Sitta: Bunge liombewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Bunge liombewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Selous, Jun 24, 2008.

 1. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  2008-06-24
  By Guardian Reporter, Dodoma


  National Assembly Speaker Samuel Sitta has called for prayers for the august House as it passes through a difficult period.

  He told hundreds of believers attending a weeklong religious seminar on `Strategies for Owning and Managing the Economy through Prayers` which ended here on Sunday evening that some legislators who fought for justice were being targeted.

  Sitta, however, expressed hope that such MPs and the National Assembly would eventually triumph.

  The facilitator and preacher of the seminar, Christopher Mwakasege, welcomed the Speaker who was among MPs attending the seminar to speak to the audience.

  The Speaker, likening the situation which the said MPs and the House were passing through with tribulations which the Biblical Job suffered, said just as Job emerged victorious from the devil's attacks, pro-justice MPs would eventually prevail.

  ``Some of the MPs who are pro justice are under attack. Ultimately, we will rise above evil,`` he said, quoting from the book of Job: ``I know that my Protector lives; and that He will eventually reign over the land.``

  In his teachings, Mwakasege said: ``Don`t feed your hunger, feed your vision.

  Even if you are in a position of leadership, you have to realise that God wants to use you, but what you `eat,` the people you associate with can ruin your relationship with God,`` he said.

  He gave an example of a boxer and a legislator saying, a boxer had a special menu that empowered him to fight.

  Mwakasege said an MP had to compare his campaign statements with his behaviour two years after being elected.

  ``If he changes for worse and does not care about the electorate, it may be because what he eats and people he associates with have corrupted him,`` he said.

  Mwakasege said there must be something that the MP had eaten or people he was associating with that could corrupt him.

  He said if a legislator was corrupt and associated himself with dishonest individuals, his behaviour would also change and he would lose the ability to make rational decisions and ultimately descend to injustice.

  Mwakasege said: ``Where are you? What have you eaten? Why is your presence not felt? Why are you not open about what you believe in?`` he asked.

  Quoting from the Book of Daniel and Psalm 1, Mwakasege urged people to be careful with what they ate and their choice of friends, lest they lost their direction in life and angered God.


  SOURCE: Guardian
   
 2. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ambaye hakusikia mifano mizuri ya Mwakasege anitafute otherwise atumie busara kuamua
   
 3. S

  Sam JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2008
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sitta: Bunge liombewe

  2008-06-24 12:20:46
  Na Boniface Luhanga, Dodoma


  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Samuel Sitta, amewaasa waumini wa dini mbalimbali nchini, kuwaombea wabunge wanaoshambuliwa kutokana na kupigania haki.

  Spika Sitta amesema waumini hao wanapaswa kufanya maombi hayo kwa kuwa Bunge kwa wakati huu linapita katika kipindi kigumu.

  Alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa kuhitimisha semina ya wiki moja ya Neno la Mungu kama ilivyofundishwa na Mwalimu Christopher Mwakasege.

  Mwalimu Mwakasege, alimkaribisha Spika Sitta kutoa salamu kwa washiriki wa semina hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri, mjini hapa.

  Bila kuwataja majina, Bw. Sitta alisema baadhi ya wabunge wanaopigania haki wanashambuliwa, hivyo maombi ni muhimu.

  ``Baadhi ya wale wanaosema haki wanashambuliwa, lakini tutashinda,``alisema Spika mbele ya maelfu ya waumini waliokuwa wakisikiliza Neno la Mungu.

  Akimnukuu Ayubu wa kwenye Biblia, Spika Sitta alisema: ``Lakini mteteaji wangu yu hai, na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.``

  Mbali ya Spika Sitta, pia wabunge kadhaa walihudhuria siku hiyo ya mwisho ya semina hiyo ya Neno la Mungu.

  Tangu kuibuliwa kwa sakata la mafisadi wanaotuhumiwa kuchota fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na mkataba wa uzalishaji umeme wa kampuni Richmond, baadhi ya wabunge wamejitokeza kulipigia kelele suala hilo huku wengine wakitaka wahusika wabanwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Katika semina hiyo, Mwalimu Mwakasege aliwafundisha Wakristo mikakati ya kumiliki na kutawala kwa kutumia maombi.

  Aidha, katika mafundisho yake juzi, Mwalimu Mwakasege aliwaasa Wakristo kuchunga mno aina ya chakula wanachokula na marafiki wanaokuwa nao.

  Alifafanua kuwa, chakula na marafiki wanaweza wakasababisha mahusiano yao na Mungu yaharibike.

  Alisema kwa mwombaji, akibadilisha aina ya chakula anachokula, anaweza kushindwa kuomba.
  Kwa upande wa viongozi wakiwemo wabunge, Bw. Mwakasege alisema mara nyingi hubadilika kutokana na aina ya chakula wanachokula na aina ya marafiki wanaokuwa nao.

  ``Mwangalie mbunge katika kipindi cha miaka miwili baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo, anakuwaje� Kuna vitu amekula kwenye ile nafasi,`` alisema.

  Bw. Mwakasege aliongeza vivyo hivyo kwa kiongozi aliyekula rushwa ambapo hubadilika baada ya muda.

  ``Anapoteza hukumu ya haki� Bila shaka kuna kitu amekula au anashirikiana na baadhi ya watu,`` alisisitiza.

