Sitta: Nipeni miaka mitano tu

Sitta: Nipeni miaka mitano tu

Cardinal06

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
963
Reaction score
327
Mhe.jpg

Idadi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaotangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, imeendelea kuongezeka baada ya Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta naye kutangaza jana.

Waziri Sitta, alitangaza nia yake katika Ikulu ndogo ya Itetemea mkoani Tabora, huku akiomba chama chake kimpitishe na Watanzania kumpa miaka mitano tu ya kufanya mageuzi makubwa ya kiutawala. "Tofauti na wenzangu wanaotaka urais kwa miaka 10, mimi nataka kutumikia nafasi hii kwa miaka mitano tu itakayoniwezesha kutatua changamoto zilizopo," alisema.

Alitaja sababu tano zilizomsukuma kuwania nafasi hiyo, ambazo ni mifarakano ya Muungano, mchakato wa Katiba Mpya, mfumo wenye motisha kwa wote ili kuchochea uchumi endelevu na wa viwanda, mikakati ya kupambana na rushwa na kuimarisha uchumi wa CCM.

Sitta aliyejigamba kuwa na uzoefu mkubwa ndani yaCCM kwa kuwa mbunge miaka 30, alisema katika muda huo amejifunza mambo mengi katika uongozi wa kisiasa, hivyo hafikirii kushindwa katika kinyang'anyiro hicho. "Kugombea nafasi ya urais wa nchi yetu, si jambo jepesi linahitaji tafakuri ya kina ukizingatia nafasi hii inabeba matumaini ya Watanzania wote milioni 45," alisema.

Sitta aliyesimikwa kuwa mkuu wa wajukuu wa Chifu Abdallah Fundikira, alisema akichaguliwa kuwania urais na kukiongoza chama chake, atatumia uzoefu wa miaka tisa na miezi sita akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kuziunganisha shughuli za uchumi za chama nawawekezaji makini ili kupunguza utegemezi.

"Chama ili kiwe madhubuti ni wajibu wa mwenyekiti kuhakikisha vitengo na vitega uchumi vinakuwa na tija inayokiwezesha kuendesha shughuli zake kwa kujitegemea… chama tawala kilicho imara kiuchumi kitakuwa na watendaji wanaofanya kazi zao kwa kujiamini na kuisimamia Serikali ili itimize wajibu wake kwa wananchi."Kitakuwa na ufanisi zaidi kuendesha shughuli zake, bila kujidhalilisha kwa kuomba misaada kutoka kwa matajiri," alisema.

MUUNGANO
Kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Sitta alisema ameona nyufa kutokana na kila pande kutoa kauli na vitendo vinavyoashiria utengano."Tunashuhudia wanasiasa wanatuhumu Zanzibar kuwa itanufaika kama ikijitenga na kuwa nchi bila yakuwa sehemu ya Muungano… baadhi ya wabara wanasema watu wa Zanzibar ni wakorofi wasioridhika na kinachofanywa na Muungano na wanahisi mfumo uliopo unaipendelea… kiongozi anayeweza kutatua hili lazima awe na uelewa wa kutosha wa asili," alisema.

Alisema ushiriki wake tangu awamu ya kwanza ya utawala wa taifa hili chini ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, unamuweka katika nafasi nzuri ya kuongoza mchakato utakaowezesha kuzijadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto za Muungano.

MCHAKATO WA KATIBA
Kuhusu mchakato wa Katiba, alisema pamoja na kutokuwa na mwafaka kamili wa kutopatikana, Katiba Inayopendekezwa ina maeneo mengi ya msingi."Binafsi naamini pande zinazosigana kuhusu Katiba Inayopendekezwa zina wazalendo ambao wanaweza kukubaliana kuwa na kipindi cha mpito cha utulivu na maelewano kitakachotuwezesha kama taifa kusonga mbele," alisema.Alitoa ushauri kwa viongozi wa kisiasa na jamii, washawishike kukubali kutokuwa na mshindi wala mshindwa.

