Kinumbo
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 3,189
- 5,822
Moja kwa moja kwenye dhumuni la mada husika, baadhi ama asilimia kubwa ya sisi watanzania tumekuwa waoga sana kwenye nyanja mbalimbali. Napenda kusemea kwenye nyanja ya hawa viongozi wetu, binafsi sio muumini wala mdau wa siasa ila kwa ninayo yaona na niliyo yaona yamenisukuma kuandika uzi huu.
Hawa watu wanaojiita viongozi katika serikali yetu wamekuwa waovu sana kwetu. Yaani kuna mambo wanafanya bila ya huruma ata chembe, bahati mbaya sisi walengwa tumetulia tu bila kuchukua hatua yoyote ile. Hawa jamaa wanatupeleka tu vile wanataka wao bila kujali ni zuri ama baya.
Jamaa kwakua wao tayari wana maisha mazuri basi wanajiamulia tu wanavyo taka. Mikataba wanayo ingia kila siku na nchi za huko wanako jua wao sio rafiki kwetu yaani full kutuburuza tu, jamaa hawana huruma kabisa. Kuna baadhi ya maeneo mpaka leo huduma za muhimu mpaka leo hakuna.
Kwa nchi kama Tanzania hatukupaswa kuwa hivi tuna kila kitu ila hawa viongozi wetu wao wanajua kujijali wao tu.
Niko kwenye hatua za kwenda kuwashtaki kwenye mahakama ya juu kabisa.