Sitokuja kusahau nilivyo husishwa na dawa za kulevya

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2022
17,796
32,148
Hellow

Hii kitu kila nikikumbuka inanifanya nichuke tahadhari sana kila ninapo pata safari Ilikuwa hivi

Baada yakupata migogoro katika familia na chuoni kidogo akili yangu ilikuwa mzito sana ndipo nilipo amua nifunge safari niludi dar nika refresh akili kwa siku tatu au nne.

Nikaondoka zangu mpaka kituoni nikawakuta madalali nikaongea nao kuwa nataka gari mzuri inayo kimbia wakasema ngoja tukutafutie basi walipiga magari tofauti yakaonekana kuja ndipo likapatika gari mmoja capricon kutoka moshi to dar


Nilifurahi punde sipunde gari ikafika nikapanda safari ikaaza nimekaa kwenye bus nachat zangu kipindi icho jf nilikuwa naingia na kuchungulia tu sichangii chochote

Gafla tukapita mgagao kabla hatujafika same kuna sehemu kuna askari wapo serious nakazi yao mabus yote yakasimamishwa pale msako ukaaza kwenye bus sina hili wale lile nachati zangu nikashutikia kofi kijana simama toka njee

Nikajua mzee kani tranck nini kwamba natoroka chuoni nilijiuliza maswali bila majibu ndipo nikamsikia afande anasema mkuu huyu hapa kijana mkague huyo yule askari uku akinisukuma nishuke Dah nililia kama mtoto kofi la kushutia af uku wanasema beba begi lako ili unaacha kusoma unasafirisha madawa dah hapo moyo ndio ulipasuka kwa hofu na simanzi

Nilipo shuka nikawekwa chini ya ulinzi kaa chini huku wakiendelea kutafuta ushahidi nikiwa njee nikawa nawaza hapa nikisema ni mtaarifu mzee wangu itakuwa jau kwaza hajui kama naenda dar na hakuna mtu anejua nikajilulipua bhna wakati uho bus bado halijaondoka wanaendelea na msako uku wakinilazimisha niseme begi langu lingine lipo wapi

Nikamwambia askari alie kuwepo njee amenishikilia nikamwambia mimi mtoto wa kamishana fulani wa kitengo fulani yule askari akasema dogo acha janja janja nikatoa vitambulisho vyangu baada ya kuviona aka kimya kidogo akamuita mwezie akaongea nae nikawekwa pembeni lakini nikiongeleshwa vizuri tofauti na mwazoni

Sasa gafla waka mpata muhusika kumbe yule nilie kaa nae ndio alikuwa na madawa ya kulevya na bangi na begi lake jeusi kama langu ase nilitamani nimlukie nimpige wakaniomba radhi pale kwa usumbufu nikapanda kwenye gari ikawa good tu ila uku nawaza sana je kama nisinge pewa uhuru wakuongea ningejikuta mahabusu

Mara ya pili tena gari ilo ilo wakati wa likizo sehemu ile ile aksari wakasimamisha gari safari hii walinifungulisha begi nzima nikamwaga nguo zangu zote pale dah nilikuwa sijafua nguo zangu nikasema naenda kufulia nyumbani ni mvivu kufua ase

Wakati wanaendelea na ukaguzu kumbe mdada wa siti ya mbele yangu ndie alibeba madawa na bangi inasemekana yule dada wakati amepanda gari alikuwa kavaa taiti lakini wakati wanamkuta na uho mzigo alikuwa amevaa nikabu kavaa saa ngapi hakuna ajuaye

Uho ndio ukawa mwazo na mwisho kupanda gari la capricon nikawa nasafiri na magari ya usiku madogo private car
 
IMG_5209.jpg
 
Moshi, arusha wanasafirisha sana mibange kwenda mikoani huko, kuna siku tulisimamishwa kwa ukaguzi ilikua basi la shabiby nilikua natoka arusha kuelekea dodoma. Wakamchukua mtu wao na ushahidi wake tukaendelea na safari.

Ile njia siyo
Kabisa iyo dah af ata mtaani wanavuta bila huoga
 
Back
Top Bottom