Sitta ampinga Ngeleja malipo fidia Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta ampinga Ngeleja malipo fidia Dowans

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 9, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Waziri katika Baraza la Mawaziri ameamua kumkosoa mwenzake hadharani kutokana na uamuzi alioutangaza hivi karibuni kwa Taifa.

  Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ndiye amepata ujasiri huo kwa kumkosoa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kutokana na kutangaza kuilipa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Sh bilioni 94, hatua ambayo anaona hakustahili
  kuitangaza yeye.

  Sitta alisema hayo jana, baada ya kumaliza kuongoza mahafali ya Shule ya Sekondari ya Dini ya Maranatha iliyoko Mianzini Kata ya Kaloleni jijini hapa.

  Alisisitiza kuwa Dowans ni ya wajanja waliocheza ujanja kwenye karatasi na Serikali kuingia
  ‘mkenge’ kulipa kitu ambacho alikielezea kuwa hakina sababu za msingi.

  Waziri huyo alisema Kampuni ya Richmond iligundulika na Kamati ya Uchunguzi ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, kuwa haikuwa halali lakini inasikitisha kuona na kusikia mbia wake, Dowans amehalalishwa, “kitu hicho ni hatari sana kufanywa na jamii itakuja kutuhukumu kwa hilo.

  ‘’Mzabuni feki anacheza karata zake na mbia wake Dowans nasi tudiriki kulipa kitu ambacho si halali … kamwe haiwezi kuwa halali katika maisha yote,” alisema.

  Sitta alitoa mfano wa mtu ambaye hakumtaja jina, kuwa ana kampuni 17 nchini, lakini jina lake halionekani katika kampuni yoyote na ambaye alidai anacheza michezo michafu na kulipwa mamilioni ya fedha.

  Alisema watu hao wapo na wanacheza na karatasi na kuhalalisha kujipatia mamilioni ya fedha za walipa kodi wa nchi hii.

  Pia Waziri alisikitishwa na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya ‘kunawa mikono’ mapema na kukubali kuilipa Dowans, hatua ambayo alisema ilimshitua sana.

  Alisema kwa jambo zito kama hilo, ni lazima Serikali ingekaa chini na kuliangalia kwa mapana na hata ingewezekana kuitisha kikao cha Baraza la Mawaziri kujadili suala hilo kwa kina na kulipatia ufumbuzi wa pamoja, lakini Waziri Ngeleja amelisema haraka jambo hilo.

  Sitta alisema Sh bilioni 94 zingejenga barabara ya lami ya kilometa 100 yenye ubora wa hali ya juu vilevile kwa kujenga shule za sekondari 300 za kidato cha kwanza hadi cha nne.

  ‘’Naweza kusema wajanja wametuzidi akili na wamefaidi kodi za wananchi kujilipa, lakini elimu bila maadili nchi inaweza kwenda mrama,’’ alisema.

  Waziri Sitta alisema kwa sasa huwezi kufanya lolote juu ya malipo ya Dowans kwani ‘’unawezaje kufunga zizi la ng’ombe wakati ng’ombe wote wameshaondoka?’’

  Alisema ataendelea kusema ukweli mwanzo hadi mwisho bila kumwogopa mtu na kamwe hawezi kuwa mwongo na mnafiki kwa jambo lolote.

  Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC) iliamua katika hukumu yake Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) iilipe Dowans fidia ya Sh bilioni 94 kutokana na Tanesco kuvunja mkataba nayo.

  Uamuzi huo uliridhiwa na Serikali baada ya Mwanasheria wake Mkuu, Frederick Werema kuipitia hukumu hiyo na kujiridhisha kuwa ni halali.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kaka Sitta ongeza spidi, kidogo kidogo utakuwa hero wa taifa hili.
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani kwenye hili JK yupo cornered kikwelikweli, anywayz ni part of the problem hence not cornered. Nimejikuta namkubali huyu mzee Sitta kuliko wakati wowote ule!!!!!
   
