Sitta Ataka Mdahalo na Lowassa Kuhusu RICHMOND; Asisitiza Kuwa Lowassa ni Fisadi!

Hivi Team ya Propaganda ya CCM mbona inazidi kupanic.Huyu Sita nae yy sio size ya Lowasa,Anna Makinda.Au Labda Tabwe Hiza ila hatamuweza pia.

MICCM mipovu inawatoka kila kukicha,yaani badala ya kutangaza Sera Lowasa..Tushakuwa Viziwi tunataka CCM iondoke tufanye maendeleo ya Tanzania mpya tuitakayo.
 
WanaJF,

Akiwa anahutubia wananchi wa jimbo lake, mhe Sitta amesema waziwazi bila kuficha chochote uhusika wa Lowassa kwenye sakata la RICHMOND.

Sitta alieleza kuwa, ni aibu kwa mtu fisadi kama Lowassa kuthubutu kugombea Urais.

Katika kukazia maelezo yake hayo, Sitta aliueleza umma wa Watanzania kupitia mkutano wake huo kuwa, Lowassa alishirikiana na rafiki yake Rostam kuunda kampuni hewa ya Dowans ambayo inaendelea kututafuna Watanzania hadi hii leo. Sitta aliongeza kuwa, "pesa ya kuwalipa Dowans imeingizwa kwenye deni la Taifa, deni ambalo mimi na wewe tunalilipa"

Aidha, Sitta amesema ikiwa Serikali ingetumia pesa ya kuwalipa Dowans pekee katika kuleta maendeleo, basi pesa hizo zingetosha kabisa kumaliza changamoto zote katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi ya walimu, kujenga maabara na vifaa vingine vya kufundishia na kuongeza shule kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sitta zaidi ya 300. Badala yake kwa uovu wa Lowassa Serikali inatumia mabilioni hayo ya fedha kuwalipa Dowans.

Katika kuhitimisha hotuba yake hiyo mujarabu, Sitta amesema ikiwa Lowassa atapinga chochote kati ya hayo aliyosema, basi anamtaka Lowassa kufanya mdahalo kupitia kituo chochote cha televisheni upande mmoja akiwa yeye (Sitta) na Mwakyembe huku upande mwingine akiwa Lowassa na mafisadi wenzake atakao wataka.

My take,

Taifa haliwezi kuongozwa na FISADI.

Naota linaongozwa nae
 
Huyu naye sijui kala maharage ya wapi? Huyu si ndiye aliyeondoa maoni ya wananchi kwenye katiba pendekezwa? Watu wengine bwana? Hivi huyu baba haoni aibu? Mimi ningemshauri atishe mdahalo, atueleze kwanini aliondoa maoni ya wananchi kwenye katiba, pendekezwa. Je kuna ufisadi mkubwa zaidi ya huyo. Bora huyu baba angekaa kimya, tu, tu be honest he deeply irritates me. He better shut up. Otherwise, he keeps on embarrassing himself. Angekuwa muungwana angekaa kimya. Huyu si ndiye alitukana watumishi wa Mungu alipokuwa mwenyekiti wa BMK?. Mimi namshauri atubu kwa Mungu wake, kwasababu amechakachua maoni ya wananchi.

Ondoa boriti kwenye jicho lako kwanza muheshimiwa, acha unafiki, na muogope Mungu. Aibu yako, hata wewe???

Kweli kabisa tumechoka na blah blah!
 
CCM wakiwa ktk dola huwa wanadhani wao ni miungu. Akiongea Mungu mengi huwa fundisho.Bahati mbaya bado huendelea jidanganya zaidi na zaidi. Wastaafu wanashinda nyumba za ibada ambazo ,walizikandamiza sana wakiwa ktk mamlaka.
 
Back
Top Bottom