Sitta awashukia maadui wake: Amwita mmoja "Mhalifu sugu"! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta awashukia maadui wake: Amwita mmoja "Mhalifu sugu"!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 2, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  TUNA IMANI NA MHE. SPIKA, KATIBU WA BUNGE – WATUMISHI WA BUNGE

  Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge wameeleza kuwa wana imani na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambaye wamemuelezea kuwa ni mtu makini asiyetetereka katika kutetea hadhi ya Bunge na Taifa kwa ujumla.

  Akisoma risala kwa niaba ya watumishi wa ofisi hiyo katika sherehe ya wafanyakazi baada ya kumaliza Mkutano wa 16 wa Bunge, Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge, Bwana Angumbwike Ng’wavi alisema kuwa wamesikitishwa na baadhi ya habari zinazozagaa kuwa eti Mheshimiwa Spika anawagawa watumishi wa Bunge, ‘’tunafahamu kuna kundi la watu linalokereka na uhuru wa taasisi ya Bunge unavyokuwa na namna Bunge linavyofanya kazi zake kutokana na sasa Bunge kuwa mstari wa mbele kupambana na uovu uliopo katika jamii yetu. Mtu yeyote anayetetea haki na kupambana na uovu mtu huyo siku zote atakuwa na uadui kutoka kwa wale wanaonufaika na uovu huo’’ alisema Bwana Ng’wavi.

  Aidha, Bwana Ng’wavi alieleleza kuwa mtu mwema kupakwa matope kwa lengo la kumkatisha tamaa siyo kitu cha kushangaza katika ulimwengu huu kwani hata vitabu vitakatifu vinaeleza kuwa Mitume wa Mungu pamoja na mema yote waliyoyatenda bado walipigwa vita na wanadamu. Wengine waliteswa na hata kuuawa.

  ‘’ Wafanyakazi wa Bunge tuna imani na Mheshimiwa Spika na tunapenda kutoa wito kwa Spika kuwa aendelee na ujasiri huo katika vita dhidi ya ufisadi kwani baadaye historia itaonyesha ni nani hasa alikuwa mkweli na mtetezi wa nchi hii na wananchi wake. Kuna mwanafalsa moja aliwahi kusema, kwa lugha ya Kiingereza “If want your name to continue living even after your death do something worth writing or write something worth reading” Kwatafsiri isiyo rasmi mwanafalsafa huyu anasema ukitaka jina lako liendelee kuwa hai hata baada ya kifo chako fanya jambo linalostahili kuandikwa au andika kitu kinachostahiliki kusomwa’’ ilisema sehemu ya risala hiyo.


  Wakizungumzia kuhusu madai kuwa Katibu wa Bunge wa sasa, hana sifa za kushikilia nafasi hiyo, Wafanyakazi hao walisema kuwa wanashangazwa na madai hayo kwa kuwa katibu wa sasa ni mtaalam aliebobea katika masuala ya Bunge na uendeshaji wake, ‘’ Bahati mbaya wanaoeneza hayo hawajafanya utafiti wa kutosha, kwani kama wangefanya utafiti wa kutosha wangegundua kuwa Dk. Thomas Kashililah ana uzoefu wa masuala ya Bunge kwa zaidi ya miaka ishirini akiwa ameshika nyadhifa mbali mbali ikiwemo Ukurugenzi wa Idara nyeti ya MipangO naTeknolojia ya Mawasiliano, Ofisa wa Bajeti, Katibu Mezani, Katibu wa Kamati za Bunge na Afisa Mfawidhi wa Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es salaam’’ ilisema sehemu ya risala hiyo.

  Wafanyakazi hao walisema kuwa Dkt. Kashililah ambae ni daktari wa falsafa ana sifa za kutosha na zimepita sifa za msingi anazopaswa kuwa nazo Katibu wa Bunge na wametoa wito kuwa asikatishwe tamaa na maneno hayo ya uzushi bali aendelee kuchapa kazi na kwa kushirikiana na Mhe. Spika aboreshe mazingira ya kazi na vitendea kazi.

  Hivi karibuni kumekuwa na juhudi zinazofanywa na watu wasiopenda jitihada zinazofanywa na taasisi nyeti ya Bunge kwa kujaribu kuwachafua viongozi wa juu wa taasisi ya Bunge kupitia magazeti na mitandao ambapo Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge limelaani na kusema kuwa sio sahihi hata kidogo.


  Imetumwa na Said Yakubu
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Watanzania hatuna imani kabisa na Spika maana maamuzi yake mengi ni kuikingia kifua Serikali Bungeni kila inapokuwa katika hali ngumu. Amefanya hivyo kwenye mijadala mbali mbali ikiwemo ya Vitambulisho vya Taifa, Richmond, Meremeta n.k. Na huu usanii wa "Tuna imani na Spika na Katibu wa Bunge" nani kautunga!? Spika, Katibu wa Bunge au wote ili kuteea ulaji wao!? Kweli nchi yetu kuna usanii wa hali ya juu.
   