  Bw. Mwakasege jana alitinga Bungeni na kutambulishwa na Spika kuwa ni mgeni wake. Alimsifia kwamba alimsikia akitoa mafundisho mazuri alipohudhuria mahubiri yake.
   
 4. S

  Sam JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2008
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkandara,
  Unaonaje wazo hili. Nadhani limekaa sawa. Shusha dua zako mzee.
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,981
  Trophy Points: 280
  Wazo hili nililitoa last week!
  Naona SPIKA KAFUATA USHAURI!
  APEWE USHIRIKIANO BILA KUJALI VYAMA!
  HOJA SI HOJA NI YA NANI...BALI NCHI IRUDISHWE KWA WANANCHI!
  Na huyo mbunge aliyetajwa hapo ni nani?
   
 6. K

  Koba JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ..yaani these bastard na kutuibia kote mpaka kuimaliza nchi leo yanataka tuyaombee? kwa lipi jema walilofanya zaidi ya kujipa magari ambayo hata senators wa States hawaendeshi na mishahara mizito mizito huku wakiendelea kubariki ufisadi kila siku.
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,981
  Trophy Points: 280
  Kitendo cha SPIKA NI CHA KUUNGWA MKONO.
  Kwani na yeye anataka hoja zijadiliwe na si habari za ZIMBABWE!
  Hivi we unafikiri ni kitendo cha kawaida kwa spika kutoa kauli kama hiyo?
  We hujui hata maisha yake yamo hatarini mara baada ya kuwekewa uchawi?
   
 8. S

  Sam JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2008
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mzee soma vizuri habari.
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,981
  Trophy Points: 280
  Sam wape mambo maana na wewe ushachungulia dili!
  SIMAMIA HAKI YA MTANZANIA SAM!
  SAFI SANA NDUGU YANGU!
  KWELI TUTASHINDA!
  JULY THE 4TH IS AROUND THE CORNER.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,981
  Trophy Points: 280
  Ule unga unga ni wazi kuwa haukuwa sumu!
  Na kama thats the case...Then wanahitaji waombewe bila kujali ni dini gani!
  Watanzania waombeeni wabunge wazalendo ili nchi isiende kubaya.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jun 25, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  tutawaombe ile dua tuliyowaombea mwaka jana! Natafuta tarehe nzuri tu..
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,981
  Trophy Points: 280
  Walirogwa mwaka jana?
  Mi nafikiri kuna kitu spika anaficha na ndio maana nikaomba atoe ile ripoti ya unga unga!
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  Nani anataka kuwaombea watetezi wa mafisadi!!!? :(
  Hili bunge halina faida yoyote kwa Watanzania, halafu bila haya wala aibu wanataka tuwaombee!!! Ama kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa!!!!
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,981
  Trophy Points: 280
  Bunge halina maana kwasababu hoja si ya Killango na ccm?
  Acheni kauli zenu hizo!
  Mlikuwa mashabiki hadi muda umepita mwingi hapa wa kukata issue na sasa mnajidai mlikuwa right!
  Msiturudishe nyuma!
  Kama mnarudi huko rudini na sisi tuendelee kuwatandikia mbali!
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  total crap! sita anataka kuturudisha wananchi kwa mungu ili hao wabunge 'wanaotishwa' wakishindwa kufanya kazi zao asema mungu hakutaka au dua zetu za kuwaombea hazikukubaliwa.

  sita afanye kazi yake ya kisheria, mambo ya mungu awaachie wananchi wafanye kwa khiari yao. ikiwa wananchi hawaamini mungu jee?
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  Mie shabiki wa Sita? tangu lini? Kusema Kilango apewe muda haina maana ya kushabikia CCM na Bunge uchwara bali ilikuwa ni kutoa nafasi tuone huyu mama kama angeweza kweli kufurukuta ndani ya Bunge na kuleta yale ambao Watanzania wengi tunataka tuyaone yakitokea ndani ya Bunge hilo na uongozi mzima wa serikali kuhusiana na mafisadi. Hebu kasome postings zangu mbali mbali hapa uone kama kuna hata siku moja niliitetea CCM au bunge hili uchwara.
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,981
  Trophy Points: 280
  Nani kasema habari za sitta?
  MWK alisimamisha shilingi kwa takriban siku mbili hapa jf!
  Je unajua muda tuliopoteza kukata issue?
  Na wewe ndio umegundua kuwa alichokuwa akisema mama ni pumba?
  Tatizo nyie ni wafuasi na mtaiharibu jf!
  Fagilieni hoja na si kujuana!
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0

  MWK alipoleta hiyo hoja hukulazimishwa wewe au wengine kuchangia.
  Jmushi pia na wewe huwa unaleta hoja ambazo hazina maana ambazo zimejaa posts zako mwenyewe.
  jee atakayechangia kwenye hoja yako nae tumseme anatetea ccm?

  acha ku attack watu bila sababu za msingi.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  Jifunze kutumia lugha ya kistaarabu!! Utafungiwa mara ngapi katika ukumbi huu wewe mtu mmoja? Na utajenga maadui wangapi kwa lugha zako za ajabu ajabu? Hili ni ombi tu unaweza kulifuata au la.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,981
  Trophy Points: 280
  Kama unataka chonga tu!
  Siko hapa kwa majungu!
  UNAFIKI WACHA!
   
Loading...