Sitakwenda tena Kanisani

Sitakwenda tena Kanisani

Tee Bag

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
7,220
Reaction score
5,626
SITAKWENDA TENA KANISANI

Mwaka Fulani Nilipata Nafasi Ya Kuwatembelea Ndugu Ambao Walikuwa Wakiiishi Mbali Na Mkoa Niliokulia. Ilikuwa Furaha Iliyoje Kutokana na Kutoonana kwa Mda Mrefu. Nilipokelewa Vizuri Sana Siku Niliyofikaa.

Maisha ya Ugenini Yakaanza, Yalikuwa ni Ya Kawaida Kwangu Maana ni Kama Nilikuwa Nyumbani tu. Niliendana Na Wenyeji Wangu Kwa Kila Kitu. Kasoro Katika Suala La Kwenda Kanisani. Ndiyoo Hatukuendana Kutokana na Mazingira Niliyokulia Wakati Wa Ujana Wangu Sikuwa Mtu Wa Kwenda Kanisani Kabisa. Nakumbuka Utotoni Ndiyo Tulikuwa Tunaenda Kanisani Kila Jumapili.

Nikakumbuka Maisha ya Sunday School Enzi Hizo.Tukishika Vifungu Vya Biblia na Kuvitumia Kama Salamu Kila Mwalimu Aingiapo Kutufundisha. Nkakumbuka Salamu Moja Tuliyokuwa Tukiitumia Sana Yohana 3:16 "Kwamaana Jinsi Hii Mungu Aliupenda Ulimwengu, Hata Akamtoa Mwanawe Pekee Ili Kila Amuaminiye Asipotee,Bali Awe na Uzima wa Milele" Shikamooo Mwaaaalimuu.

Basi Nkapata Shauku Jipya la Kwenda Kanisani. Nkawaambia Wenyeji Wangu Jumapili Tutakwenda Sote Kanisani Walifurahi Sanaa. Jumapili Asubuhi Na Mapema Nkajiandaa Vizuri Sana. Hakika Nilipendeza Kama Naelekea Ofisini Vile. Kwa Kunitazama Ni Kama Mfanyakazi Wa Benki Kuu. Kumbe Ndo Nimetoka Kufeli Kidato Cha Nne, Nimekuja Kuipotezea Aibu Tu Ugenini Huku.

Tulifika Kanisani Watu Walikuwa Wakutosha Kiasi Chake.Kiasi Kwamba Jengo lilielemewa na Uwingi wa Watu Jumapili Ile. Nilikaa Upande wa Kushoto Usawa wa Dirishani Kabisa Hivo Kila Mtu Aliweza Kuniona.

Kabla ya Ibada Yakapita Matangazo na Kisha Utambulisho Kwa Wageni. Tulikuwa Wageni Watatu Tu Wakiume Wawili na Mama Mmoja Wa Makamo Ivi. Alianza Yule Mwenzangu Kujitambulisha Kwa Kusema "Ametokea Kijijini Baada ya Kupata Ajira Katika Kiwanda Cha Saruji. Hivyo Atakuwa Akiishii Mjini Pale Na Kuanzia Siku Ile Atakuwa Akisali Pale.Akapigiwa Makofi na Vigeregere Vingii.

Nikafuatia Mimi Sikuwa na Maelezo Mengi Zaidi ya Kumtaja Mwenyeji Wangu Aliyenileta Pale Kanisani. Kisha Akamalizia Yule Mama wa Makamo Akasema Yeye Ni MfanyaBiashara na Mhubiri Wa Injili Toka Usharika Wa Mjini Pale.Basi Mhubiri Mwenyeji Akampa Nafasi Ya Kuhubiri Yule Mama Wa Makamo Siku ile.

Mahubiri Yalipoisha Mhubiri Mwenyeji Akasimama Madhabauni Kisha Akatoa Matangazo Mengine na Kubwa Zaidi Ilikuwa ni Kuhusu Ujenzi Wa Kanisa Kubwa Lililokuwa Pembeni Ya Jengo Lile. Akasema Inahitajika Michango Na Tutaanza Na Wageni Kisha Wenyeji Wataendelea.