MOTISHA KWA WOTE
Sitta alisema atahakikisha anakuza uchumi kwa kasi na kupunguza umasikini unaowakabili Watanzania.Alisema ili kukabiliana na tatizo hilo, bajeti ya Serikali itajengewa uwezo wa kutosheleza tena wenye ubora zaidi ili huduma za jamii kama vile afya, elimu na maji viweze kupatikana kirahisi.Sitta alisema kuna kila sababu kuubadili mfumo wa uendeshaji nchi uwe ni wa motisha kwa wazalisha mali.

"Mifumo ya nchi zilizopiga hatua kubwa za maendeleo duniani ni ile iliyoweka mazingira chanya ya kuaminiana baina ya Serikali na sekta binafsi, hapa kwetu halijatimia. "Watendaji serikalini wanawatazama wafanyabiashara, hawa hawana uzalendo na ni wakwepa kodi, wamejenga mazoea ya kutoa rushwa," alisema.

RUSHWA
Alisema rushwa kubwa zimekuwa na athari kubwa kwa uchumi wa nchi, kutokana na mikataba mibovu ya huduma na mauzo, manunuzi hewa, manunuzi yaliyojaa unyonyaji, uteuzi wa wazabuni na upatikanaji wa ajira, vimesababisha hasara ya mabilioni ya fedha."Nitahakikisha hatuna budi kutunga sheria itakayotenganisha biashara na uongozi ili mtu achague kimoja kati ya biashara au uongozi wa siasa.

"Kama mfanyabiashara atataka kuingia katika uongozi wa siasa, itabidi akabidhi mali na biashara zake kwa mdhamini atakayeendesha biashara hizo wakati mhusika anatumikia umma," alisema. Alisema atahakikisha miiko ya uongozi inarejeshwa na kutungiwa sheria ili kudhibiti ufisadi, hatua ya pili itakuwa kutunga sheria mpya zilizo kali na ambazo zitakuwa na matokeo ya kumzuia mtu asitamani kusaka rushwa.

Sitta alisema mali za viongozi zitamkwe kwa uwazi, mali isiyolingana na kipato na kukosa maelezo ya kutosheleza itaifishwe, kesi za rushwa ziwe na utaratibu wenye uwazi, tume inayoshughulikia maadili ya viongozi ipewe nguvu kubwa za uchunguzi ambayo itafuatilia mali za viongozi bila kuzuiliwa na mamlaka yoyote. Alisema tume hiyo itafanya kazi zake kwa kuweka mambo wazi kuhusu watuhumiwa, tuhuma zao, majibu yao na hatua zinazofuata.Sitta alisema adhabu ya utoaji na upokeaji rushwa lazima iwe kali na iambatane na mali zilizothibitika kupatikana kwa rushwa kutaifishwa.

UZOEFU WAKE
Historia inaonyesha kuwa Sitta amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwamo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) mwaka 1987, Katibu wa CCM Mkoa Iringa na Kilimanjaro.Pia alikuwa Spika wa Bunge la Tisa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM mwaka 2005-2010.

Chanzo: Mtanzania
 
kama ukiniambia ni nani ndani ya CCM, mwenye uthubutu wa kubadilisha mfumo wa kiuongozi ni Sitta peke yake. Lakini bahati mbaya na sijui kama ndio kusudi la Mungu, Sitta amejichafua sana alipoingizwa mkenge kwenye swala la katiba. JK ni mtaalamu wa kutega watu na katika suala la katiba amefanikisha kumuingiza mkenge Sitta.

Sitta alitumiwa na chama chake katika suala la katiba maana waliamini ni mtu shujaa na shupavu ambae akiamua kukomalia jambo hamna wa kumuondosha hapo. Sasa anetumiwa tu kama toilet paper na sidhani kama waliomtega watampa walichomwahidi.

CCM kaeni pembeni sasa. Habari ya mjini ni UKAWA. UKAWA ndio jibu la umasikini tuliotengenezewa na mfumoccm.
 
Watanzania hatupo tiyari kuitoa sadaka nchi yetu kirahisi namna hiyo. CCM mpaka sasa hawana mtu mwenye sifa za kuwa Rais
 
Watanzania hatupo tiyari kuitoa sadaka nchi yetu kirahisi namna hiyo. CCM mpaka sasa hawana mtu mwenye sifa za kuwa Rais

Mna uhakika chama hiki hakitobadilika ndani ya miaka mitano ijayo??
 
