Sitaki mwanangu ajiingize kwenye tasnia ya sanaa yoyote

God'sBeliever

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
5,788
3,028
Nakereka sana napoona vijana wengi wadogo wanapotea baada ya kujiingiza kwenye maswala ya muziki, kuigiza, mashindano ya miss sehemu flani, miss tanzania, michezo ya mpira, netball na dancing.

Sitaki kabisa na narudia tena sitaki kuona mwanangu anaingia katika hizi fani.
sababu kubwa ni ugumu wa kazim na vishawishi vingi, mtoto akishindwa kupambana anatoa mwili wake anatumika mno na ubaya zaidi anaweza pata UKIMWI na mimba huu na wakiume akishajipeleka kwa mashuga mami ndo kwa heri.

Nachukia sana watumishi wengi pamoja na wahusika kibao walioko kwenye hio fani wamekuwa wakiwafaidi sana watoto wetu, kuwadhalilisha, kuwaibia haki zao na matendo mengine kinyume na miili yao.

Madawa ya kulevya, uhuni na kushindwa kuendela na masomo ni side effect za hizi kazi.
nyie wenyewe ni mashuhuda mtu ukiwa maarufu hasa ukiwa mwanamke usipoweza kujisimamia na kama una akili ndogo wallah wenye nchi watakufanya sana. na ndo maana ndoa nyingi wa wanawake wabongo hazidumu sababu unakuta mwanamke keshatumia hadi basi na ubaya zaid milango yote haifungi.

Hii tasnia imekaa pabaya sana kulingana na sehemu wanazofanyia kazi ni maeneo ya starehe na kule lazima uliwe tuu na usipokua makini unaukwaa ukimwi halafu watanzania wanakuja kusema ooh ni kifua, sijui malari sijui nini kumbe wapi miwaya imekuchukua.
mitaani nako kuna usumbufu ila sio sana maana ukishajiweka public ukijulikana lazima utaonekana tuu na mitandao ya kijamii ilivyo utaliwa tuu.

Naanza kuchukua sheria kali kwa wanangu na ndugu zangu wa karibi na marafiki, pesa zipo sio huko kwenye sanaa tuu.

Narudia tena UKIMWI upo mjikinge popote pale mlipo, maeneo ya starehe kama bar, matamasha n.k muwe makini huko kuna watu wa kila aina na penye wengi pana mengi.
======

FAHAMU: Mada hii imesomwa kwenye kipindi cha Jamii Leo.

Tazama video hapa =>>: JAMII LEO: Yaliyovuma JamiiForums, Jumatatu Julai 18, 2016 - (Video)
 
Attachments

  • index.png
    index.png
    8.7 KB · Views: 59
Ingekuwa heri wakiyasoma maandiko yako wasiifanye migumu mioyo yao.
 
unamhofia sana mwanao kwa kuwa huiamini akili yake iliyojengwa na malezi yako mwenyewe.....

kama hukumlea vyema , hata akipatiwa kazi ya ofisi bado atatumiwa kama kiburudisho kwa wakuu wa idara na vitengo
hapana mkuu ana heshima yake tuu nzuri ila hayo maeneo ya vishawishi ni hatari zaid
 
Ukimwi upo kokote sio kwenye sanaa tu, wakina mzee Majuto wapo kwenye sanaa miaka nenda rudi ila bado wanaendelea kudunda hadi uzeeni, wengine mtaani hata sio wasanii but unakuta wanakufa na ukimwi wakiwa na miaka 30 tu
 
ndio hilo linawezekana ila mtoto wa kike ni risk sana hata dume linapaswa lionywe. huyo majuto itakua alipewa malezi mazuri na anajilinda, we huoni ni mjanja sana
 
Hata hao mastaa unadhani walipenda inatokea tu automatically
 
umalaya ulioko kwenye damu kamwe hautoki mpaka mhusika anaingia kaburini, kuna wanaopenda na wengine wanafanya sababu ya dhiki/shida na aibu watakayoipata pale watakapoweka mambo yao hadharani hivo wanaamua kujitoa miili yao waingize pesa za kujikimu unajua tena ukiwa star ni mzigo huwez kuwa huru
 
Ni kweli ila ukiangalia wasanii wengi wametoka familia za dini
Mfano LINAH jide ruby walikuwa waimba kwaya kanisani
Alikiba baba yake alikuwa sheh na yeye na fa wamesoma Sana dini (madrassa) walikuwa waimba qaswida
Nisha director yule baba yake ni geordavid Ana kanisa kubwa ni mtumishi wa mungu
Ndo maana nikasema inatokea automatically huwezi zuia kwa kweli
 
sawa
 
Usitukane mamba kabla hujavuka mto
Yule masogange baba yake nilisikia hakutaka mwanae awe kwenye sanaa lakini ndio kama vile wamuona
 
sijamtukana mtu mkuu ila namuomba MUNGU Anisaidie yani yale mazingira nayaogopa sana
 
Jitahidi umpe malezi mazuri vile mwanao unataka aje kuwa kwa siku za baadae coz mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, kwa kufuata mila, desturi na dini kwa ujumla.

Uigizaji, muziki, michezo ya mpira sio uhuni bali ni kazi kama kazi nyingine na pia tunajifunza kwa wenzetu nchi zilizoendelea thamani yao na kwa jinsi wanavyothaminiwa na mashabiki wao na serikali zao kama vioo vya jamii.

Wapo wanamuziki, wanamichezo na waigizaji wenye ndoa zao na wanakuwa na heshma na kuthamini familia zao, jamii inajifunza kuelimika na kuburudika kupitia vipaji vyao.

Unaweza kumuandalia vizuri future ya mwanao kwenye elimu akifika chuo kikuu akabadilika tabia zake, au akabadilika baada ya kupata kazi na pesa baada ya kuanza kujitegemea kimaisha, pia anaweza kubadilika ndani ya maisha yake ya ndoa.

Wasanii wa muziki, waigizaji na wanamichezo wabadilike, wajithamini na wajitambue wao ni vioo vya jamii
 
nice
 
Watoto wenyewe wa kuchaguliwa fani wa kizazi hiki ambao wakitaka jambo lao liwe linakuwa? hili jambo zito sana ndugu fanya malezi na muombe mola wako akuongozee kama mdau katoa mifano ya uliotoka penye migongo ya dini wakaanzia kuimba huko kisha wakabadili gia angani.
 
hali ni ngumu
 
Mmmmh! mie kijacho wangu nataka siku moja asimame jukwaa la miss Tanzania Labda tu afuate limwili la baba yake
 
Wa kwako kama atafuata mwili wa baba yake basi atakuwa na kipaji kama GIGY
 
Back
Top Bottom