BUMIJA
JF-Expert Member
- Oct 19, 2011
- 6,249
- 11,924
Katika maisha yetu ya kila siku hatuijui kesho yetu.Wengi wetu tuna dini zetu ama hatuna dini lakini lipo tumaini ambalo mioyo yetu imeshikilia.
Miaka flani nilikua nikifanya kazi wilaya B huko mkoa wa X. Miaka ile ukihitimu ualimu unapangiwa kazi moja kwa moja wala haina longo longo. Mwaka 2007 nikiwa chuo fulani nimetoka bafuni nikasikia makelele ya post hizo za ualimu kutoka.
Ualimu Miaka ile ilikua ndio kimbilio la watoto wa wakulima maana ilikuwa ni kazi ambayo unapata post mapema. Mshahara ulikuwa ni mdogo lakini bidhaa zilikuwa chini.
Miaka ile post zinatoka hata mtihani hamjafanya wa Diploma. Chuo nilichosoma kipo uchagani ila sitakitaja. Miaka ile naanza kusoma pale chuo nilikuwa sijawahi kukutana na msichana yeyote yule na nilikuwa na miaka yapata 19 hivi.
Basi bwana katika pitapita maeneo ya karibu na chuo huko nikamuona Dada Fulani anaitwa Upendo. Dada alikuwa ni mzuri sana machoni pangu na nakumbuka wakati namuona nilikuwa nakatiza mitaa nilimuona na jamaa yangu anaitwa Mlai jamaa mmoja hivi wa kichaga. Huyu jamaa yangu alikuwa anapenda sana kuvuta sigara muda mwingi.
Basi tukawa na mazoea tukipata muda tunaenda pale stationery tunakaa kwa nje pale na kulikuwa na viti vya plastiki pale nakumbuka.
Huyu ndie mwanamke wangu wa kwanza kumpenda haijawahi tokea. Nilikuwa nikilala bwenini pale namuwaza mwanamke muda wote japo sikufanya naye mapenzi hata siku moja. Huyu Dada Upendo alikuwa amenielewa nia na lengo langu.
Miaka ile ikumbukwe ugonjwa huu wa Ukimwi ulikuwa bado unaogopeka sana na dawa hizi za kupunguza makali zilikuwa sio sana.
Nilikuwa bado naogopa sana kutembea na mtu ambae hatujapima nae.
Nitaendelea na hii stori pindi ambapo tulifikia, makaribio ya kufanya mtihani wa mwisho kuajiriwa na nini kilitokea mpaka kufungiwa mshahara.
Usiombe ufungiwe mshahara na hujui hatima yake. Sitasahau maumivu yake mpaka siku nashuka kaburini.
Nitaelezea pia namna gani iliniingiza kwenye uraibu wa ulevi kupindukia nikiwa masomoni.