Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

fungu langu la kumi nitaenda kulitoa kwa mayatima na wagonjwa hospital lakini sio kanisani
kisha uje na andiko lililosema fungu la kumi pelekni kwa maskini/yatima. nadhani umemwonea wivu Mungu maana ndiye ameelekeza kutoa sadaka nyumbani mwake. suala la matumizi ya fedha ya sadaka hayakuhusu sana kama mshirika ila yanamhusu Mungu na yule aliyempa kazi ya uchungaji.
 
Natumaini wote ni wazima wa afya tele,dukuduku langu ni kuhusu utoaji sadaka makanisani nilikuwa nafikiri % kubwa ya sadaka tunazo toa zinaenda kusaidia mayatima,wajane na wasiojiweza na kueneza neno la Mungu kumbe sivyo ninafikiri sadaka zetu sisi zinawanufaisha wachungaji uku waumini tukiwa choka mbaya,kitu kilichonisukuma nisitoe sadaka ni baada ya kumuona mchungaji wetu kununua magari 3 kwa mkupuo.

Mwezi 4 alinunua LAND CRUISER V8,mwezi 5 akanunua TOYOTA BREVIS,juzi kati mwezi huu wa saba nimemuona mtoto wa mchangaji yupo ndani ya BMW mpyaaa.Nimejiuliza sana huyu mchungaji amepata wapi pesa ya kununua magari yote kwa mkupuo hivi? Jibu nililopata ni sadaka zetu ndizo zinazomfanya mchungaji atanue anavyopenda,waumini masikini choka mbaya kumbe tunamfaidisha mchungaji na familia yake.

Kuanzia leo sitoi tena sadaka wa mchango wowote ule ni heri ni dundulize hela mwisho wa siku nikawasaidie yatima na wagonjwa mahospitalini kuliko kuzidi kuwanufaisha wachungaji.

Asanteni nawatikia EID njema
Hongera kwa kufumbua macho
 
Maisha ni unavyojipanga. Biashara ya dini inalipa sana ndiyo maana watu wengi wanakimbilia. Makanisa yanaongezeka sbb biashara ipo. Jiulize kwanini Ulaya vijana na watu wa umri wa kati wanaojitambua hawasali bali ni wazee tu pamoja na kwamba ndo walikuletea majina unayoyatumia ya Patrick, Peter, James n.k, na makanisa mengi yanafungwa.
 
Hawa nawakumbusha wale wafia dini lakini kipato kama mimi halafu unapeleka nusu mshahara eti sadaka ya ujenzi nyumba ya Ibada. STUKA
 
Hapana,hayo makanisa3 uliyoyataja no makubwa kinachoingia ni kikubwa ,na kinacholiwa pia kikubwa.


.
Wewe unaenda kutoa sadaka Makanisa ya Kilokole unategemea nini..??

Makanisa yanayojielewa kama Katoliki, KKKT na Anglican ni mahala pa kutoa sadaka...Maana huko Mashule, vituo vya watoto yatima, hospitali zinajengwa..
 
fungu langu la kumi nitaenda kulitoa kwa mayatima na wagonjwa hospital lakini sio kanisani
Fungu la kumi ni tofauti na sadaka, na fungu la kumi litaliwa na watoao Huduma madhabahuni kama ma padri, wachungaji na kadhalika na imeandikwa kwenye biblia, na huo ndio mshahara wao na kama ataamua kununua magari ni yy ila ww toa tu, ni kama ww unavyopokea mshahara wako hakuna anaekupangia nn cha kufanya tusiwe na wivu na watoa Huduma Wa madhabahuni
 
Ashukuriwe Mungu Kwa kondoo wake kutoka kifungoni kwa makanisa ya sadaka tu..karibu KKKT apa utasomewa kila j2 mapato yako na Mgawanyiko wake..
 
Nina uhakika sadaka uliyowah toa hapo haifiki hata kununua baiskeli. Kw hyo hata usipotoa ataendelea tu kununua Magari bora ukatoa tu hiko kidogo Mungu akubarikie. Labda ingekuwa ni sadaka yako tu ndo imenunuela magari hayo ndo ungekuna kulalamika.
 
Kuna tatizo katika kanisa la leo. Yesu angekuja angekemea na hata kuwachapa na kuwafunga baadhi ...
Baadhi ya wachungaji na wahubiri tamaa yao kubwa ni pesa.
Jana nilipanda basi hapa Dar ndani alikuwepo kijana mmoja mhubiri kaweka hadi maspika alisoma tu mstari mmoja wa Biblia na kuanza maneno meengi hadi kusema kuwa baba yake alikuwa mchawi! Mwisho alianzaa kuomba sadaka.
siku hizi hata maombezi ni kwa pesa. Tusikatae, kuna haja ya kujihoji tunakoenda kiimani usanii umeingilia imani!
 
Wachungaji wengine ni wauza sembe. Kanisa ni geresha tu.
 
Umesema vyema mkuu lakini huku nako mambo si shwari katika baadhi ya parokia na majimbo. Kuna mapadri wanagombania hizo sadaka, kuna wale jamaa wanaohesabu hizo sadaka baada ya misa au jumuiya hupora hizo pesa. Hapa ninavyoandika mama mmoja jirani yangu amegeuza kigango fukani kuwa "sakosi" yake na anachota mapesa jinsi atakavyo.
Vikundi vya dini mashuleni na vyuoni ni miradi ya viongozi wa vikundi hivyo na wanapiga pesa bila aibu.
Mimi kutoa sadaka kanisani nilishaacha japokuwa si completely. Ninapokuwa na hela nawapa masikini zaidi yangu njiani na moyo wangu kujisikia vizuri lakini si kwa katekista, padri wala mchungaji.
Usimamizi mbovu huo mimi katika parokia ninayosali ipo poa sana kila Kitu kipo wazi Hakuna usiri tumejenga chekechea tumejenga kanisa jipya kubwa tumejenga chuo cha ufundi stadi nk paroko wetu ni zaidi ya msikivu bajeti tunasomewa mwisho wa mwaka unapokuwa na wasiwasi unaruhusiwa Kuuliza hata ukiwa peke yako huduma zote hutolewa kulingana na utaratibu wa kanisa, matumizi ni wazi
 
usiishi kwa kukariri ndugu yangu kwa utafiti wangu mdogo niloufanya japo mimi ni muislam wachungaji wengi wamesoma na wana ujuzi wao ama ajira nyingine tena zenye mpunga mkubwa sana zaidi ya uchungaji, wakristo hasa wa madhehebu makubwa huwa hawatoi nafasi ya uchungaji kwa akila mtu tuu kuna vigezo wana angalia ikiwemo elimu..sasa tuambie ilo kanisa unalo sali wewe nilipi...? usije ukawa uanasali kwenye kanisa la waabudu shetani harafu unatuletea utoto hapa
Ww sio muislam
 
Back
Top Bottom