Siri yafichuka wizi wa kompyuta polisi

Siri yafichuka wizi wa kompyuta polisi

Iyokopokomayoko

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2011
Posts
1,785
Reaction score
443
Siri yafichuka wizi wa kompyuta polisi

Mwanza. Siri za wizi uliotokea Makao Makuu ya Polisi mkoani Mwanza zimeanza kuvuja ambapo imebainika kuwa kompyuta aina ya laptop zilizoibwa ndani ya chumba cha vielelezo zilikuwa za ushahidi wa kesi ya wezi wa mashine za kuchukulia fedha(ATM).

Katika wizi huo wa benki ambao ulifanyika kwenye mashine za ATM mbalimbali na watuhumiwa watatu kunaswa Februari 10, mwaka huu saa 6 usiku wakiiba kwenye ATM za NMB,Tawi la PPF Plaza, Polisi walinasa vitu vingi vya watuhumiwa hao ikiwa ni pamoja na kompyuta mbili ambazo zinadaiwa kuibwa kituoni hapo juzi.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Polisi zimeeleza kwamba katika wizi huo uliotokea katika maghala ya Polisi, moja kati ya vifaa vilivyoibwa ni mafaili mbalimbali ya vielelezo kadhaa vya kesi zinazochunguzwa na polisi ikiwa ni pamoja na laptop hizo ambazo zilikuwa ni ushahidi kwa kesi hiyo ya wizi wa ATM.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ernest Mangu alipoulizwa kuhusiana na vielelezo vilivyoibwa Polisi, alikanusha kwamba laptop hizo zilikuwa kielelezo cha kesi za wizi wa fedha katika ATM lakini pia hakuwa tayari kueleza zilikuwa za kesi gani.

Wakati Kamanda huyo akikanusha baadhi ya askari ambao wanahusika na uchunguzi huo wamedai kuwa wizi huo uliendeshwa na maofisa wa polisi wasio waaminifu na kubainisha hakuna wizi unaoweza kufanywa na watu kutoka nje ya polisi.

Source: Habari Leo
 
Kazi yao siku hizi imebaki kujiibia wenyewe na kutumiwa na ccm kisiasa.
 
Polisi wamepewa mamlaka yote kuua, kupiga, kurusha mabomu, kuchoma watu na vitu vyenye ncha kali, kubambikiia kesi pamoja na ujambazi...
 
Sasa shida wakishajiibia wenyewe madai yao ni kuwa walioiba ni watu wasiojulikana ila tukiiba sisi tutajulikana tu.

Kazi yao siku hizi imebaki kujiibia wenyewe na kutumiwa na ccm kisiasa.
 
Kamanda wa polisi anakanusha kuhusu hizo laptop zilizoibiwa,lakini hataki kusema ni za kesi ipi?hapa napata picha mbili,
1.ni kweli zimeibiwa ila anajipa moyo kua watafanikiwa kuzipata ingawa sidhani kama hawa wezi ni wajinga kiasi hicho.
2.asipofanikiwa kuzipata,basi ndo mwanzo wa kuweka vidhibiti feki,maana ameshakanusha kuwa sio hizo,hawezi kuja kukubali badae,
Huu ndo utendaji wa jeshi letu
 
Hahahaha acha nicheke tu na kuendelea kuishi kwa nguvu za jua.
 
Polisi ni hatari kwa uhalifu kuliko hata majambazi
 
kuna mtu moja nakumbuka alikwisha leta uzi hapa mwanzoni mwa mwaka huu na kusema wezi wanaoiba kwenye ATM za NMB ni Seniors Staff wa NMB wakishilikiana na POLICE kwa hiyo hata sishangai kusikia hilo..
 
Daaah,,,kama waliingia kuiba kile kituo cha pale mjini,nawapa heshima zao,,,
pili sijui usalama wa taifa upo wapi,mule kuna ofisi za interpol,c.i.a,mkuu wa polisi,,si wajanja wa mjini wanaweza wakawawekea ile sumu ya radiation inayoua taratibu,,,
kweli the nation is at stake,,
 
Polccm wanaish maisha magumu sana jaribuni kuwachunguza hapo mlipo na wanatumika ili kujikwamua kimaisha
 
Back
Top Bottom