Sishauri mtu kusoma PhD OUT

Inaonekana kuna kutokuelewana kuhusu lengo la PhD. Kwa ujumla, mfumo wa usimamizi wa PhD unafanana katika taasisi nyingi duniani, tofauti zilizopo zikiwa ni za kiutendaji zaidi kuliko za kimsingi. Katika muktadha wa PhD, wahusika hawa wanapaswa kueleweka zaidi kama advisors kuliko supervisors, kwani jukumu lao kuu ni kutoa mwelekeo na ushauri, si kufundisha au kusimamia kwa mtindo wa darasani.

Ni muhimu kufahamu dhana hii kabla ya kuanza safari ya PhD. PhD inahitaji kiwango kikubwa cha kujitegemea kielimu, fikra huru, na uwajibikaji binafsi. Haimaanishiwi kwa mtu kulishwa maarifa kama ilivyo katika ngazi za undergraduate au masters.

Kukosa uelewa huu mara nyingi huchangia kuzalika kwa wahitimu wa PhD wasio na uwezo wa kutosha wa kufikiri kwa kina, kufanya utafiti huru, na kuchangia maarifa mapya, jambo ambalo limekuwa changamoto katika baadhi ya mifumo yetu ya elimu., unaishia kuwa na PhD urembo kama ya mama yako.
 
Huwa siamini hata bachelor za OUT. OUT ilianzishwa ili kutoa shahata feki kwa wanasiasa siyo kutoa elimu.
 
Pole sana. Wakufunzi na Supervisor(s) wetu wamejaa wivu, roho mbaya na wanawaza kimaskini hata watu wengine wapate PhD au Masters kama wao. Ndio maana nchi hii tunanyimwa ufadhili kwenye vyuo vyetu ila ukienda kwa majirani wana scholarship nyingi hadi unabaki unasikitikia Tanzania yetu
 
Unaenda chuo kinachofundishwa na watu wa diploma! Unategemea wanauwezo hata wa kuiangalia proposal ambayo hawajui hata kuiandaa na kuandika. Umechemka sana mzee.
 
HATA udsm ni Yale Yale niulize mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…