Katika makosa niliyofanya katika maisha ni kujiunga na masomo ya PhD pale Open University of Tanzania. Ningelijua ningeeda UDSM. Kwa matatizo ninayopitia sishauri mtu akasome PhD pale OUT.
Chamgamoto nilizopitia ni kama ifuatavyo:
1. Supervisor kutojibu email zangu au hata sms kwa zaidi ya mwaka mmoja.
2. Supervisor kukaa kimya bila kupitia proposal kwa zaidi ya mwaka mzima na Wala hajali. Unamtumia kazi zaidi ya mara kumi ila hajibu na yupo kimya kana kwamba hakujui.
3. Process ya kubadilisha supervisor ni ngumu Sana, unaweza kukaa mwaka mzima unahangaika tu. Nilijaza fomu ya kubadilisha supervisor wakaa kimya, nilipowakomalia wakanipa fomu nyingine, stori ikaishia hapo.
4. Yule mdada au secretary wa ofisi ya post graduate research wa OUT ana dharau Sana. Ukimpigia simu hapokei na hata akipokea akajua ni wewe ana kata simu yako. Yule dada ni shida Sana.
5. Kwa sisi tulioko mikoani ni shida kusoma PhD OUT. Hawajali kabisa. Na ukisema usafiri kwenda huko Dar utazungushwa mpaka uchoke. Nimeenda Dar kituoni kwao pale Biafra ni shida tu hakuna la maana la kunisaidia.
Kutokana na OUT kunisumbua kwa muda wa miaka mitatu huku ada yangu wamekula ila kunisaidia kwao wanaona mzigo au usumbufu kwakweli ni Bora niache kusoma hiyo PhD nifanye mambo mengine. Ila wamenipotezea muda, hiyo miaka mitatu imeenda Bure. Yani miaka mitatu unahangaika na proposal haijawahi kusahishwa hata kusomwa tu na supervisor. Ukienda ofisini kwao Biafra unaambiwa supervisor wako hayupo amesafiri.
7. Kwa kweli OUT mnakatisha tamaa, mtu anakuwa kama hasomi PhD. Kama uwezo wa kusimamia tafiti za wanafunzi wa PhD hapo si mnamwambia mwanafunzi atafute chuo kingine kuliko kupoteza muda wa mtu.