Siri yafichuka wizi wa kompyuta polisi

Siri yafichuka wizi wa kompyuta polisi

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
[h=1][/h]

Mwanza. Siri za wizi uliotokea Makao Makuu ya Polisi mkoani Mwanza zimeanza kuvuja ambapo imebainika kuwa kompyuta aina ya laptop zilizoibwa ndani ya chumba cha vielelezo zilikuwa za ushahidi wa kesi ya wezi wa mashine za kuchukulia fedha(ATM).

Katika wizi huo wa benki ambao ulifanyika kwenye mashine za ATM mbalimbali na watuhumiwa watatu kunaswa Februari 10, mwaka huu saa 6 usiku wakiiba kwenye ATM za NMB,Tawi la PPF Plaza, Polisi walinasa vitu vingi vya watuhumiwa hao ikiwa ni pamoja na kompyuta mbili ambazo zinadaiwa kuibwa kituoni hapo juzi.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Polisi zimeeleza kwamba katika wizi huo uliotokea katika maghala ya Polisi, moja kati ya vifaa vilivyoibwa ni mafaili mbalimbali ya vielelezo kadhaa vya kesi zinazochunguzwa na polisi ikiwa ni pamoja na laptop hizo ambazo zilikuwa ni ushahidi kwa kesi hiyo ya wizi wa ATM.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ernest Mangu alipoulizwa kuhusiana na vielelezo vilivyoibwa Polisi, alikanusha kwamba laptop hizo zilikuwa kielelezo cha kesi za wizi wa fedha katika ATM lakini pia hakuwa tayari kueleza zilikuwa za kesi gani.

Wakati Kamanda huyo akikanusha baadhi ya askari ambao wanahusika na uchunguzi huo wamedai kuwa wizi huo uliendeshwa na maofisa wa polisi wasio waaminifu na kubainisha hakuna wizi unaoweza kufanywa na watu kutoka nje ya polisi.
 
Kama kumbukumbu yangu iko sahihi miaka kadhaa nyuma uliwahi kutokea wizi hapo hapo Makao Makuu ya Polisi Mwanza...
 
Polisi wa Tanzania ndiyo Mjambazi wenyewe wanaotuibia na kutunyonga kila mahali hapa Tanzania.

Katika Ulimwengu huo wa usiku ambao POLISI hugeuka Majambazi hatari na yasiyo na huruma,

Vyeo vya KiPOLISI huzangatiwa na kuheshimiwa.

Kwa hiyo POLISI wa chini ukibambwa huwezi kamwe taja kwamba hata Saidi Mwema yumo kwenye Mtandao unakufa Ki REVORA

Kwa mfano Said Mwema ni IGP wa POLISI, lakini vile vile ni Bosi wa Mtandao wote wa Mharamia Tanzania,

Huyu ndo Ibilisi wao mtakatifu kwenye hiyo dunia ya usiku wa nyuki.

Ndiyo maana WaTanzania wanalipuliwa na Bomu la kurushwa kwa mkono POLISI wanasaidia kumtorosha mrusha Bomu.

Wamejiibia wenyewe kwa sababu hata hao wezi wa ATM ni dugui moja katika wizi MTAKATIFU.
 
Kama kumbukumbu yangu iko sahihi miaka kadhaa nyuma uliwahi kutokea wizi hapo hapo Makao Makuu ya Polisi Mwanza...

Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya askari kama uwizi hauwezi kutoka nje polisi wenyewe basi wezi ni hao hao polisi. Aibu kwa Jeshi la Polisi.
 
Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya askari kama uwizi hauwezi kutoka nje polisi wenyewe basi wezi ni hao hao polisi. Aibu kwa Jeshi la Polisi.

kwa taarifa yako: HAWAOGOPI WALA HAWAONI AIBU.
 
Kuna kila sababu wenyewe ndo wanahusika na hii ni ishara jinsi gani jeshi la polisi hali ilivyo kwa hivi sasa(yaani wenyewe ndo wakuu wa mafia no 1)

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ndani ya uzuri hapakosi ubaya na ndani ya ubaya hapakosi uzuri isiokuwa kwa Mungu pekee.
 
Kama kumbukumbu yangu iko sahihi miaka kadhaa nyuma uliwahi kutokea wizi hapo hapo Makao Makuu ya Polisi Mwanza...

Mwanakijiji, kumbukumbu hii sidhani maana matukio ya Mwanza mengi ni kutoroka watuhumiwa kwenye Lock Up za polisi na Mahakamani.

