Sitta apangua tuhuma za Zitto

Sitta apangua tuhuma za Zitto

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
TUHUMA za ufisadi zilizotolewa na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe dhidi ya Serikali katika mradi wake mpya wa Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC) Tanga, zimepanguliwa na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Jumapili iliyopita, Zitto akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Iringa, alisema kuna ufisadi mkubwa zaidi ya ule wa wizi wa fedha za Escrow katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) ambao unagharimu zaidi ya Sh.50 trilioni, ukifanywa na Mwenyekiti wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemalira.

Katika tuhuma hizo nzito, Zitto alisema serikali imetoa mradi kwa Rugemalira kifisadi bila kuzingatia sheria ya kutangaza zabuni. Kwamba anashangazwa na serikali kuwapa kazi ya ujenzi ya bandari ya MWAPORC watu ambao walikuwa wanatuhumiwa katika kashfa ya akaunti Tegeta Escrow pasipo kufuata utaratibu.

"ACT – Wazalendo tunamtaka Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta afanye uchunguzi kuhusu mradi huo wa MWAPORC na achukue hatua kwa kuwa huu ni ufisadi mkubwa kushinda ule wa Escrow," alisema Zitto.

Sitta katika mkutano wake na waandishi wa habari leo, ametumia dakika chache kujibu tuhuma za Zitto, akisema hakuna ufisadi wowote unaofanywa na serikali, bali watu mbalimbali wa sekta binafsi wanabuni miradi na kuja kuiombea vibali serikalini.

Amesema, "Rugemalira na watu wengine wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) wamekuwa wakijaribu kupata wabia ili kuendeleza mradi wao wakiwa na lengo nzuri kabisa kwamba tupate biashara inayotoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

"Serikali haihusiki na senti yoyote ila tunasubiri mapendekezo yao yoyote kwa hatua za awali. Niseme tu haitakuwa rahisi kukubali mradi ambao unakwenda sambamba na mradi wa reli ya kati, kwa sababu ni lazima tutazame faida itakayopatikana".

Sitta ameongeza kuwa kama kuna kundi la Watanzania wanataka kushawishi basi waanzie kuangazia upande wa Congo ambapo ni takribani kilomita 2000 ambayo inaunganisha na reli ambayo ipo kwenye mradi.

"Kwa kuwa tuna mradi wa reli ya kati kwa kiwango cha upana mpya yaani kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma, Tabora, Mwanza, Isaka, Rusumo, Kariwa, Mpanda na Karemo. Huu ndio mpango uliopo wa serikali, na unatafutiwa fedha na tumefika pazuri.

"Yoyote anayetaka kuwekeza katika mradi huu aje, ila ni lazma kuwe na uwiano. Vinginevyo tunaweza kujenga reli mbili kwenda sehemu moja harafu tupate hasara, kwa hiyo hakuna mradi wowote ambao serikali imeingia ubia ukiacha mradi wetu," amesema Sitta
 
Wakati flani Zito kama walivyo viongozi wengine wanaropoka . Wanasema mabo bila kuwa na hakika nayo ili tu wapigiwe makofi wakiwa jukwaani.

Mghosi
 
Zitto kwa kuropoka!!!
Hajui kuwa wenzie wanabuni uwekezaji utakao sustain kesho na keshokutwa yao, yeye kajikita kwenye siasa nyepesi za kutumika kama toilet paper na masrahi ya ghafla.
Hutafika mbali kijana
 
zzk nakupongeza kaz nzur unayofanya mweny akili atakufata make mpaka saizi una bifu sekta zote tofauti ni wananchi tu wanaokkubali unaowaangaikia ila nakusihi uckate tamaa
 
zzk nakushaur uctetereke kwa lolote tambua walioko jf ni wale unaowasumbua vichwa vinawauma wapenda kula jasho la wanyonge ila nnaamin mwananchi wa kawaida hayuko umu jf ambae unampigania ivo izi kelele zimo mitandaon ukienda kwa wananchi wanakulilia
 
TUHUMA za ufisadi zilizotolewa na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe dhidi ya Serikali katika mradi wake mpya wa Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC) Tanga, zimepanguliwa na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Jumapili iliyopita, Zitto akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Iringa, alisema kuna ufisadi mkubwa zaidi ya ule wa wizi wa fedha za Escrow katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) ambao unagharimu zaidi ya Sh.50 trilioni, ukifanywa na Mwenyekiti wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemalira.

