Sitta awashukia maadui wake: Amwita mmoja "Mhalifu sugu"!

Haya maneno ya Sitta ni mazito, kuwa muwazi na Mungu akulinde.
SITTA anatakiwa kuwa muwazi na sio kuongea maneno ya kufikirika.
Anatafuta huruma ya wapiga kura wake, maana sasa kapata mpizani wa kumng'oa 2010.
Kama kweli hao watu wapo na anawafahamu si awataje kwa majina na sio Hadithi za kufikirika? Mbona Slaa alimtaja mpa Rais Kikwete pale mwembe Yanga na wamemfanya nini? Siasa za uoga ndio matnda yake, kama hawezi siasa ajitoe.
Kgwamaka
 
Hivi Spika wa Bunge, chombo kinachotakiwa kuisimamia serikali katika utendaji wake, akianza kulalama kama anavyofanya Mr. Six, tumweleweje ? Ni kwamba hajui jukumu la bunge au ameshindwa kuishawishi bunge kutimiza wajibu wake. Ni majuzi tu kawaonya wabunge wasiisulubishe serikali na kwamba wakikataa kupitisha bajeti, bunge litavunjwa. Kwa maana nyingine anashauri wabunge wafumbie macho mapungufu ya serikali ili waendelee kutumbua kama wabunge. Jamani hivi tunakwenda wapi Mh. Samwel Sitta, Spika wa bunge la Jamhuri ya Tanzania - you can not eat your cake and have it !!

Waziri Mkuu Pinda anawaogopa MEREMETA, IGP Mwema anawaogopa EPA, Mwanasheria Mkuu anawaogopa KAGODA, Mkuu wa TAKUKURU Edward Hosea anawaogopa RICHMOND, Spika Sitta anawaogopa washikaji wa viongozi wa serikali na serikali nayo inawaogopa MAFISADI NA WAHUJUMU wa taifa, astaghafulilah !! Give us a break Mr. Six, rungu mnalo, katiba inawalinda, sheria mnazitunga wenyewe, ridhaa ya wananchi mnayo - tuwape nini zaidi ? Kwa maisha yangu hapa duniani hii ni mara yangu ya kwanza kumwona Spika wa bunge akilialia kama katoto kalikonyimwa kitumbua !!
But then this is Bongo - land of the most absurd !!
 
acheni upumbafu sitta anamuongelea Rostam Aziz

Asante sana kaka nashukuru umekuwa wa kwanza kumention maana swali la Halisi lilikuwa linauliza ni nani anayetajwa na spika Sita lakini watu wamekurupukia kumtolea maneno makali bila kuingia kwenye swali husika, akina GT wamekumbushia hoja zao za madawa ambazo zina miaka miwili sasa wanazipigia kelele tu pasipo sababu na ushahidi mweh....... Hebu jadilini swali husika sio mengine
 
Mhalifu sugu nadhani alikuwa anamtaja yule mbunge wa asili ya asia wanayetoka naye mkoa mmoja
 
Katika gazeti ka Raia Mwema la leo, kuna habari ambayo Spika Sitta, amezungumzia kuhusu majeruhi wa Richmond ambao wamekuwa wakimuandama na katika kufafanua bila kuwataja majina, Spika alisema kuna mmoja kati yao ni MHALIFU SUGU, je, huyu ni nani? Katika maelezo yake Sitta alisema;




Kumbe Sita anayajua yote haya, sasa kwa nini anakuja kusema sasa? Ina maana vyombo vyetu vya usalama, DPP wako wapi kumshughulikia mhalifu sugu? Hata kama Sita ana ya kwake, cha muhimu kakiri kuwa serikali yetu haiwajibiki kwa wananchi bali inawalinda wezi.
 
Sitta nae ana walakini, achague upande tujue. hii ya kukimbilia kwenye media kama mtu ambae hana nafasi ya kutoa tamko au kuchukua hatua sijui tumweke kapu lipi. Achukue hatua kama kiongozi wa mhimili mkuu wa nchi sio kama kina Mengi wafanyabiashara.

Kuwasema watu kimafumbo kama spika ni bonge la udaku unamshushia hadhi. kufanya mahpjiano na Raia mwema halafu unaficha, atuonyeshe kuwa haogopi au akae kimya kama mkuu wa kaya.
 
huyo alleged MHALIFU SUGU ndioye aliyemweka hapo alipo huyo SITTA sasa badala ya kufanya kazi kwa uadilifu naye amegeuka kuwa MHALIFU WA KUPINDUKIA kwa kuanza kufoji risiti za pharmacy....tangu lini dawa za Malaria zikauzwa dola 2,000?

hebu soma hapa:

http://taifaletu.blogspot.com/2009/07/time-to-bin-samuel-sitta.html

kuna mtu kwenye hizo comments kwenye hiyo link amesema kama anajina yuko safi then aje clean tuu kisha aelezee iweje anawaburuza watu wampe tenda kwa kulazimisha kule Dodoma?

