payuka
JF-Expert Member
- Jun 17, 2010
- 829
- 126
Wana JF nimeamua nivunje ukimya wa kuzungumzia sakata la mvutano baina ya CUF na Chadema.
Katika kutafakari mambo ikiwa ni pamoja kuangalia ni wapi vyama hivi viwili vilikotika, vilipo sasa na wapi vinataka kuelekea nikagundua mambo yafuatayo.
Fukuto linaloendelea la kuunda kambi ya Upinzani yenye kushirikisha vyama vyote:
Ni sahihi kabisa kwa CUF kutokubaliana na CHADEMA kujiunga kwenye Kambi ambayo viongozi wake wa juu wote wanatoka chama kimoja; yaani Freeman Mbowe, Zitto Kabwe na Tundu Lisu Wote Chadema. Kama kafu wangefanya makosa hayo kwa kujiunga na kambi hiyo na kukubaliana na structure ya uongozi wa juu wangekuwa wamesaidia kuipa CHADEMA points zingine za kuwa ni chama pekee ndani ya bunge chenye upinzania mkali dhidi ya CCM.
CUF pamoja na vyama vingine wangekuwa wamejimaliza wao wenyewe kwa upande wa Tanzania Bara, kitu ambacho viongozi wa CUF wameshakiona.
Kwa upande mwingine uamuzi wa CHADEMA wa kuchukua nafasi zote tatu za juu katika kambi ya upinzani uliona mbali. Nasema uliona mbali kwa sababu kama ni makosa yasio sahaulika ambayo CHADEMA ingeyafanya mwaka huu ni kuruhusu ushirikiano kwenye nafasi hizo tatu, na kosa lingekuwa tete zaidi endapo CUF ingepewa nafasi ya kuweka mtu wao na hasa kwenye nafasi ya uenyekiti. Nasema hivi kutokana na kilichotokea Zanzibar ambako CUF ina nguvu na UHAI zaidi, kwa kitendo cha CUF kuunda serikali ya shirikisho ni dhahiri watendaji wake watasaidia kwa asilimia kubwa kutekeleza ilani pamoja na matakwa ya CCM. Kitu ambacho ni kinyume na itikadi za CHADEMA ambayo inataka mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji na uwajibikaji wa serikali.
Hiyo ndo siri wana JF, kama inaingia akilini mwako asante nashukuru. Na labda nimalizie kwa kusema CHADEMA inaendelea kuongeza idadi ya wapinzani ndani na nje ya Bunge.