 3. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Sifa nyingi anazozipata SS za kupambana na ufisadi zina walakini. Ni kweli alipambana na akina EL, lakini mfano kama askari anakamata jambazi leo na kesho yake akapokea rushwa kwa jambazi mwingine ili asimkamate, huyo siyo askari mwadilifu, period. Sasa huyu Spika hawezi kujisifu kupigana na ufisadi wakati na yeye ana tuhuma kibao za ufisadi na haruhusu uchunguzi huru.
   
  Last edited: Aug 3, 2009
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Aug 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Uchunguzi huru hautaji kuruhusiwa na Spika; Kuna taratibu za kibunge za kumchunguza na hata kumuondoa Spika. Wale watu wenye ushahidi wa hizo tuhuma wawashawishi kundi kubwa la wabunge wa CCM ili waanze kufuata taratibu hizo za kibunge. Walishafanya uchunguzi huru kuhusu zile tuhuma za matibabu na matumizi ya gari na wakarudi patupu.

  Wabunge wa CCM wakitaka kumchunguza na kumuondoa Spika wanaweza. Kwanini hawafanyi hivyo kama kuna ushahidi mkubwa wa ufisadi wa spika? Ufisadi ambao tunaambiwa ni mkubwa kuliko wa Richmond?
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Mkjj, hawafanyi hivyo kwa sababu wameamua kuweka mbele maslahi ya CCM badala ya yale ya Taifa. Hivyo ndiyo maana Spika anaendelea kupeta na huku akiendeleza unafiki wake mkubwa kwamba naye anapambana na mafisadi wakati yeye mwenyewe ni fisadi na maamuzi yake mengi Bungeni yameikingia kifua Serikali dhidi ya ufisadi mbali mbali uliofanywa na mafisadi ndani ya Serikali.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Aug 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sasa basi utaona tatizo siyo Spika then! Tatizo ni wabunge wa CCM.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Aug 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni beyond wabunge wa CCM! Tatizo ni wananchi watakaowapigia tena kura hao wabunge (akiwemo spika) na kuwarudisha bungeni
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Aug 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  that is pinpointing the exact problem..!
   
 9. S

  Shamu JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hahahaha!! Hao wafanyakazi wa Bunge si wapo kundi moja na huyo mwenzao. Duh, ufisadi, na rushwa ndani ya bongo ni cancer ilyotambaa kila ofisi.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Halafu kuna wanaodhani kwamba katiba mpya itamaliza kabisa matatizo tuliyonayo. CCM haiheshimu katiba yao wenyewe je wataweza kuheshimu katiba ya nchi hata kama tukiwa na katiba mpya!? Angalia hawa mafisadi ndani ya CCM walivyoendelea kukumbatiwa ndani ya chama hicho akina Mkapa, RA, Chenge, Mramba, Msabaha, Lowassa, Karamagi na wengineo wengi.

  Kama CCM ingeamua kufuata yaliyomo ndani ya katiba yao kuhusu watu kama hawa basi wote wangeshafukuzwa CCM siku nyingi sana lakini bado wanapeta tu! Kwa hiyo hata kama tutapata katiba mpya CCM wanaweza kabisa kutoiheshimu na kufanya wanavyotaka ili wabaki madarakani miaka nenda miaka rudi. Nchi yetu jamani ina matatizo makubwa sana.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Aug 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  now you are getting the drift; Katiba mpya haitopatikana na yes nchi yetu ina matatizo makubwa sana!
   
 12. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0


  duh!

  kazi kweli kweli
   
 13. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  wanaolilia katiba mpya hawalili CCM na matatizo yake matter of fact it dont matter who is in power but what we want is power to intervene without, objection whenever we see something is not right. the right to all the available evidence kama mmoja wenu alivyosema wabunge wenyewe awawajibiki mara nyingi na awatumi nguvu zao za wote. hiyo si shuhuli yetu bali sisi ni kuingia sehemu ambazo tuna taka kuingia bila ya kupingwa ni hicho tu kwa inae muhusu.
   
 14. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Hivi maadui wa kisiasa wa Sita ni nani? isiwe kila siku anatuambia kitendawili hichohicho. Anajipa sifa ambayo nadhani hastahili, atufafanulie ni katika lipi amejitengenezea maadui?
   
 15. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Spika huyu huyu kashafanya blunders nyingi hapo bungeni.mnaweza kurejea barua ya Mheshimiwa Adam Malima kumpinga spika ipo humu humu JF.

  Mh.Shelukindo ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya bunge ameshangazwa kuona mhasibu mkuu wa bunge hana sifa za uhasibu ikiwemo CPA.

