Menyebahati
Member
- Jun 27, 2015
- 9
- 4
Muendelezo ndo hakunaga tena amah
UmeonaHii chai bhana..otherwise kuna mahala pa kurekebisha..kwanza alisema ana shahada ya Sayansi ya Jamii kisha akabadilika ana shahada ya IT..kwengine hajakosoe kutiririka sana..alaste viste..






NiceSITASAHAU (simulizi ya kweli)
NA
NIHZRATH NTANI (+255713414189)
Leo nimeamua kuelezea stori hii. Nataka jamii ijifunze kupitia tukio hili lililonitokea miaka mingi iliyopita. Nyakati hizo nilikuwa kijana. Kijana mwenye ndoto nyingi maishani. Ni miaka mingi imepita sasa......lakini bado nakumbuka kila kitu,nakumbuka kila hatua.Bado ningali nakumbuka kila tukio lililonitokea. Ni kama kutizama filamu yenye kisa cha kusisimua..............
**********
Nikiwa ndio kwanza nimetoka kutuma barua ya maombi yangu ya kazi, kwenda kwenye kampuni moja inayohusika na usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi. Asubuhi hii ilinikuta niko maeneo ya Posta,jijini Dar es salaam. Kuwepo kwa mvua za rasha rasha zilinifanya nijumuike na watu wengi kujificha pembezoni mwa korido za ofisi zilizoko maeneo hayo. Hata hivyo, baada ya muda fulani mvua zile zilikata. Nikaanza kujivuta kusogea stendi ili nipate usafiri wa kurudi nyumbani ninapoishi pale maeneo ya Ukonga Airport. Kwa muda ule wa asubuhi ya saa nne hakukuwa na shida yoyote ya usafiri, magari yalikuwa mengi. Wakati nalifuata basi moja kati ya mabasi machache yaliyokuwepo yanayokwenda njia ya Gongolamboto. Nikajikuta namgonga kwa bahati mbaya mdada nisiyemfahamu.Mungu wangu! Bila kutarajia, macho yangu yakajikuta yakiangalia baadhi ya nyaraka zilizosambaa ardhini kutokana na kitendo kile,nikajikuta mwili wangu ukiinama na kuziendea nyaraka zile na kuzikusanya kwa uangalifu mkubwa.
Sikuwa najua nini kilichoifadhiwa ndani ya nyaraka zile. Kwa unyonge niliyainua macho yangu na kumtazama binti yule kwa mara ya kwanza, nakiri kabla ya hapo sikuwa nimemtazama vizuri binti huyu. Macho yangu yakatua kwenye uso wa binti yule, nikashtuka! ni kama nimeshikwa na bumbuwazi kwa muda wa sekunde chache, mapigo ya moyo wangu yalikimbia kwa maili nyingi. Kitendo kile kilifanyika kwa haraka mno. Hata hivyo niliweza kumkabidhi binti yule nyaraka zile, na alipozipokea tu alinisindikiza na tusi na msonyo juu yake, nikabakia kufadhaika, mvulana mimi.
Wakati macho yangu yakimsindikiza binti yule akitokomea ndani kabisa ya bank ya CRDB tawi la Azikiwe lililopo jirani na eneo hilo. Nami nikajivuta na kuingia ndani ya basi, na kukiendea kiti cha kati kati upande wa dereva kisha nikakaa hapo. Dakika chache baadae basi lile likaanza safari. Mawazo ya binti yule yakaanza kunitawala. Hakika alikuwa binti mzuri ajabu na mrembo hasa ambaye nakiri sikuwahi kukutana na msichana mzuri kama yule kabla. Kila kitu kilichotokea kwa dakika zile chache zikawa zinajirudia mawazoni mwangu. Nikajikuta najiuliza kwanini binti yule atawale mawazo yangu?.Nikakosa jibu.
*****************
Milio ya coins kama ilivyo ada ya makonda wengi wanavyozichezesha pesa hizi za silver kwa mtindo wa kipekee kabisa, ilinigutusha kutoka katika lindi la mawazo kwa wakati huo. Konda alikuwa ananikumbusha nimpe pesa yake, huku nikiwa natazama nje, nikaja gundua tupo kwenye foleni ya kuvuka mataa pale tazara. Haraka nikaingiza mkono wangu mfukoni ili nitoe akiba yangu nimlipe konda yule. Hamadi! mikono yangu ilirudi patupu, hakukuwa na pochi wala pesa. Nikajikuta natafuta kila mahali ndani ya mifuko ya suruali yangu lakini majibu yalikuja yale yale, pochi haikuwepo. Nikajikuta nababaika. Wakati huo huo konda alikuwa yupo makini na mimi akisubiria nimpatie haki yake. Kwa mara nyingine tena, nikawaza! nikawaza! nikahofu kufadhaika.
