Siri yafichuka ! MOU kati ya CUF na CCM - Chadema kaeni chonjo ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri yafichuka ! MOU kati ya CUF na CCM - Chadema kaeni chonjo !

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mag3, Oct 24, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 8,175
  Likes Received: 3,736
  Trophy Points: 280
  Siri za CCM, CUF zavuja

  MAKUBALIANO kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) kuhusiana na mwendo kuelekea uchaguzi mkuu yamevuja, MwanaHALISI linaweza kuripoti. Taarifa zilizofikia gazeti hili zinasema kumekuwa na maelewano juu ya tabia na mwenendo wa viongozi wa vyama hivyo viwili ili kuzuia kuumbuana hadharani.
  Lakini gazeti limeelezwa kuwa kinachoitwa makubaliano hakikuandaliwa na ngazi ya juu ya uongozi, kiasi kwamba mgombea urais wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba anadaiwa “kuharibu dili.”
  Wakati imeelezwa kuwa CCM na CUF walikubaliana kutoshambuliana hadharani, na hasa kutoshambulia wagombea urais binafsi, Prof. Lipumba tayari amemkwaruza Jakaya Mrisho Kikwete.
  Kwenye mkutano wa kampeni wilayani Mbalizi, mkoa wa Mbeya, tarehe 19 mwezi uliopita, Profesa Lipumba alinukuliwa akisema, Kikwete hafai kuwa kiongozi kwa kuwa ameshindwa kuendesha nchi.
  Taarifa hizo zilizochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima chini ya Kichwa “Lipumba, Slaa wamshambulia Kikwete,” zilimkariri Lipumba akisema, “…matumizi makubwa ya familia yake (Kikwete), yamesababisha ashindwe kuendesha nchi.”
  “Tangu ameingia madarakani, amekuwa na matumizi mabaya, hasa ya familia yake kufanya ziara ambazo si za lazima, akiwamo mke wake Mama Salma na mwanawe Ridhiwani wanaozunguka nchi mzima kumpigia kampeni,” ananukuliwa Lipumba akisema.
  Aliwataka wananchi kutomchagua tena katika nafasi hiyo.
  Kuvuja kwa siri hii kumetokana na mawasiliano kati ya Msaidizi wa Rais, January Makamba na Mkurugenzi wa mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa Ladhu.
  Katika mawasiliano yao kati ya Januari na Oktoba mwaka huu, Makamba analalamikia CUF kuvunja makubaliano kutokana na Lipumba kumshambulia Kikwete.
  Makamba anamwandikia imeili Jussa kwa kusema, “Utakumbuka yale makubaliano yetu; imekuwaje muafaka wa kutoenda personal?” (kushambulia mtu binafsi). Imeili hiyo iliandikwa saa nane na nusu usiku wa 22 Septemba 2010.
  Akiandika kwa msisitizo, Makamba ananukuu taarifa ya gazeti na kumpelekea Jussa.
  Naye Jussa akijibu Makamba aliandika, “January, maelewano yetu yako palepale. Kosa lilikuwa langu kumsubiri (Lipumba) hadi tuonane uso kwa uso ili nimpe briefing – taarifa. Bahati leo amekuja Zanzibar na tumeelewana. Nitakupigia tuzungumze zaidi. Jussa”
  Maelezo haya ya Jussa ni ya tarehe 22 Septemba 2010 saa 11:05 alfajiri. Gazeti hili limethibitisha kuwa Profesa Lipumba alikuwa Zanzibar siku inayotajwa na Jussa.
  MwanaHALISI lilipomuuliza Jussa kwa simu, juu ya mawasiliano hayo ambayo yanaweza kutibua chama chake, haraka aling’aka na kusema, “Naomba nikuulize, wewe imeili yangu umeipataje?”
  Akiongea kwa sauti ya kufoka, Jussa aliuliza, “Umewezaje kufungua imeili yangu? Hiyo haiwezi kuwa imeili yangu. Umepata wapi kifungulio?”
  Alipoambiwa kwamba gazeti lina uhakika kuwa mawasiliano liliyonayo ni yake, Jussa alisema, “Najua nyie waandishi wa Tanzania mmezoea kutunga taarifa. Huo ni utungaji na hauwezi kuisaidia nchi hii.”
  Kwa upande wake, Makamba alikiri kumuandikia Jussa ujumbe huo, lakini akasema aliandika “kama rafiki tu.”
  “Kama ujuavyo, mimi sina wadhifa wowote ndani ya CCM. Kwa hiyo, kwa namna yoyote ile, siwezi kuwa msemaji wa chama katika mambo kama hayo.
  “Kilichopo ni kuwa Jussa ni rafiki yangu. Kwenye mazungumzo yetu mara nyingi nimekuwa nikimwambia kuhusu umuhimu wa kuzingatia siasa zenye kuleta maendeleo na si zile za mambo binafsi,” anaeleza.
  Lakini kauli ya Makamba inaonyesha ama amesahau, anaficha ukweli au anasema uwongo, kwani mawasiliano ya awali tayari yanaonyesha Jussa akikiri kuchelewa “kumwambia” Lipumba juu ya mpango wao huo.
  Ni Jussa anayesema, “Kosa lilikuwa langu kumsubiri (Lipumba) hadi tuonane uso kwa uso ili nimpe briefing…”
  Bali Makamba anaendelea kudai kuwa, “Yale ni mawasiliano kati ya marafiki na si vinginevyo.”
  Prof. Lipumba hakuweza kupatikana kutolea maelezo sakata hilo. Alipoitwa kwa simu, alijibu mara moja kuwa yuko njiani akienda Sumve, mkoani Mwanza. Simu ilikatika na hakuweza kupatikana tena.
  Naye Hamad Rashid Mohammed, mwanzilishi wa CUF na kiongozi mwandamizi, amesema hajui lolote kuhusu kile kinachoitwa makubaliano kati ya chama chake na CCM.
  “Kama Lipumba alizungumza kuhusu matumizi ya familia ya rais, hilo haliwezi kuwa jambo la kibinafsi. Hilo linahusu matumizi ya fedha za walipa kodi na hata kama hayo makubaliano yangekuwapo, kwenye hili yasingeingia,” amesema Hamad Rashid.
  Alimwambia mwandiki kuwa kama “…umeona barua ya mwenzetu (Jussa) ikizungumzia mambo hayo, naomba umuulize yeye, maana ndiye mhusika.”
  Kumekuwa na uvumi kuwa makubaliano kati ya vyama hivi viwili yametokana na msaada wa fedha ambazo Rostam Aziz, mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM aliipa CUF kuendeshea shughuli zake.
  Hata hivyo, Hamad alipoulizwa juu ya hilo alisema fedha zote wanazotumia ni kutoka kwenye mfuko wao wa ruzuku na michango ya wanachama.
  Amesema, “Mara ya mwisho nilionana na Rostam wakati tukiwa wabunge bado na sijaonana naye tangu bunge lilipovunjwa.”
  Taarifa za kuaminika zinasema Rostam Makamba na Jussa ni “pete na kidole.”
  Aidha, kupatikana kwa taarifa juu ya “mpango wa kutoshambuliana” kati ya CCN na CUF, kumeelezwa na wachunguzi wa mambo kuwa usaliti uliofanywa na mmoja wao kwa makusudi.
  Chanzo kingine cha habari hii kinasema, siyo tu taarifa juu ya makubaliano ambazo “ziko njenje,” bali kila taarifa inayotolewa na CUF inatinga ofisini na nyumbani kwa baadhi ya viongozi wa CCM.
  Kwa mfano, barua ya Naibu Katibu Mkuu CUF (Bara), Joran Bashange ya tarehe 15 Oktoba, Ijumaa iliyopita, inadaiwa kukutwa pamoja na nyaraka zinazoonyesha mawasiliano ya Makamba na Jussa.
  Katika barua hiyo, Kumb. Na. CUF/AK/DSM/NKM/B/002/A2/2010/83
  Bashange anaandika, “Chama chetu kina matarajio ya kuibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu huu.”