  SHERIA ya uhasibu inasema kila mahala penye shilingi milioni 20 mhasibu wake awe na elimu ya uhasibu ngazi ya CPA.bunge lina mabilioni ya mapesa anayeshikilia mapesa hayo hana sifa za uhasibu.umakini wa spika uko wapi?

  Katibu wa bunge Thomas Kashilillah akishirikiana na Raphael Nombo wameajiri watu wasio na sifa za kuajiriwa.TENA WOTE ni wahitimu wa chuo kimoja,intake moja.
  Kashilillah ana sifa gani zaidi ya kuwa alipigiwa chapuo na MIzengo PINDA hiyo nafasi kwa vile ni jamaa wake wanatoka wote SUMBAWANGA.

  kama watendaji wetu wangefuata sheria Thomas Kashilillah alitakiwa asiwepo kazini hivi sasa kwa madudu aliyoyafanya.

  ningependa kujua wafanyakazi gani wenye imani na spika? kisheria kungekuwa na majina yao na saini zao kuwa sisi wafuata tuna imani na spika na kashillilah.inawezekan barua hii kaandika Kashillilah kujikosha kwani haina ushahidi kuwa imeandikwa na wafanyakazi wa bunge.

  Kashilillah anadai kuwa ana PhD kama kigezo cha ufanisi wake.viongozi wangapi wana phD na utendaji wao mbaya.ina maana DR.Emmanuel Nchimbi ni mtendaji kuliko Zitto Kabwe kwa vile ana PhD?
   
 16. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mh, naomba kukuuliza maswali yafuatayo naningependa ushauri na majibu yako kwani inaonekana una mawasiliano na baazi ya whistle blowers kutoka nyumbani na una vision yako ya tanzania based on that comment especially kuhusu matatizo makubwa tz.

  kila tatizo linahitaji ubunifu mpya wa kulimaliza na inavyooneka hapa kwetu tz yako mengi maswali yangu ni machache na ningependa kama utani jibu unipe majibu ambayo yatan'goa mizizi sio short term solution na sababu zako hiyo mizizi utain'goa vipi kwa upande wako na jinsi gani uta-prevent kuto jirudia tena baadae?

  1. suala la uongozi mmbovu uliopo na tabia za uongo nani ni responsible na tutahakikisha vipi tunalitatua kwani uongozi mmbovu ndio chanzo cha matatizo (its going to be a poor march if the leader is struggling with the routine)

  2. Suala la ufisadi sio kwa viongozi tu bali it has become part of survival, way of life for many tanzanians its cultural you can argue in a sense sasa upande wako unaona litakwisha vipi iwapo hata askari anaengalia funguo bandarini akiona mida ya kufunga bandarini inakaribia anachelewesha kutoa funguo ili umpe chochote akijua likilala unastorage charge hivyo inabidi tu uonge ili umfurahishe time zikiwa mbaya. sitaki kurudi kwenye passport kwa wale wasio wajua watu mule ndani, na wala awana sauti nyingi, na mtatizo ya traffic na wachukuzi, na watu wa benki kupeana mikopo kwa kujuana na viongozi wenye mikataba ya uongo, na viongozi wanao ji binafshia mali za umma kwa unafuu na mengineo mengi yanayoendelea.

  3. tanzania ni moja ya nchi maskini duniani ingawa inaonesha kuna growth in GDP lakini the sectors involved are mainly due to foreign investmet rather than government home policies and strategies to fight poverty, therefore it seems most who benefit are those with some sort of education and even so its a very small proportion of tznians.

  how do you suppose we could maximise the assets we have after all we have the land, labour and capital to start with kama umenipata.

  4. with poverty ujue kwamba pia kuna tatizo kubwa la ignorance, which leads to most of the problems above. what do you think needs to be done to help ourselves out.

  5. what is your long term vision of tanzania in terms of stability and making sure our future generation wakija waone hope na the right and stable democracy

  Mwisho nimemaliza kama utanijibu mkuu wangu nitashukuru kupata elaborated view ya maswali yangu.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280

  Mkjj, I was born and raised in Tanganyika, therefore I know the whole drift.
   
 18. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  well ukiweza mjibie wewe kwa niaba yake, au hata zitto kama bado yumo
   
 19. O

  OkSIR Senior Member

  #19
  Aug 2, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwizi ni mwizi hata wakikaa nyuma ya mafisadi wataitwa wezi tuuuuuuuuuuuu
   
 20. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hili ndiyo tatizo la hawa viongozi wetu. Kila wananchi wanapohoji wanaambiwa wametumwa na ni maadui wa kisiasa. Yes, wewe ni mwanasiasa na ulishiriki uchaguzi ukiwa na washindani wengine , what do you expect?? Jibu maswali, na hoja zinazotolewa, facts with facts, hii ndio njia pekee ya kuwashinda wapinzani wako, siyo kila siku kulialia tu, naomba ulinzi, siasa za majitaka, nitakuwa spika mtake msitake, honestly, who says that ?
   
Loading...