Katika tuhuma hizo nzito, Zitto alisema serikali imetoa mradi kwa Rugemalira kifisadi bila kuzingatia sheria ya kutangaza zabuni. Kwamba anashangazwa na serikali kuwapa kazi ya ujenzi ya bandari ya MWAPORC watu ambao walikuwa wanatuhumiwa katika kashfa ya akaunti Tegeta Escrow pasipo kufuata utaratibu.

“ACT – Wazalendo tunamtaka Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta afanye uchunguzi kuhusu mradi huo wa MWAPORC na achukue hatua kwa kuwa huu ni ufisadi mkubwa kushinda ule wa Escrow,” alisema Zitto.

Sitta katika mkutano wake na waandishi wa habari leo, ametumia dakika chache kujibu tuhuma za Zitto, akisema hakuna ufisadi wowote unaofanywa na serikali, bali watu mbalimbali wa sekta binafsi wanabuni miradi na kuja kuiombea vibali serikalini.

Amesema, “Rugemalira na watu wengine wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) wamekuwa wakijaribu kupata wabia ili kuendeleza mradi wao wakiwa na lengo nzuri kabisa kwamba tupate biashara inayotoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

“Serikali haihusiki na senti yoyote ila tunasubiri mapendekezo yao yoyote kwa hatua za awali. Niseme tu haitakuwa rahisi kukubali mradi ambao unakwenda sambamba na mradi wa reli ya kati, kwa sababu ni lazima tutazame faida itakayopatikana”.

Sitta ameongeza kuwa kama kuna kundi la Watanzania wanataka kushawishi basi waanzie kuangazia upande wa Congo ambapo ni takribani kilomita 2000 ambayo inaunganisha na reli ambayo ipo kwenye mradi.

“Kwa kuwa tuna mradi wa reli ya kati kwa kiwango cha upana mpya yaani kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma, Tabora, Mwanza, Isaka, Rusumo, Kariwa, Mpanda na Karemo. Huu ndio mpango uliopo wa serikali, na unatafutiwa fedha na tumefika pazuri.

“Yoyote anayetaka kuwekeza katika mradi huu aje, ila ni lazma kuwe na uwiano. Vinginevyo tunaweza kujenga reli mbili kwenda sehemu moja harafu tupate hasara, kwa hiyo hakuna mradi wowote ambao serikali imeingia ubia ukiacha mradi wetu,” amesema Sitta

Bavicha lini mtaacha upuuuziiiiiiiiiii leo mr 6 ni bors kiasi cha kukubaliana na yeye.
Yaani nyi kwenu yeyote anayemshughulikia zzk nyie kwenu mwema!?
 
Bavicha lini mtaacha upuuuziiiiiiiiiii leo mr 6 ni bors kiasi cha kukubaliana na yeye.
Yaani nyi kwenu yeyote anayemshughulikia zzk nyie kwenu mwema!?

Mbona inakuwa mbinafsi, yaani Zitto atoe tuhuma halafu wengine wasijibu. Kwamba Zitto akisema tusisikilize upande wa pili??
 
Bavicha lini mtaacha upuuuziiiiiiiiiii leo mr 6 ni bors kiasi cha kukubaliana na yeye.
Yaani nyi kwenu yeyote anayemshughulikia zzk nyie kwenu mwema!?

Yaan hawajamaa wanaompinga ZITTO ndo rafiki yao kwa sasa hatakama alikuwa adui yao
 
Back
Top Bottom