  Bashange amelaumu “…taasisi mbalimbali za kitafiti ambazo hutoa matokeo (kura za maoni) yaliyopikwa kwa minajili ya kuwakatisha tamaa wananchi.”
  Jingine ambalo analalamikia katika barua ambayo tayari imevuja hadi ikulu, ni “mkakati wa kuzuia wagombea wa CUF kufanya kampeni kikamilifu kwa kuingilia ratiba zao za kampeni.”
  Alipoulizwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa kwamba naye ana mpango kama vyama hivi viwili alisema, “Hatuna mpago huo. Hatufikirii kuwa nao.”


  - Saidi Kubenea - Mwananchi


  Kumbe ! Habari ndiyo hiyo !
   
 2. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mag3, ahsante kwa taarifa hayo ndo madhara ya muafaka wa CUF na CCM zanzibar. Inabidi CUF wawe makini vinginevyo watamezwa kama dagaa.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 69,367
  Likes Received: 3,018
  Trophy Points: 280
  Wapigakura tunakwenda kufuta kazi CCM na kwa hiyo hizo MOU zao watajijua kati ya CUF na CCM labda watapanga namna ya CUF kumfunza CCM siasa za upinzani............
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,125
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Ni siku nyingi sana watu wamekuwa wakiita CUF ni CCM B, pasipo ushahidi. Imekuwa heri leo kwamba tumeujua ukweli kwamba CHADEMA inapambana na vyama viwili vyenye mlengo mmoja. Kuna haja ya kuyauliza haya siku ya mdahalo wa Lipumba tuone atakavyojiuma uma.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Du! siasa za bongo bana!!!!!!!!!
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,150
  Likes Received: 1,859
  Trophy Points: 280
  Lipumba na Maalim Seif... matendo yenu hayana tofauti na ya shetani anayewadanga watu na kuwaangamiza. Maskini wee... Mwaka 2000 mliwadanganya Wapemba walalahoi waandamane... wakauawa kwa risasi za polisi, na leo hii nyinyi mmeungana na wale wale walioua ndugu zenu mnakula kuku kwa mrija!! Ole wenu ole wenu ole wenu .. damu yao itawatafuta kulipiza kisasi!! Laana ya milele mtaipata! Ole wenu ole wenu "mnakunywa" damu za wenzenu! Hukumu ile kali inawangoja! Mungu hadanganyiki! Laana hamtaiepuka! Ole wenu!
   
 7. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,150
  Likes Received: 1,859
  Trophy Points: 280
  Na... CUF mwaka huu watalizwa tena. Lakini kwa sababu maalim ataukwaa uongozi atawanyamazisha
   
 8. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli ukifikiria damu ilyomwagika Zanzibar halafu ukaangalia viongozi wanavyonufaika na damu hizo utajuta kuwafahamu wanasiHASA
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,271
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Let us make history
  let us change the regime.
   
 10. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Mrengo upi huo mkuu? UDINI?
   
 11. u

  urasa JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  god is with us,so nobody who will be against us,hata lipumba anajua kuwa mwaka huu hana chake ndio maana akajisahau na kuvunja makubaliano yao,slaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!
   
 12. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,756
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Huyu Ismail Jussa Ladhu si ndo yule aliyekirimiwa Ubunge na JK mwishoni kabisa mwa bunge hapa au?
   
Loading...