Aoni kuwa anajizalikisha kwan kasema mwenyewe ametumikia TAIFA kwa zaidi ya miaka30 akiwa Mbunge ssa swali ndan ya hyo miaka ya utumishi wake kipa kizuri na cha maana kwa raifa amekifanya ili atushawish watz kumwamini maneno yake 30 umeshindwa je 5ndo uweze tehh hyo ngonjera
 
kama ukiniambia ni nani ndani ya ccm mwenye uthubutu wa kubadilisha mfumo wa kiuongozi ni Sitta peke yake. lakini bahati mbaya na sijui kama ndio kusudi la Mungu Sitta amejichafua sana alipoingizwa mkenge kwenye swala la katiba.
jk ni mtaalamu wa kutega watu na ktk suala la katiba amefanikisha kumuingiza mkenge Sitta. Sitta alitumiwa na chama chake ktk suala la katiba maana waliamini ni mtu shujaa na shupavu ambae akiamua kukomalia jambo hamna wa kumuondosha hapo. sasa anetumiwa tu kama toilet paper na sidhani kama waliomtega watampa walichomwahidi.
ccm kaeni pembeni sasa. habari ya mjini ni UKAWA. ukawa ndio jibu la umasikini tuliotengenezewa na mfumoccm.

Hapo umenena man Kiby maaana wajaa wamejitoa ufahamu kuwa walishaharibu
 
Last edited by a moderator:
ungeikubali CDM 2010, leo hii tungelikuwa tunajiandaa tu kukuapisha mwezi October kupitia UKAWA!!

ulichemka kuchanga karata zako vizuri.
 
haa haa kama amekuwa serikalini kwa muda wote tangu uhuru ataweza kwa muda wa miaka mitano? ndani ya ccm hakuna wa kuleta mabadiko kamwe. lao nimoja kinachoendelea ni ulaghai tu kwa watanzania.
 
Mna uhakika chama hiki hakitobadilika ndani ya miaka mitano ijayo??


ni ngumu sana mkuu, kama wameshindwa kwa miaka 50 na zaidi kutokea Uhuru sembuse miaka 5 ambayo ni mara kumi zaidi...


Nasema ni ngumu..
 
Comes rain comes Sun, Sitta tangu alipochakachua mchakato wa Katiba mpya hata aseme ameshukiwa na Yesu Kristo SITAMUAMINI kamwe.

Kitendo alichofanya Sitta kwenye BMK hastahili hata MSAMAHA wa watnzania. He should go to hell.
 
Comes rain comes Sun, Sitta tangu alipochakachua mchakato wa Katiba mpya hata aseme ameshukiwa na Yesu Kristo SITAMUAMINI kamwe.

Kitendo alichofanya Sitta kwenye BMK hastahili hata MSAMAHA wa watnzania. He should go to hell.

Viwango na Kasi mkuu
 
ni ngumu sana mkuu, kama wameshindwa kwa miaka 50 na zaidi kutokea Uhuru sembuse miaka 5 ambayo ni mara kumi zaidi...


Nasema ni ngumu..

Mabadiliko ukiyataka hata ndani ya mwez mmoja unaweza mkuu.....ni mipango na committment tu.
 
Mabadiliko ukiyataka hata ndani ya mwez mmoja unaweza mkuu.....ni mipango na committment tu.

commitment ya miaka mitano kwa nchi iliyokwisha kuoza kila Idara kama Tz ni Serikali mpya inahitajika kufumua uozo wote wa CCM wa miaka 50 na kusimamisha Serikali makini ambayo si nyingine kwa sasa bali ni UKAWA Pekee watakaoweza kuleta mabadiliko ya kweli.
 
Sitta hafai ni fisadi na mchumia tumbo,uliweza bunge la tisa ila serikali ikaona ngoja ikuaribie kupitia Bunge la katiba na kweli ukaharibu sifa yako yote.
 
Kwa mantiki hiyohiyo ya ushujaa wabjuthubutu kufanya mabaya ni wazi kuea hafai, kama alitumiwa na chama kwa maslahi ya wachache na yuko ndani ya chama kilichomtumia kukandamiza maoni ya watu, akienda ikulu atakandamiza zaidi watu hao milioni 45, haeatakuwa na matumaini kabisa chini ya sitta
 
Back
Top Bottom