Sitta: Siogopi kushitakiwa

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,723
hdp_newspaper_icon.png


[h=1]Sitta: Siogopi kushtakiwa kwa kumtetea Mwakyembe
url.gif
[/h]
[h=3] Mwananchi, Mon, 20 Feb 2012 15:36:02[/h]
[h=2] Waandishi wetu, Dar na mikoani

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema haogopi kupelekwa mahakamani kutokana na kutamka kuwa Dk Harrison Mwakyembe amelishwa sumu, kwak sababu ana ushahidi wa kutosha.

Kauli hiyo ni mwendelezo wa mjadala mzito unaotikisa nchi kwa sasa baada ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, kusema polisi wameandaa jalada la kumpeleka mahakamani waziri huyo kutokana na madai hayo.Akizungumza kwa njia ya simu jana, Wwaziri Sitta alisema kama Dk Mwakyembe amedai kuwa, ripoti ya daktari wake inaonyesha kuna kitu kwenye ndani ya mifupa kinachochea hali aliyonayo, yeye anapelekwa mahakamani kwa kosa lipi.

Tayari, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda, amemruka Manumba akisema hatambui ripoti ambayo aliitoa kwa waandishi, ambayo inaonyesha Dk Mwakyembe hakunyweshwa sumu.

Sitta akisisitizia kwamba Dk Mwakyembe kapewa sumu, alisema kutokana na hali hiyo yupo tayari kwa lolote katika hilo na kwamba, anasubiri jalada hilo lipelekwe mahakamani ambako ndiko kwenye uamuzi wa kisheria.“Ukiwa mwanasheria huwezi kuogopa mahakama, mimi ni mwanasheria namba 384 wa Mahakama Kuu.

"Nimesajiliwa kisheria na natambulika kwenye vyama vya wanasheria. Niko tayari kwa lolote litakalotokea kuhusu hilo na siwezi kuogopa kwa kusema ukweli,”alisisitiza Sitta.
Aliongeza kuwa anachotakiwa kufanya DCI, ni kuwasiliana na viongozi wake wa juu akiwamo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili aweze kuwapa taarifa hizo na kuwasilisha jalada hilo mahakamani.

Sitta alisema licha ya hilo, anashindwa kuelewa kosa linalompeleka mahakamani, ikiwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Mponda amemkana na Mkuu wake wa kazi ( IGP), Said Mwema.Alisema Dk Mwakyembe mwenyewe ametoa ufafanuzi kuhusu suala hilo na kumwambia DCI alikopata mamlaka ya kutoa tamko kuhusu afya yake,hivyo basi anasubiri jalada hilo lipelekwe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), ili afikishwe mahakamani.
Alisema anachotakiwa Manumba ni kutekeleza kile alichokusudia ili aweze kufanikiwa, kutokana na hali hiyo anasubiri uamuzi huo.

“Ni kichekesho bwana, we unafikiri mimi naogopa kupelekwa mahakamani kwa hili? Hata siku moja... niko kwa ajili ya kusema ukweli, nitasema ukweli daima na wala siogopi kwenda mahakamani, nashindwa kumwelewa huyu bwana, tena muulize Manumba ameshawasiliana na viongozi wangu wa juu maana sheria zinasema anapaswa kuwasiliana nao kabla ya kuwasilisha jalada lake mahakamani,”alisema.
[/h]
 
Manumba Katokota! kashindwa kuwachukulia hatua wauwaji, pengine naye alihusika katika mpango mzima wa kumpoteza Dr Mwak.
 
Back
Top Bottom