Sitosahau siku niliyomuona Jini lakini Bangi ilimkimbiza

young MathematiciAn

Senior Member
Oct 31, 2016
160
361
Katika maisha yangu ya ukuaji utotoni mpaka ujanani kwangu nimekuwa nikiwasikia viumbe aina ya majini tuliambiwa majini ni viumbe visivyoonekana na wanatisha sana na wengi tuliogopa kukutana na viumbe hivi wa kusadikika licha ya kutowahi kuviona.

Wapo ambao wanaamini uwepo wao na wapo ambao hawaamini uwepo wao binafsi sikuwa wa kutilia maanani sana jambo hili lakini niliamini wapo sababu nimeshuhudia watu mbalimbali wakiwa posessed na majini na wakipandisha hivyo kwa kiasi fulani niliamini wapo.

Kuna story nataka kuisimulia ambayo ilitokea mitaa ya kwetu hapahapa jijini Dar es Salaam mida ya usiku wa manane na kwa bahati nzuri au mbaya mimi ni popo napenda sana kuzurura usiku na kwa wakazi wa Dar wanafahamu mida ya usiku kwenye barabara za watembea miguu kwenye main roads aidha Kawawa Road, Morogoro Road au Mandela Road kuna kuwa na viosk ambazo hutoa huduma ya pombe, vishots, sigara na nesta marley.

Pia sehemu zingine utakuta vijiwe vya kahawa n.k. Kwa mantiki hio usiku huwa hapaboi; mimi huwa popo nikienda maskani tofauti tofauti road kupata habari na michapo tofauti tofauti ukizingatia ni karibu na nyumbani hivyo sura za usiku huwa nazijua na huwa ni burudani kubishana n.k

Katika moja ya maskani au kiosk kinachotoa huduma ya shots, sigara pembezoni mwa barabara moja kubwa na maarufu hapa jijini Dar alitokea dada mmoja alijifunika mwili mzima alikuja kufungua kibiashara chake na alikuwa anauza juice na cha kushangaza dada yule alikuwa hakuuzii bidhaa na haruhusu yeyote yule afungue friji na hata akiuza hakuruhusu usogelee friji ama ufungue hiyo friji

Kama ujuavyo road huwa kuna mama ntilie wanaotoa huduma ya chakula na siku hio bi dada yule aliwahi kufungua kibanda chake ilikuwa saa saba usiku na mida ile ilikuwa mama ntilie bado wapowapo la haula mara tukaanza kusikia mama ntilie wa kwanza kapandisha mashetani mara mwingine kapandisha na wa tatu kapandisha ikabidi watu wajae wajue nini kinaendelea ndipo wale mama ntilie waanze kusema yule bi dada sio mtu ni jitu la hatari, sasa yule bi dada akafyonza akaanza kusema wanafikiri wanavyopandisha wananitisha wanajisumbua tu sasa wahuni huku pembeni kuona vile wakaanza kuwasha ganja kila mmoja sasa yule bi dada akasema hapo kidogo mnaweza kunifukuza.

Na kweli aliondoka mita kadhaa sasa akatokea ustazi mmoja baada ya kuona hali ya taharuki na makelele na alikuwa haamini yaliyokuwa yanasemwa kuwa yule bi dada ni jini, akawa anamshawishi yule dada aondoke ili kuepusha shari na kweli alifanikiwa akawa anaondoka nae kama kumsindikiza ampandishe daladala sasa walipofika kama mita 400 daladala likawa linatokea yule ustazi akalisimamisha na yule dada akapanda sasa jamaa anageuka aondoke anamkuta bi dada na yule bi dada akamwambia ustazi yule hilo sio basi langu la kwangu hilo linakuja na kweli dakika 0 nyingi hiace tupu lilitokea na akapanda na kuondoka.

Sasa kesho yake tunashangaa wale mama ntilie wanapandisha tena kumbe yule bi dada alikuwa anapita chini kwa chini mtaa wa nyuma ili atokee juu; kuona vile akaanza kusema mbona mnanichukia kwani nimewafanya nini nyie mniache kwa amani.

