Sitta awafungulia mashtaka Lowassa, Rostam CCM

Sitta awafungulia mashtaka Lowassa, Rostam CCM

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Ezekiel Kamwaga

Toleo la 334
15 Jan 2014




WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema amewashitaki wanasiasa wenzake, Edward Lowassa na Rostam Aziz, kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo vyao vya kifisadi.



Akizungumza na Raia Mwema juzi Jumatatu, Sitta alisema tayari amewasilisha vielelezo vya ushahidi wake ndani ya chama hicho na anachosubiri kwa sasa ni majibu ya tuhuma zake hizo.
“Tayari nimepeleka maelezo yangu kwenye chama kwa ajili ya kuchukua hatua. Haya mambo ninayoyazungumza kila siku si porojo bali ni ukweli na nina vielelezo vya kuthibitisha hayo na tayari nimevipeleka kwenye chama,” alisema Sitta, mwanasiasa mkongwe ambaye amewahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania.


Sitta hakutaka kuingia undani wa tuhuma alizozitoa kwa maelezo kwamba anasubiri kwanza chama kitoe majibu ya hoja zake.



Katika mazungumzo yake hayo na gazeti hili, Sitta alitamka kwamba ingawa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Rostam Aziz, Mbunge wa zamani wa Igunga na mfanyabiashara tajiri, ndiyo aliowataja kwa tuhuma za ufisadi, anafahamu pia mafisadi wengine walio ndani ya CCM lakini ameamua tu kuwataja hao kwa sasa.



Sitta alikuwa akijibu tuhuma za Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba, aliyezungumza na gazeti hili juzi Jumatatu na kudai kwamba chama hicho hakina mafisadi na kwamba wanaosema hivyo wanakivuruga chama badala ya kukijenga.



Katika maelezo yake, Makamba alisema; “Kama akina Lowassa wangekuwa mafisadi, wangekuwa tayari wamechukuliwa hatua na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) au vyombo vingine vya dola.



“Kama hawajachukuliwa hatua na bado ni viongozi halali waliopitishwa na chama kwenye nyadhifa zao, basi watu hao si mafisadi. Sitta anatakiwa awataje kwa majina mafisadi anaowasema badala ya kulitumia neno hilo kuzungumza kijumlajumla,” alisema.



Akizungumza kwa utulivu, Sitta alisema kisiasa, mtu haondokewi na tuhuma za ufisadi kwa vile tu hajakamatwa na vyombo vya dola au ushahidi dhidi ya tuhuma zake haujapatikana.

“Kwenye siasa, mtu kujulikana kama fisadi au si fisadi hakutokani na kutokamatwa na vyombo husika. Ni tabia ambayo mtu unaionyesha kwa jamii ndiyo inakuwa taswira yako.


“Ndiyo maana, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba mke wa Kaisari hatakiwi kutuhumiwa kwa uchafu. Hata kama hakufanya makosa, kule kutuhumiwa tu ni kubaya.

“Kwa bahati nzuri, namfahamu vizuri Makamba. Nafahamu kwamba ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakipokea pesa kutoka kwa Lowassa na Rostam. Sasa anapokuja hadharani na kuwatetea mimi sioni cha ajabu.


“Watu kama akina Makamba ndiyo wamelea ufisadi katika nchi hii. Ninaposema Makamba ni mlezi wa mafisadi sisemi kwa bahati mbaya bali kwa sababu nafahamu misaada wanayompa,” alisema Sitta.



Akizungumzia suala la kukamatwa kwa mafisadi, Sitta alisema lina ugumu kwa sababu, kwa tabia, mafisadi ni watu wajanja na wanaofanya mambo yao katika usiri mkubwa na wana mahusiano na watu walio katika mfumo.



Alisema kama Tanzania haitakuwa tayari kupambana na mfumo uliopo ambao unalea mafisadi na ufisadi, itakuwa ngumu kupambana na rushwa ambayo alisema ndiyo adui mkuu wa nchi kwa sasa.



Hii si mara ya kwanza kwa wanasiasa kuweka hadharani tuhuma kati yao, mara ya kwanza ilikuwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kudai Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewahi kupewa fedha na Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono ili pamoja na mambo mengine, kumhujumu aliyekuwa mgombea wa CHADEMA Musoma Vijijini katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.



Kutokana na tuhuma hizo, Zitto naye alikuwa mkali akisema anatumaini Mkono pia amemwambia Lissu kwamba Mbowe naye aliwahi kuchota mabilioni kadhaa kutoka Mkono, licha ya Mkono kutambuliwa na chama hicho kuwa ni fisadi.



