Siri zingine mmh! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri zingine mmh!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jun 15, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Kuwa mkweli na muwazi ni moja ya misingi ya kujenga mahusiano yanayodumu na hata kukabiliana na dhoruba mbalimbali za maisha ya mahusiano ya ndoa.

  Swali kubwa ambao wengi hujiuliza, wanaume kwa wanawake hasa wale ambao wanaingia kwa mara ya kwanza katika mahusiano ya uchumba na hatimaye ndoa ni swali lifuatalo.

  Je, nikieleza ukweli wote wa maisha yangu ya nyuma haiwezi kuathiri mahusiano na kupelekea mwenzangu kufikia hatua ya kuachana nami?

  Inawezekana huko nyuma ulidhalilishwa (kubakwa nk) au uliwahi kutoa mimba nk. Je, kumueleza mpenzi wako jambo kama hilo haliwezi kupelekea yeye kukuacha hata kabla ya kuoana au unaweza kumueleza baada ya kuoana kwamba mwenzio nilibakwa au niliwahi kutoa mimba nk?
  Je, kuna umuhimu wa kutunza au kusema ukweli mapema kabla ya mahusiano kufika mbali?

  James alipooana na Jane, Jane hakumueleza kabisa terrible secret aliyokuwa nayo ingawa tangu siku ya kwanza walipogundua wanawaweza kuoana alikubaliana kwamba ni muhimu kila mmoja kueleza ukweli na kuwa wazi kusema ukweli na ukweli (trust/honest) kuwa ndiyo msingi wa mahusiano yao.

  James na Jane walifahamiana tangu walipokuwa shule ya msingi ingawa baadae kila mmoja alienda shule tofauti tofauti ya sekondari na chuo hadi walipokutana na kuamua kuoana.

  Baada ya kumaliza sekondari Jane alipoata mimba na akaamua kuitoa ili kwenda chuo na James hakuwa anajua hilo kwa kuwa aliyempa mimba alikuwa mwanaume mwingine.

  Baada ya kuoana waliishi kwa furaha, amani na upendo wa hali ya juu hata hivyo furaha hiyo ya ndoa ilikuwa inazimika kila pale Jane anapofikiria namna alitoa mimba (abortion) na hata alipokuwa anawaza namna ya kuanza familia alikuwa anajisikia hatia na kujiona hastahili kwani alishajihusisha na kosa la mauaji ya motto asiye na hatia tumboni mwake.
  Baada ya kukaa kwa muda mrefu na hiyo siri inayomuumiza ilifika siku akawaza na kuamini kwamba akimwambia James hiyo siri basi James atamsikiliza na kuendelea kumpenda kwani atakuwa amesema ukweli.

  Siku moja James na Jane walitembelea wazazi wa Jane huko Korogwe Tanga, wakiwa chumbani wawili tu, Jane akaamua kutoboa hiyo siri inayoutesa moyo wake kwa kumwambia James kwamba
  “KUNA KITU NILIKUWA SIJAWAHI KUKWAMBIA NACHO NI KWAMBA NILITOA MIMBA BAADA YA KUMALIZA SEKONDARI NA NILIFANYA HIVYO ILI NIWEZE KWENDA CHUO”

  James hakuamini kile Jane ameongea amesema, kwani alimfahamu Jane tangu watoto na wakasoma shule moja ya msingi na zaidi Jane alikuwa ni mwanamke ambaye huwezi kuamini kwamba aliweza kupata mimba na zaidi kupata wazo la kuitoa hasa kutokana na malezi ya familia yao na maisha yake kwa ujumla.
  Kilichomuumiza zaidi James ni kile kitendo cha Jane kwenda kutoboa siri yake siku ambayo wanakuwa kwa wazazi kwake, James alitafsiri kwamba Jane aliamua kutoa siri akiwa kwa wazazi wake ili hata kama baada ya kutoa hiyo siri James akaamua kuachana naye yeye Jane atakuwa huyo nyumbani kwa wazazi wake hivyo amepata sehemu ya kuishi baada ya kukurusha bomu lake.

  Hata hivyo baada ya Jane kuiweka wazi hiyo siri mahusiano na mume wake yalibadilika na yakaingia kwenye wakati mbaya kuliko nyakati zote na kilichomuumiza James ni kwa nini Jane alificha hiyo siri hadi baada ya kuaoan kwanza na si kabla ya kuoana.
  Kama Jane ameweza kutunza siri kubwa kama hiyo kwa huo muda je, anaweza kuaminiwa maeneo mengine ya maisha yake?

  Pia tukumbuke kwamba binadamu si Mungu kwamba unapokiri dhambi zako basi anakusamehe na kusahau.
  James hakusahau na alijiona ni mwanaume ambaye hafai duniani kwamba aliyemwambini duniani alificha siri kubwa.

  “Huwezi kurusha kombora zito kama hilo na ukategemea mambo yataenda kama kawaida kuna kulipa gharama (price)

  Sasa ndoa ilibadilika, kila ukitokea mgogoro au kutoelewa kokote sila ya James ilikuwa ni abortion ambayo Jane alifanya.

  Ilifika mahali Jane alijiona ilikuwa afadhari kubaki na siri yake moyoni kuliko kukaa nayo kwa muda mrefu halafu unakuja kuitoa kwani ilikuwa ni kama amemkabidhi James silaha (magic bullet) ambayo James aliendelea kuitimia maisha yao yote ya ndoa yao.

  Sasa kila alichokuwa anafanya Jane katika ndoa yao kilikuwa hakitoshi kwa kuwa ni msaliti, mficha siri na mnafiki……….

  Je, ungekuwa wewe ni Jane ukifanya nini na hiyo siri?
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  nisingethubutu kumweleza
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Siri ili iwe siri haina budi kubaki kuwa siri.
   
Loading...