Sitaisahau siku hii ya Alhamisi

Kichaa Msafi

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
1,087
2,133
Habari zenu waungwana,
Hongereni kwa kazi na poleni kwa ukata tulionao.

Nije kwenye mada, mwaka 2010 mwezi wa 12 tarehe 23 siku ya alhamis pale Dodoma nilipatwa na tukio moja lililoniacha kinywa wazi. ilikuwa hivi, nimetoka zangu chuo udom nikapita homu makole ndo nilikopanga, nikaweka baadhi ya vitu vyangu kisha nikatoka nikaenda pale dodoma hotel kumsalimia kaka yangu alikuwa anapaki tax yake pale,

Ile kufika pale nikasalimiana na wale marafiki zake na kaka kwani yeye sikumkuta, ile bado sijakaa sawa kuna mtu alikuja na kuniomba pembeni kidogo tuongee, ile namkaribia tu akanitia tanganyika jeki, na kuniambia nipo chini ya ulinzi, baadaye niligundua kwamba ni polisi, nikamuuliza kosa langu akaniambia ntaenda kulijua huko kituoni,wale madereva wakawa wanashangaa tu imekuaje,

Yule polisi akanipeleka mpaka kituoni pale stesheni kwenye kighorofa cha kwanza, kufika kule namkuta dada mmoja anamimba halafu analia vibaya sana, polis akamuuliza ndio huyu, bila kupepesa macho akajibu ndio huyu, nikabaki nashangaa imekuwaje, kuna polisi mmoja alikuwa wa kike akanipiga kibao cha nguvu kidogo na kusema yaani wewe kaka unaonekana mzuri na mpole wa sura kumbe ni mwizi na tapeli,

Nikashtuka nikamuuliza kwa nini umenipiga na nimemtapeli nani,akaniambia nifunge mdomo wangu, basi yule polis aliyekuja kunikamata akamwambia yule dada aeleze ilikuwaje, akasema hivi. Nilimnukuu.

Mimi nimetoka Dar es Salaamu na basi la shabiby, ili nije kupanda treni niende nyumbani kwetu sumbawanga, baada ya kufika hapa dodoma stand huyu kaka alikuja kwangu na kunionyesha simu hii kwamba anaiuza, akaionyesha ilikuwa ni motorola bapa, akaniambia anaiuza elfu 80,

Mimi niliipenda nikamwambia nina elfu 50, akakubali nikainunua, aliniambia niifiche kwasababu ni ya dili, hata sikuikagua tena sababu mara ya kwanza niliiona kuwa ni simu na hata kuiwasha niliiwasha, basi nilivyompa pesa na yeye alivyonipa simu nikaitia kwenye mkoba na kuondoka pale stand na nikaja hapa stesheni ili nikate tiketi ya treni kwenda sumbawanga,

Baada ya kufika hapa nikaamua nitoe line kwenye simu yangu hii,(ilikuwa vodafone vile vidogo) niweke humu kwenye simu aliyoniuzia huyu kaka, kufungua kifuniko cha nyuma ili niweke line nakuta kuna sabauni na sarafu ya sh 20 na wala sio simu, nikachanganyikiwa na wakati nawaelezea watu ndo nikamwona huyu kaka aliyeniuzia hii simu akiwa pale kwenye tax ndo nikaja hapa kituoni kutoa taarifa ili mnisaidie. mwisho wa kunukuu.

Kiukweli nilichoka sana baada ya kusikia maelezo yale, nikaulizwa umesikia maelezo ya huyu dada nikasema ndiyo, nikaambiwa sasa nijieleze, nikajieleza kuanzia naamka mpaka nimeenda chuo yaani nilijieleza mizunguko yangu yote kuanzia kuna kucha, yule askari wa kiume akamwambia yule dada kafananisha lakini yule dada alikaza sana kwamba ni mimi tu,

Kaka yangu alivyorud trip yake akaja juu na madereva wenzake wakajitahidi kuwaelezea polisi kwamba mimi kila siku baada ya chuo lazima nije pale na yule dada atakuwa kafananisha, lakini haikuwezekana dada anadai alipwe pesa zake tu,

Alipokuja mkuu wa kituo nae akajitahidi kumweleza yule dada kwamba kafananisha, yeye akasema kama polisi wale hawawezi kumsaidia basi yeye ataenda mpaka ofisini kwa RPC akeseme kwamba yeye kamwona mwizi wake polisi hawataki kumkamata, basi kwa kuwa ilikuwa jioni karandinga ya polisi ikaja kuchukua wahalifu wengine ili wapelekwe kituo kikubwa, kaka yangu na wale madereva wengine wakachangishana fedha na kuamua kumlipa yule dada ili mimi nisiende kulala kituoni.

Nikaachiwa pale lakini wakati ninashuka chini akili ikaniambia niwaombe maaskar wamsachi yule dada kwenye mkoba wake isije ikawa anazo simu nyingi za vile na ukawa ndio mchezo wake kuwabambikia watu, kweli baada ya kuusachi zilikutwa zipo simu kumi na mbili za aina mbalimbali lakini zote ndani sabuni,

Nilipandwa na hasira sana kwanza zike pesa nilimnyang'anya kwa nguvu, na wakati polisi wanaendelea kushangaa nilimpiga kichwa kimoja matata sana akazimia na nikatoka na yule askari wa kike nilimpiga kibao matata sana wakanikamata na nilikaa selo siku tatu xmass niliisherehekea polisi.

Nailaani sana siku ile
 
Pole sana mkuu. Kila mtu ana jambo linalokereketa moyoni kuhusu maisha yake. Chukulia kama funzo flani la kukupa changamoto ya kukabiliana na magumu yote yatakayokuja mbele yako.
ahsante bibie Numbisa ushauri mujarabu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom