Siri ya kutimuliwa mawaziri yafichuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri ya kutimuliwa mawaziri yafichuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Apr 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kura kumkataa Pinda kumbe ilimlenga Rais Kikwete
  [​IMG] Filikunjombe: Angezungumza Zitto isingekuwa na nguvu
  [​IMG] Makinda awashukia mawaziri wanaojisafisha nje ya Bunge  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete


  Imebainika kuwa mkakati wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ulimlenga Rais Jakaya Kikwete.
  Mkakati huo uliandaliwa ukiwa ni sehemu ya kushinikiza kutimuliwa kutoka kwenye nyadhifa zao, mawaziri waliotajwa kuhusika kwa namna tofauti katika wizi na ubadhirifu wa mali za umma.
  Hata hivyo mkakati huo unadaiwa ‘kuvujishwa’ kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, hivyo kuibua hoja ya kupiga kura hiyo, ikimuelekea Waziri Mkuu, Pinda.
  Hayo yamebainika huku Kamati Kuu (CC) ya CCM ikiridhia mpango wa Rais Kikwete kuwashughulikia mawaziri wanaotajwa katika kashfa hizo na kulisuka upya Baraza la Mawaziri.
  Mawaziri wanaotakiwa kujiuzulu kutokana na kashfa tofauti ni Mustafa Mkulo (Fedha na Uchumi) Cyril Chami (Viwanda na Biashara) William Ngeleja (Nishati na Madini) na Omar Nundu (Uchukuzi).
  Wengine ni Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), George Mkuchika (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Profesa Jumanne Maghembe (Kilimo Chakula na Ushirika) na Dk. Haji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii).
  Hata hivyo, kwenye orodha hiyo anatajwa pia Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu.
  Habari za uhakika kutoka ndani ya wabunge wa CCM walioasisi mkakati huo, kisha ukakubalika kwa idadi kubwa miongoni mwao, zilieleza kuwa kura ya kutokuwa na imani ilipangwa kupigwa dhidi ya Rais Kikwete.
  Hali hiyo ilifikiwa kama sehemu ya kumshinikiza awawajibishe mawaziri wanaotuhumiwa kwa wizi na ubadhirifu wa mali za umma.
  “Lengo la awali lilikuwa kutumia kanuni za Bunge zinazohalalisha kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Kikwete, lakini tukaliona hilo ni jambo kubwa sana hivyo tukaamua kumheshimu Rais wetu,” kilieleza chanzo chetu kutoka miongoni mwa wabunge wa CCM.
  Kwa mujibu wa chanzo hicho, wabunge wa CCM walielezea kumheshimu Rais Kikwete hivyo kuondokana na azma ya kumpigia kura hiyo, ndipo ikatafutwa mbinu mbadala ya kushinikiza kuondolewa kwa mawaziri hao.
  “Hivyo mkakati wa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haina maana kwamba Pinda ana makosa, bali ni mchakato utakaofanikisha kujiuzulu kwa mawaziri husika,” kilieleza chanzo chetu.

  SPIKA MAKINDA AWASHUKIA MAWAZIRI
  Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema kitendo cha baadhi ya mawaziri waliotakiwa kuwajibika kutokana na ubadhirifu wa fedha za umma, kujitetea nje ya chombo hicho cha uwakilishi wa wananchi, hakina mantiki bali kukidhi utashi binafsi.

  Akizungumza kwa njia ya simu na NIPASHE Jumapili juzi, Makinda alisema kauli za kukanusha taarifa zilizowasilishwa bungeni ama kutoa vielelezo kwa lengo la kujiweka kando ya tuhuma zilizotolewa hakuathiri mambo yaliyoamuliwa ndani ya Bunge.
  Ingawa Makinda hakutaja majina ya mawaziri wahusika, lakini mmoja wao ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, ambaye alikaririwa akipinga

  tuhuma zilizotolewa bungeni dhidi yake.
  Maige ameonekana na kusikika kwenye vyombo kadhaa vya habari, akikanusha tuhuma dhidi yake na kusema huenda kuna mkakati wenye lengo la kisiasa, vinginevyo yeye ni mtu safi.