 4. k

  kabindi JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tangu January Mwaka uanze hii sasa ni taarifa ya kwanza kunikuna! huyu Bwana angefaa kuwa rais wetu! lakini bado wakati hupo! BINADAMU JASIRI NA MWEYE AKIRI TIMAMU ANATAKIWA KUWA KAMA SITTA!
   
 5. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna tatizo la kiutandeaji katika baraza la mawaziri wa Kikwete. Kuna wengine hawana lengo la kufanya kazi kama timu bali wanahangaikia umaarufu. Wengi katika mawaziri hao, wamekuwa wakiongea mno na vyombo vya habari. Huyu bwana kama haamini kile wanachokifanya wenzie na njia yake ya kukosoa ni kupitia vyombo vya habari, basi ni vyema angeamua kukaa pembeni na kuwa Mbunge wa kawaida nadhani angeheshimika zaidi.
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kweli watu kama hawa wanaofanya CCM iwe unstable tunawataka sana . But naona Six kaanza vison 2015 mapema anajiweka katika postionaili tumtofautishe na "wale"

  But whtever the case whatever the motives we need more four or five sixies within CCM
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  asante six..lkn ni changamto kwa watanzania kuwa malipo yanayotaka kufanywa na ccm si harali tuchukue hatua..wabunge wetu nanyi tusaidieni kwa hili
   
 8. Lisa Rina

  Lisa Rina JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 1,771
  Likes Received: 2,043
  Trophy Points: 280
  Finger pointing haitotusaidia kitu!ur also the government!
  Mnatutia hasira tu kelele nyingi thn ucku mnalala!something need to be done n nt jus a pointing then what!
   
 9. W

  We can JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sita, heshima yako itapanda kama utasema:
  1. Wamiliki wa Dowans ni (a)......, (b)......, (c).........
  2. Mwenye kampuni 17, na akiwa ametumia majina tofauti tofauti ni..................................
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Jan 9, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sasa kama Baraza la Mawaziri halijaitishwa angeenda kusemea wapi? Hukumuni kwa haki sio kwa jazba na makengeza ya akili!
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Jan 9, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tatizo hapa ni ushahidi wa hao wamiliki wa makampuni 17 ambao majina yao hayaonekani anywhere! Hapa ndio IGP Mwema alitakiwa kutupa taarifa za kiintelijensia kuliko kukimbilia kuua watu ovyo wasio na hatia!
   
 12. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mzee umenena!
   
 13. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hakuna hukumu hapo juu mali ni mawazo. Well nani alimuuliza kwamba baraza la mawaziri limesema? Yeye Sitta naye ni Serikali. Kama haiamini Serikali kwanini asikae pembeni abaki kuwa muhimili mwingine peke yake? Kwani yeye ndiye msemaji wa Baraza la Mawaziri juu ya agenda zake? Kama hawaamini wenzie na kuhakikisha kuwa wanaonekana wa hovyo, anasababu gani ya kufanya nao kazi? Huyu bwana amekuwa na hasira zaidi baada ya kuukosa Uspika. Angeweza kufanya vyema katika wizara aliyopo na akaheshimika zaidi. Aangalie mifano ya kina Magufuli hata leo hii ukianzisha wizara ya kuchimba mitaro ukampa magufuli, utajua kule kuna mtu anafanya kazi. Sio yeye ambaye amejiegeuza msemaji wa kila kitu. Ni bora kuchagua kuwa mbunge au kukaa pembeni kabisa na kwenda kwenye chama kingine. Kwa kumalizia ni vyema nikamtolea mfano Mbunge Zitto. Yeye amekuwa akipingana na wenzie katika chama, na hapa jamii forum wengi saana wamekuwa wakimuhukum. Kuna tofauti ipi na Sitta?
   
