Huyu aliyeandika haya ndiye yuleyule Mufiyakicheko kweli? Au uliamua kutuua kwa kicheko?ENYI MNAOONEKANA KUWA WASAFI NA KUMBE NDANI WACHAFU mko kama maji safi lakini machungu,ambayo kwa kutazamwa kwa nje yanaonekana safi kabisa lakini yakipimwa hakuna hata tone linalokubaliwa. Naam mwonzi wa jua huangukia sawasawa juu ya vumbi au juu ya kioo lakini hutofautiana katika kurudisha nuru kama nyota inavyotofautiana na dunia
Mkuu mbona hueleweki? Hiki ulichoandika ni kiswahili au? Unasoma darasa la ngapi?
Usijali mufiyakicheko umeeleweka na umeleta taarifa muhimu endelea kutujuzasijabahatika kwenda shule ila uliye enda shule inaonekana akili yako haina akili nenda jukwa la ruhga
huyu sitta haelweki
↲Hii umeandikiwa kaka/dadaENYI MNAOONEKANA KUWA WASAFI NA KUMBE NDANI WACHAFU mko kama maji safi lakini machungu,ambayo kwa kutazamwa kwa nje yanaonekana safi kabisa lakini yakipimwa hakuna hata tone linalokubaliwa. Naam mwonzi wa jua huangukia sawasawa juu ya vumbi au juu ya kioo lakini hutofautiana katika kurudisha nuru kama nyota inavyotofautiana na dunia
Unapopost usitetemeke mkubwa,tulia andika kitu chenye maana siyo unaandika utadhani ni mipasho.rudia tena ulikuwa unamaanisha nini?
wewe vipi? kipi kisichoeleweka hapo???? Au umetumwa kuvuruga mada?sijabahatika kwenda shule ila uliye enda shule inaonekana akili yako haina akili nenda jukwa la ruhga
EWE MWANA WA ROHO Hakuna amani yoyote kwako ila tu kwa kujikana mwenyewe na kumgeukia mngu kwani ya kupasa kujitukuza katika jina la mngu na siyo katika jina lako mwenyewe weka imani yako ndani ya mngu wekeza kwa mngu↲Hii umeandikiwa kaka/dada
sita
ameereza nijinsi gani wenye pesa ndani ya ccm walivo kuwa wamepania kumtowa ikashindikana kwamaelezo yake anasema vyama vingine vilimshawishi kugombea uraisi bado alibaki imala anashanga kusakamwa
mimi sihusiki na ccj hao walionifata nyumbani kunitaka nijiunge na vyama yvao leo wananipaka matopo kajifananisha na chuma chapuwa hakuna mwanachama aliye pata misukosuko kama 6 kayaeleza hayo mbeya
chanzo live G fm mbeya
EWE MWANA ANASA ZA DUNIA Ni ya kupendeza milki ya kuwa hai kama ungeifikia ni ya fahari milki ya umilele kama utapita dunia ya mauti ni tamu furaha kuu takatifu kama utakunywa katika kikombe kisichoelezeka kutoka katika mikono ya mngu kama utafikia daraja hili utaokolewa kutoka katika maangamizi ya dhambiAnawahi kuanzisha thread, asije kuta imeanzishwa humu.
Asante mkuu nifani za watuMufiyakicheko,Thread yako ilipaswa isomeke hivi: Sitta ameeleza ni jinsi gani wenye pesa ndani ya CCM walivyo kuwa wamepania kumtoa ikashindikana. Kwa maelezo yake anasema vyama vingine vilimshawishi kugombea Uraisi lakini bado alibaki imara. Anashangaa kwanini anasakamwa! ''Mimi sihusiki na CCJ,hao walionifuata nyumbani kunitaka nijiunge na vyama vyao leo wananipaka matope'' alisema Sitta. Amejifananisha na chuma cha pua na akasema hakuna mwanachama aliye pata misukosuko kama yeye. Yote haya kayaeleza huko Mbeya. Chanzo: Live G FM Mbeya.
jf napenda niwakumbushe kunaandiko
EWE MWANA WA KUWA !
usiitakie roho yeyote kile ambacho wewe usingejitakia na usitamke lile usilolitenda maneno yako yaendane na vitendo vyako fahamu kwa ukweli yule awambiaye watu wawe wa haki nayeye mwenyewe akatenda udhalimu huyo siye wa mngu ata akiitwa kwa jina la mngu
Hongera ndugu, inaonesha unaimani ktk Mungu (nadhani ulimaanisha hivyo ulipoandika mngu)Samahani, hivi, mtu wa imani kwa nini umejipa jina la Mfia Kicheko?EWE MWANA WA ROHO Hakuna amani yoyote kwako ila tu kwa kujikana mwenyewe na kumgeukia mngu kwani ya kupasa kujitukuza katika jina la mngu na siyo katika jina lako mwenyewe weka imani yako ndani ya mngu wekeza kwa mngu
unapendekeza niitwe nani?Hongera ndugu, inaonesha unaimani ktk Mungu (nadhani ulimaanisha hivyo ulipoandika mngu)Samahani, hivi, mtu wa imani kwa nini umejipa jina la Mfia Kicheko?