Sasa kuna muuza kahawa mmoja anayeuza kwa kutembeza alisimulia kuwa yule bi dada alikutana naye njiani na alisimamishwa na kumuuzia kikombe cha kahawa yule bi dada kisha bi dada yule akatoa 10,000 na kumkabidhi yule muuza kahawa na kumwambia achukue yote kisha akawa anaondoka sasa yule muuza kahawa kugeuka nyuma kumtizama bi dada haoni mtu na wakati sehemu ile ni open space kwa simulizi ya yule muuza kahawa alitoka spidi mithili ya digidigi akimbizwaye na chui na aliacha deli na kashata zake pale.

Hii ni True story na kama kuna mtu anabisha aje usiku aulize watu wa sehemu hii kuanzia mama Ntilie na watu mbalimbali sababu wengi ni walewale na walishuhudia na ndio siku yangu ya kwanza katika maisha yangu kumuona Jini na sijui yule dada saizi kahamia pande zipi maana bila wale mama Ntilie haki ya Mungu tungekuwa tunaishi nae bila kujua.
 
Karibu saana Sana kwenye Festival yetu
IMG-20190403-WA0019.jpeg


You are strong than what you think...
 
Kwa taarifa yako, uvutaji wa bangi bila mpanglio utakuelekeza katika kulifungua jicho lako la tatu bila kuwa tayari.

Sehemu kubwa ya wavuta bangi jicho la tatu huwa tayari limekuwa activated. Na likiwa activated bila kujiandaa, utasikia sauti zikiongea ndani ya kichwa chako. Hatua itakayofuata ni kuona watu waliokufa zamani ikiwa ni pamoja na jamaa zako wa karibu.( Ghosts). Ukiisha ona na kuongea na wafu, tayari umesha fika katika dimension plane ya viumbe unaowaita majini.

Hivyo, usijidanganye kuwa ukivuta bangi Ati jini atakuogopa. Ndio maana wavuta bangi huwa wanaongea peke yao kama vile wanaongea na watu, ni kweli, wanasikia sauti zikiwapa maagizo. Kalaga bahho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa taarifa yako, uvutaji wa bangi bila mpanglio utakuelekeza katika kulifungua jicho lako la tatu bila kuwa tayari.

Sehemu kubwa ya wavuta bangi jicho la tatu huwa tayari limekuwa activated. Na likiwa activated bila kujiandaa, utasikia sauti zikiongea ndani ya kichwa chako. Hatua itakayofuata ni kuona watu waliokufa zamani ikiwa ni pamoja na jamaa zako wa karibu.( Ghosts). Ukiisha ona na kuongea na wafu, tayari umesha fika katika dimension plane ya viumbe unaowaita majini.

Hivyo, usijidanganye kuwa ukivuta bangi Ati jini atakuogopa. Ndio maana wavuta bangi huwa wanaongea peke yao kama vile wanaongea na watu , ni kweli, wanasikia sauti zikiwapa maagizo. Kalaga bahho.

Sent using Jamii Forums mobile app
UMENENA KWELI MKUU 100%
 
Bangi hufungua mlango wa mapepo na wavuta bangi huingiliwa na viumbe hawa na kuwafanya washirika katika uhalifu na agenda nyingine za kuzimu.
 
Kuna jini liliniibukia somewhere nikatoa DUSHE likasepa na lingebaki ningelipiga mpini sipendagi ujinga ningelishushia wazungu
 
Kuna jini liliniibukia somewhere nikatoa DUSHE likasepa na lingebaki ningelipiga mpini sipendagi ujinga ningelishushia wazungu
Yapo majini mahuni, ile kutekeleza dhamira yako hiyo ungelijisikia kama unaanza kutenda kweli, halafu ukajisikia kama kausingzi flani ka starehe, kuja kuzinduka baba upo uchi wa mnyama juu ya mnazi!

Hapo akili ndiyo ingelikusogea mkuu, maana yale hayatakagi ujinga.
 
Back
Top Bottom