Sitta Ataka Mdahalo na Lowassa Kuhusu RICHMOND; Asisitiza Kuwa Lowassa ni Fisadi!

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
WanaJF,

Akiwa anahutubia wananchi wa jimbo lake, mhe Sitta amesema waziwazi bila kuficha chochote uhusika wa Lowassa kwenye sakata la RICHMOND.

Sitta alieleza kuwa, ni aibu kwa mtu fisadi kama Lowassa kuthubutu kugombea Urais.

Katika kukazia maelezo yake hayo, Sitta aliueleza umma wa Watanzania kupitia mkutano wake huo kuwa, Lowassa alishirikiana na rafiki yake Rostam kuunda kampuni hewa ya Dowans ambayo inaendelea kututafuna Watanzania hadi hii leo. Sitta aliongeza kuwa, "pesa ya kuwalipa Dowans imeingizwa kwenye deni la Taifa, deni ambalo mimi na wewe tunalilipa"

Aidha, Sitta amesema ikiwa Serikali ingetumia pesa ya kuwalipa Dowans pekee katika kuleta maendeleo, basi pesa hizo zingetosha kabisa kumaliza changamoto zote katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi ya walimu, kujenga maabara na vifaa vingine vya kufundishia na kuongeza shule kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sitta zaidi ya 300. Badala yake kwa uovu wa Lowassa Serikali inatumia mabilioni hayo ya fedha kuwalipa Dowans.

Katika kuhitimisha hotuba yake hiyo mujarabu, Sitta amesema ikiwa Lowassa atapinga chochote kati ya hayo aliyosema, basi anamtaka Lowassa kufanya mdahalo kupitia kituo chochote cha televisheni upande mmoja akiwa yeye (Sitta) na Mwakyembe huku upande mwingine akiwa Lowassa na mafisadi wenzake atakao wataka.

My take,

Taifa haliwezi kuongozwa na FISADI.
 
Naona CCM yote imechanganyikiwa kwa sasa, kitengo cha Propaganda ndio kipo kazini mitandaoni. Kila kada ana haha kutafuta silaha ya kupigania.

UKAWA wanasonga mbele na Lowassa anakwenda Ikulu, ameshamaliza kuiteka Dar, sasa kuteka mkoa kwa mkoa, mpaka mwisho.
 
Mbona kipindi hiki ccm wana muwasho wa mdahalo sana wa urais?
Mbona kipindi cha Dr. Slaa mlikua hamtaki kusikia mdahalowa urais?

Na sisi kipindi hiki tunasema HATUTAKI kajadalianeni wenyewe sisi tupo busy na WATANZANIA.

Huo muda utoke wapi mkuu? Wao maji ya shingo yamewafika wanatafuta pa kutokea...
Na sisi tunachomoa tu ili wazame vizuri.
 
nae sita aeleze wakati akiwa mkurugenzi na waziri wa CDA dodoma kwa muda wa miaka 10 kila mwaka milioni 300 zilikwenda wp kuanzia 1971 - 1981 na wakati huo dola ya marekani ilikuwa kati ya shilingi moja na nusu na shilingi tano za tanzania uko wapi huo mji mkuu waliojenga DODOMA?

kwa wale wa umri mdogo CDA Maana yake ni Capital Development Authority. ilikuwepo miaka hiyo
 
Sita kakosa hoja ya msingi. Kama Lowasa anahusika na richmomd si wampeleke mahakamani?Lowasa katoka madarakani 2008,siku zote hizo walikua hawaongei eti kwa sababu kahama chama basi ni fisadi what a nonsense, Mm sipendi porojo ambazo hazina msingi. Badala ya kunadi sera zao kila siku ni Lowasa Lowasa. CCM nawaonea huruma sana,kwa mwendo huu ukawa wanachukua nchi asubuhi mapeeema.
Badala ya kuongelea ishu ya escrow ya juzi tu hapa wanongea mambo ambayo hawana ushahidi nayo.
 
Wanamapinduzi cha msingi ni kujua kwamba ccm wamesambaza watu wao kwenye mitandao kwa leongo la kumchafua presidaa wetu mtarajiwa. Watanzania wana akili sana na hamuwezi kubadili walichoamua. Watanzania wanataka mabadiliko nnje ya ccm
 
Back
Top Bottom