  “Hayo yanayoendelea nje ya Bunge hayawezi kushawishi mambo yaliyoamuliwa bungeni, yale yanayosemwa huko hayawezi kubadilisha msimamo tuliofikia,” alisema.
  Makinda alisema ripoti zote zilizowasilishwa bungeni, kujadiliwa na kutolewa maagizo haziwezi kubadilika ama kuathiriwa na matukio yanayotokea nje ya Bunge.

  Alisema kitendo cha Waziri kutoa ufafanuzi ama kuzungumzia mambo yanayomhusu, ni moja ya haki zake kwa vile hakuna mamlaka yenye kumziba mdomo.
  “Bunge haliwezi kumziba mtu mdomo kwa sababu kila mtu ana uhuru wake wa kuzungumza, kwa hiyo waendelee tu kuzungumza lakini msimamo wa Bunge upo pale pale,” alisema.

  FILIKUNJOMBE ANENA

  Mbunge wa Ludewa (CCM) aliyekuwa mmoja wa walioshinikiza kuondoka madarakani kwa mawaziri wanaotuhumiwa, alisema hatua hiyo itaiweka CCM kukubalika katika jamii na kuwa na uhakika zaidi wa kudumu madarakani.
  Akizungumza katika mahojiano maalum ya NIPASHE Jumapili jijini Dar es Salaam juzi, Filikunjombe alisema tuhuma zinazowakabili mawaziri husika ni moja ya maeneo yanayoiathiri jamii pana ya Tanzania hivyo hakuna sababu ya kuweka mbele maslahi ya kisiasa.

  Alisema kama hoja ya kuwataka mawaziri kujiuzulu ingesimamiwa kidete na wabunge wa upinzani, isingekuwa na nguvu kama ilivyotokea kwa upande wa CCM.
  “Hoja hii ingesimamiwa na akina Zitto Kabwe isingekuwa na nguvu kwa maana watu wangesema ni kawaida ya upinzani, lakini wabunge wa CCM tuliposimama na kuzungumza, imeleta matokeo makubwa,” alisema.

  Filikunjombe alisema hali ya ustawi wa jamii imedumaa huku baadhi ya viongozi wa serikali wakiwemo mawaziri wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wakijilimbizia mali kinyume cha sheria.

  “Tunapokuwa majimboni kama kule kwangu Ludewa, wananchi wanahoji kuhusu ukosefu wa huduma bora za afya, elimu, miundombinu na maji safi na salama,” alisema.
  Aliongeza,“ kwa hali ilivyo sasa na hulka hii ya mawaziri wasiokuwa waaminifu kuhujumu rasilimali za nchi, si rahisi kuyafikia maisha bora kwa kila Mtanzania.”

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  sasa mbona walitaka kutumia njia ndefu sana kumwajibisha rais?
   
 3. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Kumuondoa Kikwete ndio ultimate solution from present kamikaze. Hata kama haikufanikiwa sasa lakini tuendelee kuangalia uwezekano wa kufanya hivyo, maana ki-ukweli ndio jawabu
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyo Kikwete asingemuweka Utoh na kumpa meno kisheria na kuweka shria ya kujadili ukaguzi bungeni, mngeyajuwa hayo?

  Tumieni akili japo kidogo.
   
 5. Ciphertext

  Ciphertext Senior Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uoga tupu.
   
 6. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Angeng'olewa jk wote wangerudi kwenye uchaguzi ndivyo sheria inavyotaka, ishu wameogopa kurudi kwenye uchaguzi sio kumheshim Rais
   
 7. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani hapa wa kuondoka ni JK ndiyo suluhisho la yote.Hata akifanya mabadiliko vyovyote vile kanuni anazo tumia kuteua ni zile zile.Yeye ushikaji mbele mengine yatafuata ndiyo kigezo chake cha kwanza.Hebu tujiulize,alipotoka Msabaha Nishati na Madini uteuzi mpya umeleta tija?
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Siasa zetu zimejaa unafiki tu...kama walikuwa na nia kweli wangempa za uso boss kuliko kutengeneza story
   
 9. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kwa taarifa yako hoyu rais wako dhaifu hakuwa na vision ya kujua kama report ya mteule wake ingewasulubu watendaji wake na kumuacha yeye uchi kama mbumbumbu.

