Sitta chukua hatua

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Kwa muda mrefu spika sitta amesikika mara kadhaa akiipinga serikali hadharani.mojawapo ya masuala anayoyapinga ni malipo kwa kampuni ya dowans. Kinachonishangaza mzee huyu amebakia kulalamika bila kuchukua hatua, hana tofauti na mwananchi wa kawaida ambaye hana uwezo wa kukaa meza moja na JK.

Sitta kwa nafasi yake alitakiwa kumshauri au kumshawishi mh raisi kwamba kuilipa dowans ni ufisadi. Sina hakika kama alishawahi kumuandikia barua JK au kupeleka hoja binafsi kwenye cabinet kuhusu suala la dowans.

Kama ikishindikana kwenye cabinet basi Sitta afanye maamuzi magumu mfano kuongoza maandamano ya wanaharakati dhidi ya dowans,kuanzisha chama cha upinzani au kuhamia chama cha upinzani chenye nguvu kama chadema.kuendelea kupiga kelele kwenye T.V na magazeti ni kujitafutia umaarufu tu.

Nashauri mzee sitta aamue kunyoa au kusuka kwa vitendo na sio kuuma na kupuliza kama hawezi akae kimya ashughulikie mambo ya EAC.

Najua mzee huyu huwa anapitia humu jamvini kama mimi,hata kama hapiti naomba mumfikishie salamu kwa niaba yangu.

Jingalao
 
naona umepata dua kutoka kwa wanazuoni wa kiislamu.
 
kubwabwaja ndani ya ITV hakusaidii.sitta jivue gamba acha manunguniko
 
una muda wa kutosha kuchukua hatua kabla hujachukuliwa!
 
Huyu mzee na rafiki yake Mwakyembe ni wanafiki wakubwa na wachumia tumbo. Mwakyembe kwa kauli yake mwenyewe bungeni alikiri kuficha baadhi ya mambo katika ripoti yake ya richmond ili kuinusuru serikali ya CCM isianguke. Sitta naye akatoa mchango wake kuinusuru serikali kwa kuuzima mjadala wa richmond kihuni.Hawa wanafiki wawili wasingetumia matumbo yao kufikiri na kutanguliza masilahi ya watz leo hii kusingekuwa na hili jinamizi la dowans kwani mchezo wote ungeishia pale bunge na hata JK asingekuwa pale magogoni. Sitta afunge domo lake kwani yeye ni sehemu ya jinamizi hili. UKICHEKA NA NYANI UTAVUNA MABUA.
 
All in all kama alilijua hili wakati richmond inanunuliwa na dowans na dowans kuchukuwa hiyo sabuni si alikuwa bado spika na alikuwa kwenye pozishen nzuri ya kuuwaka mezani ndani ya bunge ktk mkataba huo wa dowans na serikali, kwanini asubirie mambo yakishaharibika ndo aanze kupinga kwakuishia kwenye vyombo vya habari pasipojuchukua hatu?
 
Kwa muda mrefu spika sitta amesikika mara kadhaa akiipinga serikali hadharani.mojawapo ya masuala anayoyapinga ni malipo kwa kampuni ya dowans. Kinachonishangaza mzee huyu amebakia kulalamika bila kuchukua hatua, hana tofauti na mwananchi wa kawaida ambaye hana uwezo wa kukaa meza moja na JK.

Sitta kwa nafasi yake alitakiwa kumshauri au kumshawishi mh raisi kwamba kuilipa dowans ni ufisadi. Sina hakika kama alishawahi kumuandikia barua JK au kupeleka hoja binafsi kwenye cabinet kuhusu suala la dowans.

Kama ikishindikana kwenye cabinet basi Sitta afanye maamuzi magumu mfano kuongoza maandamano ya wanaharakati dhidi ya dowans,kuanzisha chama cha upinzani au kuhamia chama cha upinzani chenye nguvu kama chadema.kuendelea kupiga kelele kwenye T.V na magazeti ni kujitafutia umaarufu tu.

Nashauri mzee sitta aamue kunyoa au kusuka kwa vitendo na sio kuuma na kupuliza kama hawezi akae kimya ashughulikie mambo ya EAC.

Najua mzee huyu huwa anapitia humu jamvini kama mimi,hata kama hapiti naomba mumfikishie salamu kwa niaba yangu.

Jingalao
Sita ni mnafiki tu, nakuunga mkono! Hana msaada wowote kwenye hlo suala
 
Back
Top Bottom