Sitaki kuamini kuwa social media hazina msaada wowote kwa viongozi wetu

baba anjela

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
431
310
Mimi naamini social network au social media ni sehemu ambayo kiongozi unaweza kupata kero nyingi na mambo mengi yanayowakumba au kuwa kero kwa wananchi unaowatumikia, siyo rahisi kwa kiongozi au vyombo vya habari vya serikali kuwafikia wananchi na kuweza kukusanya kero...zao..ila pale viongozi wanapopuuza kile kinachoongelewa na wananchi wao kupitia social media,wajuwe hawatutendei haki.nijukumu lao kuchuja kipi cha kufanyia kazi na kipi cha kupuuza... icho ndicho chakufanya.

jamani lazima tujuwe nani mwajili na nani mwaajiliwa... mimi na amini viongozi wote mliochaguliwa na kura au kuteuli wa nyote mmeajiliwa na wanachi na si vyama vyenu... hivyo ni muhimu wakatusikilliza sisi kwanza kabla ya ilani zao za vyama vyao.

viongozi ni muda wakutambua bosi wenu sichama chako bali ni sisi wananchi...msitujali tu kipindi cha kampeni ...baada kuwaweka madarakani..mnatupuuza...ni mbaya mno...

jaribuni kuheshimu maoni yetu kwanjia yoyote tutakayo wafikishia ili mradi njia hizo hazivunji sheria za nchi..

lazima mjuwe chama ni utambulisho tu wapi unatokea, ila wananchi ndiyo wenyemamlaka ya kukupa wewe hiyo nafasi ili uwatumikie wao na sikutumikia chama chako..

viongozi lazima mtambue muda wa mwananchi kuchagua chama ulishapitwa...leo wananchi tunachagua mtu... hivyo tambueni bosi ni sisi wananchi wala sichama chako...kero za wananchi ndiyo ilani yako ya kwanza...alafu ilani yako ya pili ni ile inayotokana na chama chako
 
Back
Top Bottom