Alianzia kwa Yule Mama Wa Makamo Yule Mama Akasema Anatoa Laki Moja Kwa Ajiri ya Ujenzi. Akafuatia na Yule Mwaume Mwenzangu Akasema Anatoa Elfu Sabini Na Tano kwa Ajiri ya Ujenzi.

Ilipofika Zamu Yangu Ikawa Shughuli. Mfukoni Nina Mia Tano Ya Sadaka Ambayo Alinipa Mwenyeji Wangu. Watu Wote Kanisani Wakawa na Shauku la Kuniona Ntasemaje. Kwa Muonekano Wa Nje Nilionekana Kama Mtu Anayejiweza Sana. Kumbe Sikuwa na Chochote Zaidi ya Ile Mia Tano.

Mhubiri Mwenyeji Akaongezea Msumari Wa Moto Moyoni Mwangu. Akasema Bado Mgeni Mmoja Kule Upande wa Dirishani. Nikajikausha Lakini Watu Wote Wamenigeukia Mimi.Moyoni Nkajisemea Kwanini Nilikuja Kanisani Ona Naumbuka Sasa. Aibu Ikanitawala Miguu Ikatetemeka Nkasimama kwa Wasi Wasi na Aibu Kuu. Huku Midomo Ikintetemeka.

Nkapata Ujasiri Wa Kudanganya Tu Ili Niepukane na Fedhea Ile. Nkasema Naahidi Kutoa Mifuko Mitano Ya Saruji.Hivyo Nitaiwasilisha Jumapili Ijayo.Tofauti na Wenzangu Walipomaliza Kutaja Michango Yao. Walipigiwa Makofi na Shangwe za Vigeregere.Kwangu Ilisikika Miguno na Maneno ya Chini chini Kuonyesha Hawaniamini Kwa Ahadi Ile.

Nkajiona Sina Thamani Pale Kanisani Aibu ikanitawala Mpaka Ibada Inaisha.Hata Sikuelewa Iliishaje Naona Kwa Sababu Nilikuwa na Mawazo Kichwani. Tulipotoka Hata Sikugeuka Nyuma Tena Nilipofika Nyumbani. Nikatafakari Sana Tukio Lile Nikajisemea Moyoni "Sitakwenda Tena Kanisani".

By Aswile Mwanyasi
0754426142
FB_IMG_1563700662776.jpeg
 
Umedanganya nafsi yako ndio maana unajutia ,siku nyingine sema ukweli mfano sina cha kuchangia adi wakati mwingine.
Me kanisani waliwai nisimamisha ,nikasema mbele yao leo nimekuja kusali sikujiandaa na mchango na siwezi weka ahadi yoyote.
 
peleka mifuko ya watu mkuu,,,
tehteh eti jumapili ijayo,,usingetaja lini utatoa ,,
Image result for mifuko ya cement
 
Hilo ni kanisa dhehebu/jengo. Hakuna mafundisho halisi ya Kristo hapo. Wewe usiache kwenda kanisani kwa sababu hiyo.
 
Kwani ukiacha kwenda kanisani utakua unamkomoa nani..?
 
USIACHE KWENDA KANISANI kwa sababu tu kanisa ulilokwenda ni FEKI- halifuati Biblia inavyoagiza. Yesu alisema wazi NI MAKOSA MBELE YA MUNGU KUTANGAZA KIWANGO CHA SADAKA MTU ANACHOTOA. Yesu alisema:- "Wewe utoapo sadaka hata mkono wako wa kushoto USIJUE ufanyalo mkono wako wako wa kuume. Maana yake sadaka yako inatakuwa iwe SIRI hata kwa mkeo. SIO ITANGAZWE KWA WAUMINI WOTE WALIO KANISANI. Kwa sababu hiyo, usiache kwenda kanisani. Badala yake, mwombe Mungu akuonyeshe ni kanisa gani unatakuwa uwe unaenda. Ukiomba hivyo iko siku utakuja kujua ni kanisa gani Mungu anataka uwe unaenda
 
Sijaelewa dhumuni la kuweka namba yako hapo, weka wazi.... unataka tukuchangie ili ukatimize ahadi yako..!!
 
Back
Top Bottom