MAHELO. E.B
Member
- Aug 13, 2013
- 27
- 6
SITAKI KUAMINI KUWA PESA INA NGUVU KULIKO SHERIA.
Inasikitisha kuona watuhumiwa dhidi ya MAUAJI ya Bi. Stephano Bahati (14/05/2010), aliyekuwa Katibu wa CCM kata ya Isamilo jijini Mwanza wote wameachiwa huru leo tarehe 11/10/2013. Kibaya zaidi aliyekamatwa (kwa jina Jumanne Osca) akikimbia baada ya kufanya tukio la mauaji nae kaachiwa huru baada ya Jaji kukataa ushahidi uliotolewa mahakamani na Mkemia mkuu kuwa damu iliyomwagika ofisini alipochomewa kisu marehemu hadi kufa ilikuwa inafanana na damu iliyokuwa kwenye nguo ya muuaji (ndugu Jumanne Osca) pamoja na mnuso wa mate yake.
Kesi hiyo ya mauaji ilimuhusisha aliyekuwa Meya jiji la Mwanza (Biyondo) baada ya bwana Jumanne Osca kudai kuwa alikodiwa na huyo aliyekuwa Meya kutekeleza agizo la kumuua kwa ahadi ya kupewa donge nono la pesa.
Wakati huo huo ndugu Jumanne Osca aliwashangaza askari magereza kutoka mkoa wa Tabora baada ya kumkuta Gereza la Butimba mkoa wa Mwanza. Kilichowashangaza ni kumkuta Jumanne Osca Butimba gerezani kwa kosa jingine la mauaji, ikiwa na maana kwamba ndugu Jumanne Osca alitoloka kutoka gereza lililoko mkoani Tabora alipokuwa amefungwa kwa kosa la mauaji.
Baada ya Jaji kuwaachia huru imekuwa kama tamthilia na kusababisha gumzo kuanzia ndani ya hiyo Mahakama kuu iliyopo Jijini Mwanza hadi maeneo mbalimbali ya mjini kati.
Wananchi wengi wamesikia wakisema wajipange vema kuiadhimisha siku ya kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa (Mwl. J.K. Nyerere) wakida alizikwa na sheria zote za nchi hii. Sheria zote zilizobaki ziko chini ya sheria mama iitwayo MONEY LAW (sheria pesa).