That is very cheap my brother or sister as the case may be!
 
Kumbe Sita anayajua yote haya, sasa kwa nini anakuja kusema sasa? Ina maana vyombo vyetu vya usalama, DPP wako wapi kumshughulikia mhalifu sugu? Hata kama Sita ana ya kwake, cha muhimu kakiri kuwa serikali yetu haiwajibiki kwa wananchi bali inawalinda wezi.
Ssssssssssshhhhhhhhhhhhhhhh pole pole bwana. Hata Dr Mwakyembe alisema siku ile kwamba mengine waliyafunika kutoifanya serikali i collapse. Kwa hiyo 6 anajua mengi bwana, ila aliiheshimu serikali yake inayompa ulaji na starehe.
Wakimkologa si hapo anasema?
Na hapa ndipo nadhani Kikwete akae kimya maana yale maneno ya daktari yalikuwa mazito. Akirudia kutetea mafisadi kama alivyofanya siku ile Karimjee kwa kuwalisha uongo wazee wa Dar, atafulia.
 
Sitta acha longolongo.....tamka hayo majina...wacha kulalama bila kuchukua hatua....grow up!
 
Mtindo huu wa kutukanana nje ya mahakama aliuanza Mengi, akafuatia Mwakyembe na Rostam sasa naona Sitta naye!
Tusipoangalia nchi itakuwa na utamaduni wa kusutana kwenye vyombo vya habari.
Rais wa nchi yuko kwenye jumba la kioo...anashindwa kuwashushia mawe watu hawa. Na hilo wote wanalijua...
 
Sitta anazidi kujitia aibu kila anapofungua mdomo wake . Hoja anazojenga ni za kitoto , kwa hiyo jenereta ndio lililosababisha samani za ndani ya nyumba yake iwe milioni 200? Halafu anasema hizo furniture ni mali ya serikali ?... mmmh, Technically nitakubalina naye , lakini mara atakapostaafu zitakuwa zake ! Kusema ukweli hii issue imemshika pabaya na ndio maana imemwingia kichwani ...
 
- Mhhh! maneno ya a sitting National Speaker ni mazito sana na yaangaliwe vizuri hayo, kwa hili nampa pass ahsante kwa kutufungua macho zaidi ingawa hakuna jipya, lakini angalau Spika ahajawa kama kina Msekwa, Mangula na kitine, yaani kusubiri kwanza mlo uishe, huyu amefanya kama ninavyoshauri mara kwa mara hapa JF, sema ukiwa ndani, tena kwenye mlo,

- Kwa hili Spika ubarikiwe na Mungu wa Mbinguni and I love it!

Respect.

FMEs!
 
Ha ha ha h

He he he..


Sasa kumekucha..Lakini mboni haya ya Dowans wakati akina Zitto wanashupalia mitambo inunuliwe yeye mbona hakutoa mwongozo? alikuwa anasubiria nini? Anasubiria mpaka 'ulaji' wake uguswe ndio a-spill the beans?

Ila yote kwa yote wanavyokaangana ni kheri kwetu wapenda nchi..
 
Kwa mnaowafahamu tunaomba Majina ya hao watatu wanaosemwa na spika 6 kwani tuliombali home (Tz) tunahitaji msaada wenu mliokaribu au mnaofahamu ili tuweze kuchangia mada.
 
Mnaouliza majina mnashangaza sana. Kwani hamlijui jopo la mafioso linalojitwalia utajiri wa nchi yetu? au ninyi sio wenzetu?
 
Kama hajasema jipya ina maana hajatufungua macho; labda wewe.

- Amethibitisha na ku-approve tunayoyajua tayari, na hasa kwamba Zitto was wrong kusema Dowans ni good kwa taifa letu.

- Na sio mimi ila ni masilahi ya taifa kwanza, wewe na mimi tunakuja baadaye.

Field Marshall Es!
 
Amethibitisha na ku-approve tunayoyajua tayari

Kama amekuthibitishia ina maana ulikuwa huna hakika, ulikuwa huyajui. Na kama tunayajua, basi hakuna alichotuthibitishia. Halafu hakuna kitu kama "ku-approve tunayoyajua." Ndio nini hicho, Kiswahili, Kikwere, Kiingereza? Watanzania, na Waafrika by extension, wengi wana shida sana ya kujieleza, si raia, si viongozi.

Spika mzima anaongea kwa mafumbo-fumbo, kama mdaku mdaku tu. Unamjua "mhalifu sugu," mtaje! Balls huna.
 
Back
Top Bottom