  Rais mapaka ashauriwe na wakina Nape ndiyo anatenda, mimi namini hata hiyo report hakuisoma na kama aliisoma hakùelewa kama angeisoma na kuilewa angekuwa ni mtu wa kwanza kabisa bila hata kusubiri bunge amefanya màmuzi ya kuwaajibisha watendaji wake mapema.

  Tumia akili japo kidogo!
   
 10. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,823
  Trophy Points: 280
  hii habari ya kusema eti mpango wa kumwajibisha Pinda umevuja kutokea CCM na ulilenga mahususi kumuwajibisha raisi na eti Zitto aliudakia ni habari ya uongo na ya kutunga.
  Imagine hoja ya kumwajibisha Pinda wamesaini wabunge 5 tu wa CCM, je ingekuwa ni kuweka saini kwa ajili ya kumwajibisha kikwete kuna mbunge wa CCM angethubutu kuweka saini kweli??
  Hizi Spinning zingine hazina maana zaidi ya kudhalilisha tasnia ya uandishi wa habari.
   
 11. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  Kwa akili zangu kidogo zinaniambia Utoh yupo pale kikatiba, Rais ni lazima amchague mkaguzi mkuu wa mahesabu kwa mujibu wa katiba na si kwa utashi wake,na mkaguzi mkuu wa hesabu anafanya kazi kwa sheria zilizotungwa na bunge na si Rais wako Kikwete na hata Taarifa kujadiliwa bungeni si Rais wako anayeamua ipelekwe ni hitaji la kisheria. mi naona wewe ndio umeshindwa kutumia japo kaakili kidogo Mkuu
   
 12. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sina hakika kama wabunge wa CCM wanauwezo wa kuingoa serikali yao,maana wanaogopa wanaweza shindwa kurudi tena mjengoni kama uchaguzi utaitishwa tena.
   
 13. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani unaishi nchi jirani,****** alimpa meno Utoh alilenga kuzima hoja za wapinzani kuhusu serikali kutowajibika badala yake imekula kwake,alifikiri ingekuwa inajadiliwa tu bungeni na kupotezewa,ndo maana wakati fukuto la shinikizo la kujiuzuru mawazili linaanza alisema nin upepo tu utapita,kama ulivyopita wakati wa mgomo wa madaktari,Kimsingi yeye ndo tatizo,haiwezekani watu unaowateua mwenyewe waboronge halafu usema wewe uko vizuri!,ni mwendawazimu tu anaeweza kuamini hilo.Jk anachofanya ni kama kuvaa nguo mpya wakati anauchafu wa majuma kadhaa bila kuoga,hii haitaondoa harufu ya jasho la uchafu,think deep utaelewa nini namaanisha
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Una uelewa mfupi sana.
   
 15. King2

  King2 JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mwl. Nyerere aliona mbali. Alipinga vikali huyo jamaa (mkwère) kuwa rais. Ona sasa anavyobolonga, serikali vituko vitupu.
   
 16. mujusi

  mujusi JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Sio kweli. Mbona Wabunge wa CCM walikataa kutia saini katika ile karatasi iliyekuwa ikitembezwa na Zitto ya kutafita saini 70 za wabunge. Wangemwondoaje Waziri Mkuu au Rais bila ya kupata hizo saini saini?
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Uelewa wako mdogo sana kuhusu mambo ya nchi.
  Kwanza sio kila aliyeteuliwa na rais anafurahia upuuzi wa serikali hii.
  Pili si kikwete aliyempa mamlaka ya kufanya anavyofanya utoh ila ni katiba. Na kwa taarifa yako katiba imeshamnyima ruhusa ya kumuadhibu utoh kwa namna yoyote ile labda tu utoh mwenyewe aamue kuacha kazi au astaafu.
  Umbumbu wako wa ki ccm unakupoteza.
  Shwaaaaaaaaaaaaaan
   
 18. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,984
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Siasa uchwara,, hakuna cha zitto wala fulukunjombe,,mnayumbisha nchi.
   
 19. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #19
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Naona huyo Filikunjombe anataka ku spin ili ionekane wao ndio waliokuwa na impact, he is dead wrong kufikiri mabaya yao yote yamefutwa na sahihi zao 5.
   
Loading...