Kwa ujasiri wa kiume nilimjibu konda yule, nimeibiwa pochi na pesa iliyokuwemo. Konda hakunielewa hata kidogo, akaanza kutoa maneno ya kashfa na ya udhalilishaji juu yangu, huku akisema ni tabia za vijana wengi kusingizia kuibiwa mara wanapodaiwa nauli. Nikafadhaika! Maneno yale yalinifanya niwaze sana, nikaanza kujiuliza nikiwa msomi wa shahada moja ya elimu ya jamii, leo nadhalilika kwa kutokuwa na shilingi mia nne tu ya nauli? Konda yule akawa anaendelea kusisitiza kuhitaji nimlipe nauli yake. Dada mmoja kama malaika akajitokeza pasipo tarajia;...wakati nikiwa nimebakia nafikiria kumwambia konda anisaidie huku nikiwa na hofu kutokana na matamshi yake dhidi yangu, nikajikuta nadhamiria kumuomba anishushe. Hata hivyo kabla ya kuyasema hayo, nikasikia sauti ya kike kutoka nyuma ya kiti changu ikimwambia konda akate nauli yake na yangu.
Haraka niliyageuza macho yangu na nikajikuta yanagongana na ya msichana mrembo wa haja. Bahati kubwa hii? Nilijiuliza. Haraka nilimjibu "asante" nae akaachia tabasamu huku akinijibu "husijali kaka", Wakati huo huo konda alikuwa anarudisha chenji kwa yule dada. Safari ikaendelea. Nikajikuta mawazo yangu yanamkumbuka yule dada niliyemgonga pale posta, nikaanza kuhisi kuwa tukio lile lilipelekea kuibiwa pochi yangu bila kufahamu, sikumbuki ni muda gani nilibiwa lakini najua kuna mvulana alikuja na kumuuliza yule dada tatizo mahali pale. Wakati naendelea kuwaza...nikaanza kuwaza maisha yangu chuoni.
Nikawakumbuka marafiki ambao tulikuwa tukiambizana vyumbani wakati huo tukiwa hosteli kwa furaha na kupeana matarajio makubwa ya kuwa tukimaliza chuo, tutapata kazi nzuri, tutaishi maisha mazuri na hata kuwa na familia nzuri. Kila kitu kilikuwa kinakuja kama tamthiliya fulani ndani ya mawazo yangu, nikajikuta nachukia mfumo wa ajira ya nchi yangu hata mfumo wa elimu pia. Walimu wetu chuoni hawatuambii ukweli hali halisi ilivyo baada ya kuhitimu elimu yetu. Nikajikuta najichukia mwenyewe badala ya walimu hao. Nikaanza kuwakumbuka wazazi wangu waliokuwa kijijini Mbeya, wamejenga matarajio mema juu yangu, mwaka wa pili sasa nahangaika kutafuta kazi,kila mahali nilipotuma maombi yangu hakuna nilipoitwa kwa usaili. Maisha ya kuishi kwa watu yalielekea kunichosha, hata hivyo si mimi tu hata walezi wangu walianza kunichoka.
Nikaanza kuchukia ni kwanini nilitumia muda wangu mwingi kusoma, kusoma kusiko na faida? Kutokuwapo na kazi yenye kuniingizia kipato kukapelekea nimpoteze 'My Girlfriend' Binti yule wa Kimanyema niliyekuwa nafikiri ananipenda kwa dhati, kumbe alikuwa ananidanganya. Mwanamke niliyempata Chuoni, nilimpenda kweli kweli lakini baadae aliniacha kwa sababu sina pesa. Wako wapi wanaosema pesa haina umuhimu katika mapenzi?.Mnajidanganya. Nikaanza kuyakumbuka matendo yake kwangu,nyakati fulani alilia kwa ajili yangu hasa nilipomuuzi, alinihakikishia kuwa mimi ni wake na yeye ni wangu mpaka ndoa na hakuna kitakachotutenganisha. Kumbe nilikuwa napumbazwa.Nikajikuta nikiwachukia viumbe hawa wanaoitwa wanawake. Hata hivyo bado moyo wangu haukuepa maumivu yale. Sauti ya konda ilinigutusha kutoka katika lindi la mawazo yale, tayari gari limewasili kituoni, kituo kilicho pembeni na uwanja wa ndege. Haraka nilishuka nikaanza kutembea.