Ila Dar kituo cha Msimbazi waliwahi kuiba Mishahara ya Polisi ofisi ya Uhasibu.
 
Tanzania haina jeshi la polisi bali kuna mkudangiko wa wahuni na majizi yaliyokubuhu
 
Polisi walitoroka na fedha kariakoo baada ya kuzisalimisha kwa majambazi(kova aliunda tume),Polisi wakutwa na magunia 12 ya bange ndani ya Deffender Moshi,Polisi wachakachua madawa na kupeleka unga wa mahindi kama kizibiti(mkemia mkuu athibitisha),polisi wanahusika mtandao mkali wa upitishaji wa magari pwani ya dar es salaam(kova aliunda tume),Polisi akutwa na fuvu la mtu akitumia kuwabambikiza watu kesi(morogoro),Polisi wahusika ulipuaji wa mabomu Arusha soweto(mtoto alithibitisha kupigwa risasi na polisi),Polisi ndio waliomuua Mwangosi Daudi Iringa picha ipo mitandaoni,Polisi wahusika na wizi wa laptop kituoni mwanza tarehe 19july,Polisi akamatwa akitorosha mafuta na ma container Bandari Dar es salaam,Polisi wavunja nyumba za watu kupora mali(JWTZ waliwanasa wahusika) na kuwabaka Mtwara(maiti ya mama mjamzito akutwa na tundu la Risasi),Polisi ahusika kumwagia tindikali mgoni wake na kumwambia atokomee(kisa kiko channel 10-ni jamaa wa kigamboni,silikumbuki jina ila ni kipofu tangia amwagiwe),Polis wakike kituo magomeni apiga picha za uchi(jina na picha ninavyo navihifadhi kwa sababu ya maadili-jamilla ....),Traffic wanakula rushwa barabarani tena waziwazi (waulize makonda wanawajua tena kwa majina) nk nk hembu niambie katikai baadhi tu ya matukio niliyoyataja Watawala hawajastuka kama jeshi la polisi ni kandamizi,wauaji,majambazi,matappeli,mafuska nk nk kiasi kwamba wamekosa credibility mbele ya jamii?
Je kuna sababu ya kulifumua na kuangalia tena misingi ya jeshi la polisi?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Sometime sijui niseme nini maana niko speechless, afu cheki watakuja watu humu kuwatetea hao polisi ni kama vile utani lakini haichekeshi. Sipendi vurugu lakini mtu atavumilia mpaka lini? Majadiliano hayasaidii, tume hazisaidii dawa iliyobaki ni kuchapana bcoz haya hayana mwisho kwa mwenendo huu.
 
Polisi walitoroka na fedha kariakoo baada ya kuzisalimisha kwa majambazi(kova aliunda tume),Polisi wakutwa na magunia 12 ya bange ndani ya Deffender Moshi,Polisi wachakachua madawa na kupeleka unga wa mahindi kama kizibiti(mkemia mkuu athibitisha),polisi wanahusika mtandao mkali wa upitishaji wa magari pwani ya dar es salaam(kova aliunda tume),Polisi akutwa na fuvu la mtu akitumia kuwabambikiza watu kesi(morogoro),Polisi wahusika ulipuaji wa mabomu Arusha soweto(mtoto alithibitisha kupigwa risasi na polisi),Polisi ndio waliomuua Mwangosi Daudi Iringa picha ipo mitandaoni,Polisi wahusika na wizi wa laptop kituoni mwanza tarehe 19july,Polisi akamatwa akitorosha mafuta na ma container Bandari Dar es salaam,Polisi wavunja nyumba za watu kupora mali(JWTZ waliwanasa wahusika) na kuwabaka Mtwara(maiti ya mama mjamzito akutwa na tundu la Risasi),polisi wamtorosha mtuhumiwa, Polisi ahusika kumwagia tindikali mgoni wake na kumwambia atokomee(kisa kiko channel 10-ni jamaa wa kigamboni,silikumbuki jina ila ni kipofu tangia amwagiwe),Polis wakike kituo magomeni apiga picha za uchi(jina na picha ninavyo navihifadhi kwa sababu ya maadili-jamilla ....),Traffic wanakula rushwa barabarani tena waziwazi (waulize makonda wanawajua tena kwa majina) nk nk hembu niambie katikai baadhi tu ya matukio niliyoyataja Watawala hawajastuka kama jeshi la polisi ni kandamizi,wauaji,majambazi,matappeli,mafuska nk nk kiasi kwamba wamekosa credibility mbele ya jamii?
Je kuna sababu ya kulifumua na kuangalia tena misingi ya jeshi la polisi?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums



Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom