha ili kumtia mtu hatiani. Wakati maumba anshutumiwa kaingilia haki ya Mgojwa kwa kusema hakupewa sumu iweje nae Sitta aseme moja kwa moja kwamba kapewa sumu au yeye haingilii haki ya mgonjwa?
Hata kama swala la kupewa sumu lipo je Mwakyembe maadui wake ni hao wanaotajwa kuwa Mafisadi tu na hakuna uwezekan wa mwingine yeyote ambaye ana conflict nae katika nyanja yeyote ile?
Hapa ushahidi wa kutosheleza ndio kitu muhimu. Labda swali kuu liwe ni nani anayeweza kutoa ushahidi wa kutosha ambao utakuwa wa kuaminika?

Mimi naona kwa Tanzania hii mtuhumiwa akiwa polisi haki huwa haipo lamuhimu ni Sitta kumfikisha Manumba mahakamani kwa kutoa taarifa za uongo hapo atakuwa ametenda haki,Japo awali nimesema hakuna haki itakayo patikana kama mshitakiwa ni polisi lakini kwa kuwa wote wanamamlaka serikalini labda haki inaweza kupatikana.
 
What happens to Po-210 after it enters the body?
Between 50% and 90% of ingested Po-210 passes thru the gastrointestinal (GI) tract and leaves the body in the feces. The retained amount enters the bloodstream where it concentrates in the soft tissues. Approximately 45% of ingested Po-210 is deposited in the spleen, kidneys, and liver; 10% is deposited in the bone marrow and the remainder is distributed throughout the body. Within the bloodstream, Po-210 combines with hemoglobin.
 
sasa sita wasaidie wananchi na polisi basi kutaja jina la mtuhumiwa kusema tu kalishwa sumu si kumtetea,mshauri ndugu yako swape waandishi ripoti yote kuna wasomi wengi tu wataidadavua, sita umegeuka kasuku anae kariria maneno k alishwa sumu,sumu,sumu inawezekana unasema ukweli sasa kama huendibele zaidi ya hapo titakupuuza

tiss/a001
 
MH sitta una chuki ya asili.unaipotosha jamii.tutajie basi huyo alompa sumu,sasa unapong'ang'ania ivo af hutuambii mhusika unataka tufanyeje sisi wanakijiji tuohangaika na kuuza mchicha ili watoto wetu wapate kula.
 
Back
Top Bottom