Sijui ni kitu gani kilinifanya nigeuke nyuma kabla ya kuvuka barabara. Nikajikuta nabakia na mshangao mkubwa! .Ndio! macho yangu yakakutana na binti yule mwokozi wangu, binti aliyenionea huruma na kunilipia nauli ya basi lile. Haraka nilimpa tena asante kwa msaada wake, binti yule akanijibu "nisijali", nilimuuliza wapi anapoelekea, alinijibu yeye ni mgeni mahali hapo na amekuja kumsubiri mgeni wake kutoka nje ya nchi, hata hivyo amewahi sana, atafika hapo masaa mawili baadae. Binti yule aliniomba nimuoneshe mahali panapopatikana chips nzuri apate kula, ni baada ya kumwambia mimi ni mwenyeji mahali hapo. Nikachukua jukumu la kumsindikiza, nilimpeleka kwenye Cafe zilizoko pale karibu na kituo cha tax.
Baada ya kufika pale nilianza kumuaga kwa minajili ya kuondoka. Binti wa ajabu alipinga uamuzi wangu, akaniomba tuwe pale tupate wote chakula na kinywaji kisha angeniruhusu kuondoka kama sitajali. Kumbuka sikuwa nimetia chochote tumboni kwa wakati huo,hakika sikujivunga.....nikavuta kiti na kukaa. Kuwepo kwangu na binti yule mahali pale kukapelekea kutambuana, alinifahamisha kuwa anaitwa Nadia, ni sekretari wa kampuni moja ya Bima nchini na yupo pale kwa ajili ya kumpokea rafiki yake mmoja. Nilijitambulisha kwake kuwa naitwa Richard Kamba.
Nilimuelezea maisha yangu kwa ufupi, hata hivyo sikuwa natambua kwanini namuelezea maisha yangu mtu nisiyemfahamu? Hata hivyo nguvu fulani iliniambia nimefanya jambo sahihi kwa wakati ule. Baada ya muda tuliachana na binti yule, alinipa Bussines Card yake, akinisisitiza kuwa nikifika nyumbani nimpigie, maana simu yangu nayo ilikuwa imeibiwa kwa tukio lile la Posta. Vile vile alinipatia noti ya elfu tano, bahati ilioje? kwa dakika zile nikajikuta nasahau yote. Nilipofika nyumbani nilioga na kupata chakula nilichokikuta, kazi ya kutazama vipindi vya television ikachukua nafasi yake kama ilivyo siku zote.
Hiyo ndio ilikuwa kazi kubwa nikiwa nyumbani, kushinda kwenye tv. Baadae nilipokumbuka kumpigia simu Nadia, nikatafuta Bussines Card ile bila mafanikio, sikumbuki wapi nilipoiweka, nilitafuta mwishowe nilikata tamaa. Na sikuiona tena. Maisha ya hapo nyumbani hayakuwa yenye furaha kwa upande wangu hata kidogo, sikuwa na kazi ya kufanya na muda mwingi niliutumia kukaa sebuleni na kutazama tamthiliya za kifilipino na baadhi ya filamu za Bongo movie yalikuwa maisha yangu ya siku zote. Mwaka sasa, bado ningali natafuta kazi na hakuna mahali nilipowahi kuitwa hata kwenye usaili tu. Walezi wangu walianza kunichoka taratibu hapo nyumbani hivyo nilianza kufikiria kurudi kijijini, mahali walipo wazazi wangu, hata hivyo bado moyo wangu haukuwa radhi kurudi Tukuyu. Sikuweza kukata tamaa. Tukio la ajabu likatokea....
***********************
Miezi miwili baadae nikapokea simu ya mdada mmoja huku akihitaji kuzungumza na Richard, bila shaka niliipokea simu ile na kuzungumza nae kwa umakini mkubwa, ndipo alipojitambulisha anaitwa Aisha ni Katibu Muktasari wa kampuni ya Tanzania Transport company, akinipa taarifa ya kuitwa kwenye usaili siku ya jumamosi ofisini kwao kutokana na maombi ya nafasi ya kazi niliyoomba miezi michache iliyopita. Hakika ilikuwa tukio lenye kuleta furaha sana kwa upande wangu.