Na Mwandishi Wetu - Majira
KIZUNGUMKUTI cha uasisi wa Chama Cha Jamii (CCJ), kimeendelea kuwazunguka makada waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
vigogo walioko serikali, ambapo 'muasisi' mwingine amejitokeza akiweka hadharani madai yake juu ya waliohusika katika mpango huo.
Daniel Ole Porokwa, ambaye alijitambulisha kuwa ni kada wa CCM, akizungumza jana na waandishi wa habari Dar es Salaam, alikiri kuombwa kuwa mmoja mwanzilishi wa CCJ, akidai kuwa alishawishiwa kufanya hivyo baada ya kukutana mara kadhaa na Bw. Nape Nnauye, Dkt. Harrison Mwakyembe, Bw. Fred Mpendazoe na Bw. Samuel Sitta.
Alidai kuwa katika mikutano zaidi ya mitano aliyofanya akiwa na Bw. Nnauye na Dkt. Mwakyembe, wenzake hao walimweleza mpango wao wa kuanzisha chama cha siasa kuwa umelenga kuondokana na utawala wa kiimla wa CCM, kwa hoja kuwa chama hicho kilipofikia hivi sasa, hakiwezi tena kuaminiwa kukabidhiwa madaraka kuongoza dola.
Kwa madai ya Bw. Porokwa, viongozi hao aliokuwa akikutana nao katika mipango ya kuanzisha CCJ, walisema CCM haiaminiki tena machoni mwa Watanzania na kimepoteza mvuto mbele ya umma, kwa sababu kimeacha misingi yake, iliyowekwa na waasisi wake, akiwemo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.
"Nimeamua kufanya hivi (kutoa madai hayo) kwa misingi miwili mikuu. Kwanza, sisi kama viongozi ni sharti tuwaoneshe wananchi wetu na wanachama wa chama chetu njia sahihi tunayotakiwa kupita, tuamini katika hiyo njia tunayoelekea. Pili, mmoja wa msingi mkuu wa chama chetu ni kusema ukweli...uongo na fitina ni mwiko.
"Ni kweli niliwahi kuombwa kuwa mmoja wa wanachama waanzilishi wa CCJ. Nilikutana mara kadhaa na Mheshimiwa Nape Nnauye, Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe na Mheshimiwa Fred Mpendazoe.
"Aidha nilikutana mara moja na Mheshimiwa Samwel Sitta baada ya Mheshimiwa Nape na Mwakyembe kunitajia kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ, nami kutaka uthibitisho wa hicho walichonieleza. Naye Sitta alieleza kuwa nilichoelezwa na Nape na Mwakyembe hakina chembe ya mashaka," alisema Bw. Porokwa.
Aliongeza sababu nyingine ya kuamua kusema hayo ni baada ya kuwasikia Bw. Nape na Dkt. Mwakyembe wakimkana Bw. Mpendazoe, ambaye ndiye aliyeibua tuhuma hizo za vigogo wa CCM na serikali waliohusika kuanzisha CCJ, akijenga hoja kuwa itakuwa ni vigumu kwa chama hicho na serikali yake kuwatumikia wananchi;
Kama viongozi wake wamefikia hatua ya kusigana kiitikadi na kutokuwa wamoja katika masuala ya msingi ya utawala na uongozi wa nchi, kwa maslahi ya Watanzania wote.
Akijibu shutuma hizo baada ya kupigiwa simu na Majira, Bw. Sitta ambaye alisema alikuwa safarini kutoka Arusha, alijibu;
"Hivi waandishi wa habari hili suala...people can change parties let alone kuanzisha vingine...kwa hiyo amenizungumzia mimi...let us forget it, sisi tunashughulikia mambo makubwa zaidi ya hayo," alisema kisha akakata simu.
Naye Dkt. Mwakyembe alipoulizwa bila kufafanua alisema 'Muulizeni huyo Porokwa kama aliacha kugombea ubunge kwa sababu ya pesa, leo kapewa shilingi ngapi ili azungumzie suala hilo.