Katika majibu yake kuhusu tuhuma hizo, Mbowe ambaye ametishia kumshitaki Zitto, alisema kuchukua fedha kutoka kwa yeyote akiwamo Rais Jakaya Kikwete au CCM si tatizo bali tatizo ni nia iliyopo kuhusu fedha
unazochukua.




- See more at: Raia Mwema - Sitta awashitaki Lowassa, Rostam
 
Mimi si mwanasheria, ila kama sheria haimzuii sitta kupeleka mashtaka yake mahakamani.. naye pia asimnyooshee kidole makamba! nayeye analea mafisadi. Sababu anawajua na ushahidi anao, kwann asiwapeleke mahakamani anawashitak kwenye chama!
 
fISADI NDANI YA BARAZA LA MAWAZIRI??????? WHAT SHAME WILL IT BE HAPPEN TO MR KIKWETE!!!!!!!!!!!!!
 
Sita maji shingoni na hana namna yoyote ya kupata faraja hila kwa kutafuta huruma ya watu kupitia mgongo wa Lowasa. Huyo Rostam ni mapitio tu lakini anayemtafuta ni Lowasa. Namwambia atafute chorus nyingine kwa Lowasa hiyo watu wameichoka kwani washajua udhaifu wake, tamaa zake na unafiki wake kupitia migongo ya watu, kwa ufupi hawezi kujibeba hila kuptia mgongoni kwa Lowasa. Hafai hata kidogo. Yeye ni mwanasheria badala ya kwenda kwenye vyombo vya sheria amebaki kulia lia kwenye vyombo vya habari kutia jina la Lowasa. Nakwambia acha watu tunazidi kukuona limbukeni wa kinyamwezi, Lowasa kwako kitu kingine na kama vita ya siasa safi imekushinda jiunge naye, wajajna wako hivyo. Si maneno yangu ni msemo wa Kiingereza ''If you can't fight them join them'' Nina wasiwasi mzee wewe utakufa kwa kihoro kwani nadhani kila mara unaona kivuli cha LOWASA MBELE YAKO NA WALA SI NYUMA YAKO. Tutakunaga tu maana michosho sasa. Sijawahi sikia Lowasa anazungumzumzia mtu, huwa anazungumzia issues (hoja), jifunze hilo kwake basi
 
CCM tumeichoka na dhambi zao zote...
yoyote alienda ndani ya ccm kwangu mimi sehemu ya uhalifu wa nchi hii!!

Sitta ni fisadi kama mafisadi wengine walioko ccm.
 
Maskini Rostam akina Nappe wanambana mbavu

cc FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Huyu Mh. Sitta atuondolee unafiki hapa. Si yeye ndiyo aliyeizima issue ya Richmond BUNGENI wakati akiwa SPIKA? Sasa wanaanza kukanyagana nafasi ya kuwania urais ndiyo anatuletea ngonjera zake.
 
Si Lowassa, Sitta, Sumaye, wala Membe. Hawa wote si chaguo la CCM la urais wanapoteza muda wao bure.
 
Sitta kishaona mambo magumu.

Mzee Sitta, ikiwa waliweza kukung'oa uspika hivi unafikiri una lingine tena utalosema likawa lina maana? Yaani ni aibu sana kwako kile ki dada kukuangusha uspika, wewe sasa kaa ulee vijukuu achana na siasa maji taka.

Hujapona jeraha moja unataka jingine?
 
Kwa kweli CCM yote imeoza kwa Ufisadi, walianza wakiwa wadogo wakota mikia sasa mikia imekatika hat wakiingia shimoni uwezi kuwavuta, kumbuka CCM ni kama ukoo wa panya, baba mwizi, mama mwizi, kaka jambazi.
 
Sita sawa na Mugabe, yupo tayari kusema/kufanya lolote ii mradi aende magogoni. Sitta, Malecela, Mukama, Makamba X2, Membe, Zito, Nchimbi, Lyatonga, Lipumba na Slaa wote ni hasara
 
Hv huyu mzee mda wote alikua wapi.!?au hasira za uspika hazijaisha??
 
Tubuni maana ufalme wa MUNGU umekaribia....!! ndipo mtakopolia na kusaga meno. Mtalia na mafisadi yenu msipate msaada, yatawahonga vijisenti ivo mkiyafanikisha yanawaacha solemba, mtakanyagana na kugombana nyinyi kwa nyinyi msiafikiane kwani na nyinyi pia ni mamburura..!! mnatumia mda mwingi kuchimbana vijembe kila mmoja akitetea upande wake hadi mnatamka na uongo na maneno ya kukufuru! Hakika nawaambia waTZ msipobadilisha mitazamoyenu mtaangamia sababu hamna maarifa zaidi ya kujipendekeza kwa hao wahujumu uchumi wa nchi!
 
Back
Top Bottom