Nikaazimia kushinda usaili huo. Jumamosi kwa upande wa Dar es salaam mara nyingi nyakati za asubuhi huwa hakuna shida ya usafiri, lakini mimi saa moja kamili ilinikuta nimeshafika Msasani mahali ilipo ofisi za Kampuni ile, nakiri kabisa sikuweza kupata usingizi usiku wa kuamkia siku yangu ya usaili. Hata hivyo niliwahi sana maana ofisi ile ilikuwa inafunguliwa saa mbili na nusu asubuhi na usaili ulipangwa kufanyika saa nne asubuhi, hata hivyo sikujali sana umbali wa muda huo. Nikasubiri kwa hamu kubwa. Baada ya kuvumilia sana huku nimekaa na watu nisio wafahamu malengo yao, tukaja kuitwa wale wote waliotakiwa kufanyiwa usaili siku hiyo, ndipo nikatambua sikuwa peke yangu, tulikuwa kama watu sita hivi.
Nikasogea na kukaa kwenye chumba ambacho kilitengwa maalumu kwa shughuli hiyo. Tukakaa kwenye benchi ya kisasa lililopo pembeni ya chumba kwa ajili ya kusubiriwa kuitwa. Muda Ukawadia na nikapigwa na bumbuwazi. Nilikuwa mtu wa kwanza kuingia chumba cha usaili, ikiwa ni mara yangu ya kwanza kufanyiwa usaili tangu nilipoanza kutafuta kazi, hivyo suala la hofu sikuweza kuepukana nalo. Hofu ikanitawala. NI wakati ambako nilisikia sauti kwenye masikio yangu ikaniambia "Richard ondoa hofu uliokuwa nayo, jiamini kwa sababu hii ni nafasi muhimu ambayo umeipata, shinda hofu hii" Kauli hiyo ilisambaa kwa kasi ya ajabu masikio mwangu, haraka nikashusha pumzi kwa nguvu zote.
Wakati huo tayari nipo ndani ya chumba kizuri ajabu. Chumba chenye kunakshiwa na rangi nzuri na vitu vya thamani kubwa.Chini ya chumba kile kulitandikwa zulia zuri jekundu, pembeni ya ukuta kulikuwa na tv nzuri ya kisasa iliyokaa vyema ukutani pale. Macho yangu kwa kasi ile ile yakaendelea kusawiri chumbani mle. Hakika ni chumba kilichokuwa kinavutia sana kwa harufu nzuri iliyosambaa chumbani mle ,huku hali ya kiubaridi ikitawala kwenye chumba kile. Wakati ukawadia. Wakati nikiendelea kustaajabu uzuri wa chumba kile ghafla sauti ya kike ikasikika " Naitwa Nice Abdalah ni Afisa Uajiri wa kampuni hii na nipo hapa na Afisa habari Mr Salim Mhando, karibu sana ndugu" Wakati huo nilimuona yule dada akivua mawani yake kwa utulivu husio kifani.
Ni wakati huo huo macho yangu yalipokimbia maili nyingi kwa kasi ya ajabu na kutua usoni mwa msichana yule. Nikashtuka! Sikuamini macho yangu kwa wakati ule. Haraka kumbukumbu zangu zikarejea kwa kasi ya ajabu, nikajiuliza wapi nilimuona binti huyu? wakati huo huo mapigo ya moyo wangu yakawa yameongezeka kwa kasi isiyo ya kawaida. Ni wakati ambapo moyo wangu ukahisi hali ile ile, hali ambayo niliwahi kuhisi kipindi fulani uko nyuma. Naaam! haraka nikamkumbuka..."Ndiye huyu! ndiye yeye hasa" Nikajiambia... .
Ni binti yule yule ambaye nilikutana nae Posta na kumgonga kwa bahati mbaya tu kama nilivyohisi kwa upande wangu , ni binti huyu ambaye alinifanya nipewe maneno ya kashfa na konda, ni binti huyu ambaye alinifanya nipoteze simu yangu ya thamani wakati wa tukio lile. Badala ya kuanza kumchukia nikajikuta nabakia kutabasamu..tabasamu la uongo. Tabasamu la kihisia! nikajikuta najitambulisha..."Naitwa Richard Kamba na nipo mahali hapa kwa ajili ya usaili" Wakati najitambulisha macho yangu yalikuwa yanamtazama binti yule ambaye naweza kusema kwa wakati huo ni adui yangu. Hata hivyo sikuona chochote kilichobadilika usoni kutoka kwa binti yule mrembo. alionesha sura ile ile yenye kuvutia. Ajabu ilioje?
