Sirudi tena Jukwaa la Siasa

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,037
Reaction score
168,684
Sina hamu....
Yaani visiku vihache tu jukwaani nikakutana na kiziba mdomo.
Ni ku like tu ndiko walikoniachia. Hamna kukoment wala kuanzisha thread.
Bora nijirudie zangu kwenye jukwaa la Mtambuzi niendelee kula minofu ya mbuzi kama kawaida.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nilipoingia hapa wenyeji wakaniambia Kule si kuzuri kumbe kweli? na mimi huwa nashinda hapa hapa.
 
Yaani bora mtu upigwe ban usiingie kabisa JF kuliko kuzuiwa ku comment. Inauma sana. Yaani ni sawa na ulale na mkeo kitanda kimoja wote mkiwa watupu halafu akunyime tunda. Pole sana Bujibuji
 
Last edited by a moderator:
kichwa kimewaka moto nini mkuu, welcome again
 
Sina hamu....
Yaani visiku vihache tu jukwaani nikakutana na kiziba mdomo.
Ni ku like tu ndiko walikoniachia. Hamna kukoment wala kuanzisha thread.
Bora nijirudie zangu kwenye jukwaa la Mtambuzi niendelee kula minofu ya mbuzi kama kawaida.

Jukwaa lile halitaki pupa
 
Mi kule naingia kwa machale stress tupu haukawii kukosanaa na kina Matola
 
Last edited by a moderator:
Mimi nilipoingia hapa wenyeji wakaniambia Kule si kuzuri kumbe kweli? na mimi huwa nashinda hapa hapa.

Kule ukitaka pawe pazuri isifie Chadema na uiponde Ccm na umtukane Zito mbona utapendekaaaa
 
Sina hamu....
Yaani visiku vihache tu jukwaani nikakutana na kiziba mdomo.
Ni ku like tu ndiko walikoniachia. Hamna kukoment wala kuanzisha thread.
Bora nijirudie zangu kwenye jukwaa la Mtambuzi niendelee kula minofu ya mbuzi kama kawaida.

welcome back!
 
Huko kwenye Jukwaa mama la Siasa ndiko kwenye ban za kufa mtu!! Watu wanarushiana makombora mwishowe unakula kifungo!!! Yaani kule ni hasira kufa na kupona. Sisi wapya tumeshakanywa kabisa uwe makini na kina Lizabon, Chama, Rejao, Ritz, Marcopolo, mwekundu, Chris Lukosi na wengine maana wanaweza kutibua hasira ukarudisha ikala kwako wakati wao wanapeta tu.
 
Mkuu mara ya kwanza kuingia jukwaa la siasa Ritz alinifanya nikaigwa ban la siku 30...Ila kuna watu wanakera kama akina lizabon,mingoi,simiyu yetu,Lukosi na wengine wengi dah yan kero tupu ila tunakomaa nao tu!
 
Pole sana mkuu, mimi ngoja nijiimarishe kidogo nisome upepo hata kule jukwa ala Siasa nitaenda tu.. Hata kwa sasa napita huko kiasi chake ila ninapenda niwe kule zaidi. Kila mtu anapenda kuchangia siasa za nchi yetu sema wengine wanakuwa vichwa maji hawataki ukweli hata uozo wanatetea tu.
 
Mkuu mara ya kwanza kuingia jukwaa la siasa Ritz alinifanya nikaigwa ban la siku 30...Ila kuna watu wanakera kama akina lizabon,mingoi,simiyu yetu,Lukosi na wengine wengi dah yan kero tupu ila tunakomaa nao tu!

Bila kumsahau mamaaa kubwaaa faizafox halafu wap hawana preshaaa ban unaipata mwenyeweee
 
Last edited by a moderator:
Bila kumsahau mamaaa kubwaaa faizafox halafu wap hawana preshaaa ban unaipata mwenyeweee

Mkuu alikuwepo msumbufu mmoja HAMY-D siku hizi simuoni tena kule..alikuwa anatuvuruga kweli..kila mara ni yeye na Dr. huyu naye alinisababishia ban la siku 7.....ila hapa mmu ukipigwa ban basi wewe kilaza mkubwa!
 
Last edited by a moderator:
pole mkuu, kule unaenda kwa step. alafu inabidi uwe na roho ngumu. unaweza predict majibu hata kabla haujaanza kusoma comments. mimi huwa napitia mada zotezote na kukoment panaponivutia,
kwa sasa PHOTO ndo ma best for stress releasing, biashara na ujasiliamali kwa kupata awareness ya issues, ila nimeanza kugundua MMU kunakautulivu na upendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…