Siri ya Kushinda Ubunge,Udiwani Hii Hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri ya Kushinda Ubunge,Udiwani Hii Hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Jan 26, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wakuu! I hope ur all fine.
  Wengi wetu tumekuwa tukiamini kwamba ili mtu ashinde Ubunge au Udiwani basi ni lazima awe na alots of money na hii imepelekea watu wengi hasa vijana na wale wenye kipato kidogo kuogopa kugombea. Hali hii imesababisha wafanyabiashara wakubwa hapa nchi kujikita kwenye siasa kwa kuwa wanauwezo kifedha hata kama hawana good will kwenye game hili. Lakini mtaalam Tip O’Neil- the former Spika wa Marekani anatuambia kwamba fedha sio kigezo cha kwanza cha kushinda Ubunge ama Udiwani au post yeyote ya kisiasa ,yeye anachambua kwamba fedha ni kigezo cha mwisho na sio cha kwanza kama wengi wa Watanzania na nchi nyingine za Afrika tunavyoamini. Hivi ndivyo anavyoeleza……

  First and fore most ni
  Personality…..anachambua kwamba ni lazima mgombea uwe na personality nzuri kwa wapiga kura wako….ni lazima uuzike,ni lazima uwe na mahusiano mazuri na wapiga kura wako….

  Agenda …..Mtaalamu huyu anaamini kwamba agenda ndio kigezo cha pili cha kukufanya ushinde….ni lazima uwe na agenda ambayo inakubalika kwenye eneo husika unalogombea….ukiwa na hii ur likely to win the Election….You must have a specific agenda.


  Organisation…..You must be very well organize so that you can organize ur activities smartly……..Kama utakuwa smart basi ur in a safe side to win

  Resources….
  Hili suala la resources ni la mwisho kabisa lakini ni muhimu kwani suala la fedha halikwepeki kwani unahitaji fedha so that to meet all necessary requirements and activities before and during campaigns.


  Haya ndugu zangu, tukiyazingatia haya Ubunge ni wako,Udiwani ni wako..kazi kwenu.


   
 2. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  vp kuhusu urais, maana huo ndio ninauangalia kwa ukaribu zaidi
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Jan 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Soma kwa makini between lines utagundua kilichochambuliwa.
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Good...lakini hayo yote uliyoweka hapo juu kwa watu wetu wengi huyageuza chini juu, kwa maana kuwa pesa ndio hupewa kipaumbele kuanzia mgombea mwenyewe hadi wapiga kura. Juzi juzi nilikuwa kikazi kwenye wilaya moja kwenye mkoa wa kanda ya kati.Mikakati inapangwa na wapiga kura jinsi ya kuzitafuna pesa za hao wanaoonekana wana nia ya kugombea ubunge...
   
 5. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  asante kwa elimu....
   
 6. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Vipi kuhusu kwenda Mlingotini?
   
 7. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #7
  Jan 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ki uhalisia Tip yuko sahihi kabisa tatizo ni sisi nchi za Afrika tumeweka pesa mbele na ndio maana hatuwapati viongozi makini wanaotufaa..ila kama tukibadilika fikra basi hali ndio inavyopaswa kuwa.
   
 8. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  asante sana gender sensitive kwa kutuwezesha hata sisi tusio na pesa twende jimboni kuukwaa ubunge. na kubaliana na huyo spika kuwa pesa should be the last reason to win election. na kwa mantiki hii ni kwamba hapa bongo wanaoshinda kwa kigezo cha pesa ni watoa rushwa, na watanzania wengi kumbe tu wapokea rushwa kwa sana.na ndo maana viongozi wetu are stealing our money for paying us, or compansating their money given to us during campaigns. so watanzania tuangalie vigezo hivyo vingine vya personality, agenda and so on, ili tusiibiwe.
   
 9. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2010
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tip oneil anaongelea siasa za marekani ambako watu wamekwenda shule na wanaelewa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya vingozi bora na maendeleo. hapa kwetu siasa haziendi hivyo unahitaji chumvi, chupi, khanga, tishati, vitisho, ffu na waandishi makanjanja wakukupamba magazetini. sasa bila hela utawezaje hivyo? kwetu sisi mtu mwenye personlity ni yule mwenye hela. vijembe na vibwagizo ni ajenda tosha. vingine vyote ukiwa na ngawira vitakuja.
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Tutakwenda hivyo mpaka lini?huoni kuwa inawanyima haki wengine wasio na uwezo?huoni kuwa tunapata viongozi wasijali maslahi ya wanachi kwa kuwa wanakuwa wamepita kwa kutumia pesa?
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  naamini haya yana ukweli mkubwa sana; lakini vile vile kinachoeleta tofauti kati ya hivyo vyote siyo personality, resources, organization wala kitu kingine isipokuwa ajenda. Je mgombea anasimamia nini?
   
 12. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwa Tanzania uongezee na chama cha siasa, unachosimama nacho..ni muhimu hasa kwa maeneo ya vijijini
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe...Agenda ni suala la muhimu sana lakini kwa bahati mbaya sana hapa Tanzania ni maeneo machache sana ambayo yanaangalia agenda..wao wamezoea kupewa ahadi fake(zisizotekelezeka)
   
 14. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #14
  May 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nimeirudisha tena,tunaribu kujadili kwa mara nyingine ili kwa wale tunaogombea tupate mbinu mbalimbali za kushinda uchaguzi ulioko mbele yetu.
   
 15. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #15
  May 8, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hata hii thread nina maslahi nayo sana.

  Pia uwezo wa kuwajua/kuwasoma wapinzani wako ni jambo la muhimu sana.Najaribu kuwasoma kwa karibu nikiwa gizani ingawa wao wamejiuza tayari tangu mwaka jana..wengine hata wameshamalizana kabla ya kura za maoni.
   
 16. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #16
  May 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ben kwanini unawasoma wapinzani wako ukiwa gizani?Unaogopa nini kujitokeza hadharani?Wakati ndio huu wa kujitangaza
   
 17. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #17
  May 9, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Huu nao ni mkakati kwa sasa!
   
Loading...