Bwana Mfumo. Hayo uliyoyasema ndio kigezo cha kuwa na chuki kati yetu na upande wa pili? Kati ya serikali na wakristo. Hiyo mikataba ilianzia kwa nani? Ikiwa wakristo waliomba, serikali ikakubali. Lakini sisi tunapeleka madai yetu, lakini serikali inasuasua. Nani wa kumlaumu hapa kati ya wakristo na serikali? Ni nani wa kumjengea chuki kati ya wakristo na Serikali? Mi naona kama ni madai, hasira, chuki na tuzielekeze kwa serikali ili itimize haya tunayoyataka ili tulingane na wenzetu. Haki zetu tunamdai nani kati ya serikali na wakristo? Kama tunaidai serikani, hakuna sababu ya msingi kupoteza muda kwa kujaribu kutaka kujilinganisha na wakristo. Tupoteze muda katika kudai haki zetu kwa serikali bila kuharibu uhusiano uliopo kati ya dini hizi kuu hapa nchini. Tena serikali ya sasa rais ni mwislamu, makamu ni mwislamu, tunao wabunge na mawaziri waislamu wa kutosha. Tuwashinikize hawa kuwa madai yetu yana msingi. Wakishindwa, chuki na hasira zetu ziwe juu yao, badala ya kuleta malumbano na watu wa imani nyingine.