 14. B

  Baba Tina Senior Member

  #14
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sitta endelea kukandamiza na kusema ukweli, tatizo hizo pesa za dowans zinapita kwingi sana, ngeleja na mwanasheria mkuu sio wajinga kuridhia malopo hayo nina wasiwasi huenda nao wana shea yao. Inawezekana vipi hukumu inatolewa halafu wanaridhia malpo bila hata ku appeal????????????????????//
   
 15. J

  Jahazi New Member

  #15
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si hekima wala busara kudhani ama kukusudia kuwaaminisha watanzania kuwa kusema ukweli ni tendo linalofanywa na mtu anayetaka au umaarufu. Kwani umaarufu wa Mzee Six uliporomoka lini kiasi cha kumshangaza yeyote? Ama pengine ulitaka kumzushia kwamba analipa kisasi? Yote si ya kweli! Je, kama ishu ya kitapeli iloundwa na wezi wa hapa walovaa makoti ya madaraka walopora wananchi kwa ujanja leo inaitwa Dowans na juzi na jana ilitwa Richmonduli isingekuwepo, unaweza kutuambia angeuonyeshaje umaarufu unaousema? Nyufa ziwafichazo mijusi hawa wafyonzao uchumi na maendeleo ya Taifa ka kupe karibu itafungwa kwa kuundwa na kuzinduliwa kwa Katiba mpya za Tanzania na ile ya Tanganyika maana kwa hali ilivyo hivi sasa hizi mbili na ile ya Visiwani ndo mwafaka endelevu wa Taifa letu.
   
 16. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Wamiliki wa DOWANS ni wana nguvu sana kiasi ambcho hata JK anawaogopa...hii inanikumbusha Jinsi PABLO ESCOBAR alivyokuwa na nguvu ...kama mtakumbuka mwanasiasa jasiri Rodrigo Lara Bonilla yaliyompata baada ya kutaja hadhrani kuwa Esobar is drug baron....Namfananisha Sitta na Bonilla
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Jan 9, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sasa kama mwenye nchi amekaa kimya kama kamwagiwa maji ya baridi kuhusu malipo haramu ya DOWANS watu wakae kimya? Huu utaratibu wa kuongea kila mtu kivyake katika Serikali ya JK ni wa kawaida kabisa! Kombani kadai Serikali haina fedha kugharamia mchakato wa Katiba mpya, AG akadai kuwa Katiba mpya "hapana" ila viraka "yes!" JK akaja mwishoni kudai kuwa ataanzisha mchakato wa Katiba mpya, sijui sasa atatoa wapi fedha! Sasa sioni kwa nini unashangaa nini kuhusu mzee wa watu Sita kukemea uporaji huu wa mchana kweupe? Au mwenzetu umeahidiwa mgao?
   
 18. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwanza la Kombani na la Sitta linautofauti mkubwa hasa! Kombani na mwenzake Werema walikuwa wanaongelea ishu zilizo chini ya mamlaka yao na si za waziri mwingine. Pia hawa watu wawili hawakuhusisha matamshi yao na baraza la mawaziri. Tatu two wrongs........
   
 19. G

  Godwine JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  sitta toka kwenye chama chetu na kwenye uwaziri wewe hutaki wana ccm tuibe pesa .....wewe kwani ukuwepo kwenye kikao cha kuchuma pesa kuimarisha chama wewe ni mtu gani usiyejua madili.........kikwete mtoe sitta si mwenzetu kwani anatuhujumu.........kwenye mabadiliko ya mawaziri mtoe kama mama watoto alivyotoka.............fedha za 2015 lazima ziibwe mapema
   
 20. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kwa maelezo haya, ina maana Sita alipanga kuachia ngazi kama baraza la mawaziri lingebariki malipo kwa Dowans. Sasa Mheshimiwa labda akaona asiitishe kikao kujadili suala hilo kwani hiyo ingempa credit mzee Sita
   
Loading...