Sisi wanawake bwana!

Mama Mwana

JF-Expert Member
Jun 6, 2023
1,206
3,879
kunaye mtu mmoja alikua na mpenzi wake, mapenzi shatashata huku bibie akikataa wanaume waliokua wanakimbizana kuleta posa kwao kwa kisingizio ana mtu wake, kama uzuri amejaaliwa binti huyu, ni mzuri mashallah

Kaka wa watu kajitafuta kajipata, kajitutumua kwenda ukweni akapangiwa mahari tena ya bei na vitu ghali akatimiza yote mpaka tarehe ya ndoa ikapangwa, kisanga kikaja bibie kafumaniwa na mume wa nduguye tena kakiri si mara moja wala mbili shemeji anatelezesha utamu kwake.

Ujinga unaokuja ni mama wa mwanaume kushinikiza mwanae aoe hivyohivyo kisa watu wameshatoa michango na sare vitambaa wamekata hivi mama kweli unaweza kumshauri mwanao huu wazimu?
 
kunae mtu mmoja alikua na mpenzi wake, mapenzi shatashata huku bibie akikataa wanaume waliokua wanakimbizana kuleta posa kwao kwa kisingizio ana mtu wake, kama uzuri amejaaliwa binti huyu...
Hatari sana. Hili lilimkuta jamaa yangu, alimfunia mkewe mtarajiwa siku 2 kabla ya ndoa na bado akamuoa. Hadi leo wapo wote mwaka kama wa nane
 
Back
Top Bottom