Siri yafichuka wizi wa kompyuta polisi

Siri yafichuka wizi wa kompyuta polisi

We ulitegemea akaibe nani kituoni kama sio polisi wenyewe, ina maana cku hiyo hakukuwa na polisi waliokuwa zamu! Tz hii
 
Siri yafichuka wizi wa kompyuta polisi

Mwanza. Siri za wizi uliotokea Makao Makuu ya Polisi mkoani Mwanza zimeanza kuvuja ambapo imebainika kuwa kompyuta aina ya laptop zilizoibwa ndani ya chumba cha vielelezo zilikuwa za ushahidi wa kesi ya wezi wa mashine za kuchukulia fedha(ATM).

Katika wizi huo wa benki ambao ulifanyika kwenye mashine za ATM mbalimbali na watuhumiwa watatu kunaswa Februari 10, mwaka huu saa 6 usiku wakiiba kwenye ATM za NMB,Tawi la PPF Plaza, Polisi walinasa vitu vingi vya watuhumiwa hao ikiwa ni pamoja na kompyuta mbili ambazo zinadaiwa kuibwa kituoni hapo juzi.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Polisi zimeeleza kwamba katika wizi huo uliotokea katika maghala ya Polisi, moja kati ya vifaa vilivyoibwa ni mafaili mbalimbali ya vielelezo kadhaa vya kesi zinazochunguzwa na polisi ikiwa ni pamoja na laptop hizo ambazo zilikuwa ni ushahidi kwa kesi hiyo ya wizi wa ATM.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ernest Mangu alipoulizwa kuhusiana na vielelezo vilivyoibwa Polisi, alikanusha kwamba laptop hizo zilikuwa kielelezo cha kesi za wizi wa fedha katika ATM lakini pia hakuwa tayari kueleza zilikuwa za kesi gani.

Wakati Kamanda huyo akikanusha baadhi ya askari ambao wanahusika na uchunguzi huo wamedai kuwa wizi huo uliendeshwa na maofisa wa polisi wasio waaminifu na kubainisha hakuna wizi unaoweza kufanywa na watu kutoka nje ya polisi.

Source: Habari Leo

Hii iko wazi kabisa!! Mwizi wa URAIANI pamoja na ununda wao siyo kitu rahisi kwenda kuiba KITUO CHA POLISI!!!! Huu wizi umefanywa na MIJIZI ya humo ndani ya jeshi la polisi tuu!!
 
Nimeisoma hii taarifa toka POLISI MKOANI MWANZA YAFAFANUA KWA KINA KUHUSU VIELELEZO VYA KESI VILIVYOIBIWA KITUONI HAPO - MPEKUZI nikagundua polisi hapako salaama tenaa na kuna milolongo ya kupotea kwa vielelezo vya kesi mbalimbali, mfano aliyekamatwa kameza madawa ya kulevya yakipelekwa kwa mkemia mkuu yanageuka na kuwa unga wa ngano, gongo inageuka kuwa maji. Pesa zilizoibwa benki zinapotea au zinakuwa noti za bandia na mengine mengi ya aina hiyo... Mfano hai soma hii habari

POLISI MKOANI MWANZA YAFAFANUA KWA KINA KUHUSU VIELELEZO VYA KESI VILIVYOIBIWA KITUONI HAPO



WATU wasiofahamika idadi yao wanaodhaniwa wezi, wameiba vielelezo katika stoo ndogo ya Kituo Kikuu cha Polisi Kati, Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza baada ya kuvunja madirisha.

Tukio la wizi huo lilifanyika Julai 15, mwaka huu, majira ya usiku wa kuamkia Jumatano katika jengo la Polisi Wilaya ya Nyamagana.

Akizungumza na gazeti la MAJIRA jana, Kamanda wa Polisi Mkoa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ernest Mangu, alisema wezi hao kabla ya kuingia ndani ya jengo hilo, walivunja dirisha la ofisi za Elimu, Ukaguzi Kanda ya Ziwa na walipofanikiwa kuingia ndani, walivunja dirisha na kuingia kwenye ofisi za Polisi Nyamagana na kutanua nondo kwa jeki na kisha kuingia kwenye stoo ndogo ambamo vielelezo hivyo vilitunzwa na kuiba begi moja la nguo na kompyuta mbili mpakato.

Moja ya kompyuta hizo ni kielelezo katika kesi ya ujambazi ambayo mtuhumiwa alikamatwa nayo, ambaye kwa sasa yuko mahabusu katika Gereza Kuu la Butimba.

Kamanda Mangu alisema kompyuta ya pili ni kielelezo cha kesi ya uharibifu wa mali inayomkabili fundi mmoja na begi la nguo ambazo mwenye nazo hafahamiki.



Begi hilo liliokotwa na polisi baada ya kuwakurupusha wezi hao waliokimbia na kulitelekeza.

Alieleza kuwa eneo walikopitia wezi hao usalama wake ni mdogo kwani ni uchochoroni na hakuna ulinzi wala mwanga wa taa, hivyo wanajaribu kuangalia kuboresha usalama wa hapo na maeneo jirani.





Mwisho wa kunukuu.

My take nadhani ni wakati sasa wa kila mtu kuchunga mali yake wakati kikosi chetu cha polisi kikinolewa ilivyo na jeshi la green guard chini ya General, Field Marshal M Nchembe..


attachment.php
 
Nadhani wawaajiri wamasai walinde vituo vyao, ili wapate muda zaidi wa kuwadhibiti wapinzani.
 
Back
Top Bottom