***************
Nilianza usaili ule kwa kujibu kila swali kwa umakini mkubwa na uwerevu wa hali ya juu, majibu yangu yalionekana kumfurahisha sana Afisa habari wa kampuni ile, wakati wote kila nilivyokuwa nikijibu kwa umahiri mkubwa alikuwa akibakia akitabasamu na huku akiandika kitu nisichokifahamu kwenye 'Note Book' yake. Ndipo binti yule mrembo aliponiuliza swali ambalo lilionekana kama la mwisho kwa upande wangu. Aliniuliza: " Unataka ulipwe mshahara kiasi gani?" Hakika lilikuwa swali gumu kulijibu na kuna sauti nikaisikia masikioni mwangu ikinisisitiza nilijibu swali hilo kwa uangalifu wa hali ya juu.
Nikajibu: " Napaswa kulipwa kutokana na kiwango ambacho kampuni hii imekitenga kwa ajili ya nafasi ninayoiomba. Napaswa kulipwa kutokana na utendaji wangu na kiwango cha faida nitakachokiletea kampuni. Pia napaswa kulipwa kutokana na kiwango cha elimu yangu" Nikamaliza kulijibu swali lile. Na kuwatazama wale watu wawili hapo hapo nilimuona yule afisa habari akitabasamu na kumuangalia binti yule kwa furaha hata hivyo sura ya binti yule ikabakia vile vile katu haikujibu tabasamu la afisa habari yule. Nikafadhaika! Baada ya usaili niliruhusiwa kuondoka mahali pale huku yule afisa habari akinipa pongezi za kipekee na kunipa matumaini makubwa juu yangu ya kupewa ajira katika kampuni ile.
Tofauti na yule binti mrembo yeye aliguna tu. kisha akafunga kitabu chake na kuvaa mawani yale ambayo yalionekana wazi ni ya macho. Nilitoka ndani mle nikiwa nusu nina furaha na nusu nikiwa na huzuni, hasa nikikumbuka kuwa binti yule mrembo alikuwa ni kama ufunguo wa ajira yangu, ni yeye ndie atakayeamua nafasi yangu, Nikasali! nikasali! Nikasali kwa Mungu wangu nishinde usaili ule.
**************
Wiki zikapita, hadi miezi ikapita, sikuwahi itwa na kampuni ile kwa ajiri ya ajira. Hakika nilikata tamaa kabisa ya kuajiriwa na nikatamani kujiajiri mwenyewe hata hivyo nilikosa mtaji wa kuanzisha biashara. Mjini nikapaona pachungu huku manyanayaso yakizidi toka kwa walezi wangu. Maisha yalikuwa magumu sana, Mwanaume mimi nilikosa hata pesa ya vocha. Wakati mwingine nilitegemea chenji zinazotokana na mahitaji madogo ninayotumwa kwenda kununua na kiasi kidogo kinachobakia ndio hutumia kununua vocha. Nilikata tamaa ya maisha.
Nikazidi kuchukia muda wangu niliyoupoteza kuitafuta elimu. Wakati ukawadia. Ni siku chache baadae nikaliona tangazo kwenye gazeti la serikali kuhusu nafasi za ajira kutoka shirika la ndege ya Ethiopia, ambalo limefungua tawi hapa nchini. Niliandika maombi yangu na kuambatanisha CV yangu yenye nyaraka za kuthibitisha kile nilichokiandika kwenye wasifu wangu haraka nikatuma. Wiki moja baadae niliitwa kwenye usaili. Baada ya siku tatu kupita nilipokea simu ya kuhitajiwa ofisini kwa kupeleka nyaraka zangu halisi ni baada ya kuelezwa kushinda usaili niliyofanya.
