Siri ya maisha na kifo na melanie chuma

Siri ya maisha na kifo na melanie chuma

Joined
Nov 25, 2022
Posts
2
Reaction score
2
SIRI YA MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
( SIMULIZI YA KIJASUSI

EP 01
ARUSHA
Kikao cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika katika makao makuu ya Jumuiya hiyo yaliyopo Arusha Tanzania kilimalizika kwa mafanikio makubwa. Kikao hicho cha kawaida kilichohudhuliwa na marais kutoka nchi zote sita zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, kilipokea na kujadili taarifa mbalimbali zinazohusu jumuia
hiyo ikiwamo taarifa kuhusiana na mchakato wa uanzishwaji wa sarafu moja ya Afrika Mashariki ulikofikia.

Kikao hicho pia kilijadili ombi la nchi ya jamhuri ya kidemokrasi ya Congo kujiunga na Jumuiya hiyo na kuikubali kuwa mwanachama wa saba wa Jumuiya hiyo.

Jambo lingine lililofanyika katika kikao hicho ni nchi ya Tanzania kuchukua nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya kikao kumalizika na wakuu wa nchi kuzungumza na wana habari
kuhusu yale yaliyojiri katika kikao hicho, wakuu wote wa nchi walielekea katika hoteli ya Kobe Village kwa ajili ya kupata chakula cha mchana na baada ya chakula baadhi ya wakuu wa nchi waliondoka na walibaki wachache waliokuwa na mazungumzo binafsi na Rais wa Tanzania na baada ya kumaliza mazungumzo yao marais wa Kenya na Burundi wakaondoka akabaki Rais Patrice Eyenga wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambaye alikuwa na mazungumzo binafsi na mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki rais wa Tanzania Dr Fabian Kelelo. Dr Fabian alimkaribisha Rais Patrice katika chumba chake kwenye hoteli kubwa Jijini Arusha Kobe village kwa ajili ya mazungumzo maalum.

Walinzi wote wa marais hawa wawili wakabaki nje na kuwapa nafasi wakuu wao wazungumze faragha.
JE WANA MAZUNGUMZO GANI? USIKOSE MWENDELEZO.
 
SIRI YA MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA 02



“Karibu sana ndugu Patrice” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais Dr Fabian kwanza ninakushukuru sana kwa namna ulivyojitahidi katika kikao kuwashawishi marais wakubali ombi la nchi yangu kujiunga na Jumuiya hii.Ni muda mrefu tumekuwa tukiitafuta nafasi ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini migogoro na mapigano yasiyokwisha nchini kwetu ndivyo vimetuchelewesha. Ninashukuru sana kwa kutukubali na sisi tuingie katik aJumuiya hii. Ni furaha kubwa kwa wananchi wa Congo kujiunga na wenzao” akasema Rais Patrice Eyenga “Mheshimiwa Patrice nina kupongeza sana kwa maamuzi haya makubwa ya kuiunganisha nchi yako na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ninaamini nchi yako itanufaika sana na fursa zilizomo katika Jumuiya hii. Kuna maombi mengi ya nchi zinazotaka kujiunga na Jumuiya hii lakini tumeyachambua na baaadhi ya nchi zimekataliwa nyingine tunaendelea kuzijadili lakini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo tumewakubali kwa kuwa ninyi ni ndugu zetu tunafanya biashara pamoja na kushirikiana katika mambo mbali mbali ya kiuchumi hivyo mnastahili kabisa kujiunga na

Jumuiya ya Afrika Mashariki” ak



asema Dr Fabian “Kwa niaba ya wananchi wa Congo ninashukuru sana” akasema Patrice na ukimya ukapita mle ndani “Karibu sana tuijenge Afrika Mashariki” akasema Dr Fabian na ukimya mfupi ukapita kisha Patrice akasema “Dr Fabian tukiachana na hilo la kukubaliwa uanachama kuna jambo lingine kubwa ambalo nataka kuzungumza nawe ili kwa pamoja tuone namna ya kulitatua” akasema Rais Patrice “Karibu” akasema Dr Fabian



“Mheshimiwa Rais, Tanzania na Congo tumekuwa marafiki na ndugu kwa miaka mingi. Tanzania imekuwa ni nyumbani kwa watu wa Congo. Kila pale kulipokosekana amani nchini kwetu wengi wa watu wa Congo walikimbilia huku. Watu wetu wameishi hapa kwa amani miaka nenda rudi na kwa sasa baada ya machafuko vita na mauaji kumalizika, raia wote wa Congo waliokuwa wakiishi katika nchi mbalimbali kama wakimbizi wameanza kurejea nyumbani na kwa pamoja tunaijenga Congo mpya. Uchumi wetu umeanza kukua, viwanda vingi vinajengwa, miundo mbinu inaboreshwa na kwa nafasi hii tuliyoipata ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki nina imani tutapiga hatua kubwa sana na ndani ya miaka michache ijayo nchi ya Congo uchumi wake utapaa kwa kasi ya kushangaza kwani ni nchi tajiri imejaa rasilimali.
 
Back
Top Bottom