Kila kitu kilienda kama simulizi nzuri ya kuvutia. Hatimaye nikaajiriwa rasmi kama Afisa wa IT yaani 'Information Technology' Kumbuka nina shahada ya kwanza ya IT kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Maisha yakaanza kwa upande wangu. Nilianza kazi kwa juhudi kubwa na kujituma kusiko kwa kawada huku nikiazimia kufidia muda wangu nilioupoteza kwa kipindi chote. Miezi minne baade niliomba kuhama na kuanza maisha ya kujitegemea. Ilikuwa jambo gumu walezi wangu kunielewa hawakupenda kuhama kwangu kwa haraka kwa kipindi hicho. Nilijaribu kuwashawishi na mwishowe wakakubaliana na uamuzi wangu. Wakati huo huo nikaanza kujiuliza inakuwaje sasa wananipenda, wananililia nikae pale ilhali kipindi sina kazi walikuwa wananinyanyasa? Huku wakinishinikiza nirejee kijjini ....
Nikagundua kuwa ni kwa sababu ya kazi yangu, nikasema kwa sababu ya pesa. Hakika pesa ni kila kitu "Nikawaza|". Nilipanga chumba na sebule eneo la Mbezi Kimara, mbali na mahali walipo walezi wangu. Sikutaka kukaa karibu na wao. Nilitaka kuwa uhuru zaidi katika eneo jipya. Miezi michache baadae nilibahatika kupata mkopo ambao niliutumia kununua vitu vya ndani kama Tv, masofa ya kisasa na vingine vingi. Sasa chumba changu kikaanza kuwa na mwonekano mzuri na wenye kuvutia. Pia ukumbuke kwa kipindi hicho sikuwa na msichana hata mmoja, hakika niliwachukia wanawake. Kila siku inayokwenda ,nilimuomba Mungu anioneshe mke wangu kwa sababu wakati huo sikuwa nawaamini wanawake pamoja ya kukutana na vishawishi vingi kwa wakati huo.
******************************
Mwaka mmoja baadae kupitia akiba niliyokuwa nikijiwekea nilifanikiwa kununua kiwanja maeneo ya Chamazi. Nilianza kufurahia maisha na hata mwonekano wangu ulianza kubadilika nilikuwa mvulana mtanashati sana, kila mmoja aliyepata kuniona kabla ya kuajiriwa alibaki akipigwa na bumbuwazi mara tu alipopata bahati ya kukutana nami. Nilikuwa mwaminifu na mtiifu sana kazini. Uwezo wangu wa kufanya kazi bila kuchoka, ushirikiano wangu na wafanyakazi wenzangu uliwavutia wakuu wangu wa kazi. Hivyo nikajikuta nakuwa mwakilishi wa shirika sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi.
Kote huko nilipopitia shirika lilikuwa likipata sifa kupitia mimi. Nikafarijika sana na kuendelea kufanya kazi kwa bidii zaidi. Jambo nisilotegemea likatokea! NI miaka miwili baadae yaani miaka miwili na miezi sita tangu niajiriwe kwenye shirika hili. Tukapata msiba mzito wa kuondokewa na Meneja wa shirika kwa upande wa Tanzania. Kifo cha meneja huyu kilikuja baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Tazara wakati huo akielekea nyumbani kwake Tuangoma Mbagara.
Baada ya kumalizika shughuli nzima ya mazishi ya meneja wetu. Wiki moja baadae nikaripoti kazini. Niliwasili jumatatu ya asubuhi kama kawaida yangu na baada ya kuwasilimia marafiki zangu nilielekea ofisini kwangu. Hata hivyo nilijikuta nikiwa na maswali mengi baada ya secretary wa ofisi ya meneja kunichangamkia kusiko kawaida huku akinitizama kwa tabasamu fulani lenye kumaanisha kuwa kuna jambo muhimu angependa kuniambia. Wakati huo bado miguu yangu na akili yangu nilishavilelekeza kuelekea ofisini mwangu. Niliingia ofisini mle kama ilivyo kawaida, na kukuta bahasha imewekwa juu ya meza yangu ikiwa imeandikwa jina langu .
Nilishtuka sana, na kwa kasi ya ajabu haraka niliifungua barua ile na kuisoma kwa muda ule ule huku ningali nimesimama. "Mungu wangu!" Nilijikuta natoa sauti hafifu huku nimepigwa na butwaa. Mle ndani ya barua ile ambayo nimeisoma kuwa imetoka makao makuu ya shirika likitoa taarifa ya kuteuliwa kwangu kuwa meneja mpya wa shirika la ndege la Ethiopia Airline. Kila kitu kilikuwa kama tamthilliya fulani ya kifilipino, nikajihisi kama nipo ndotoni. Nilifumba macho na kufumbua tena bado macho na akili yangu yaliniambia kuwa sio ndoto. Ni ukweli halisi. ITAENDELEA.......