Siri ya Kuchapiwa hii hapa

Siri ya Kuchapiwa hii hapa

Jokajeusi

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2018
Posts
6,336
Reaction score
10,895
Habari Wakuu!

Katika uzi huu nitajaribu kueleza chanzo kikuu cha watu kuchapiwa au kuibiwa wake zao. Lengo la uzi huu si kuleta mitafaruku ndani ya ndoa bali kuishi kwa kufuata misingi mikuu ya maisha ili kufurahia maisha yetu.

Hakuna jambo linalouma kama kuchapiwa, kupigiwa, kulambiwa mke wako umpendae kwa dhati. Mke ambaye unahangaika kutwa kucha kuhakikisha nafurahia maisha. Kiukweli inauma sana na kama hutokuwa na busara basi madhara makubwa huweza kutokea.

Mwanamke hupenda kupendwa, hupenda kuhisi, kusikia, na kuona yakuwa mume wake anampenda. Na wanaume kiasili wanapenda kuona wake zao wakifurahi na wakipendeza. Pia wanaume wanapenda kusikilizwa, kunyenyekewa na kuabudiwa.

Siku hizi watu huhangaika na madawa kuwaridhisha wanawake. Biashara hii imekuwa biashara kubwa ulimwenguni. Na makampuni mamia yameundwa na yananufaika na dawa za nguvu za kiume.

Zipo Siri Kuu mbili ambazo ni chanzo cha wanaume wengi kuchapiwa Mke wako:

1. Kutokushika Amri za Mungu
Hii ni siri ya kwanza, Ikiwa hushiki amri za Mungu na unazivunja kwa makusudi kabisa. Tegemea Usaliti wa kipekee kwa mke wako. Mwanamke lazima achepuke na mwanaume mwingine. Kuchapiwa ni moja ya adhabu kubwa apewayo mtu na Mungu wake. Huwezi ukachapiwa ikiwa unashika amri za Mungu. Haijalishi una kibamia, haijlishi huna pesa, haijalishi wewe una mapungufu kiasi gani. Ilimradi unatimiza mapenzi ya Mungu na unahaja ya kuyafanya basi huwezi kuchapiwa. Amini usiamini ukichapiwa jua hiyo ni adhabu kubwa upewayo na Mungu. Mungu anajua maumivu ya mapenzi yalivyo hivyo adhabu hii ni mahususi na kubwa kama vile maradhi.

Mke wa TAJIRI anaweza akachapwa, Mke wa Waziri, Rais, na Viongozi wakubwa huweza kupigwa tuu na hata kuleta watoto wa nje. Mke wa Wana muziki mashuhuri na maarufu huliwa tuu bila tabu yoyote ikiwa watu hao hawafuati sheria za Mungu. Ila Mke wa Mtu ashikaye sheria na maagizo ya Mungu hawezi kuchapiwa kamwe. Mungu ameichagua adhabu hii mahususi kuutesa moyo wa watu wakaidi. Zipo adhabu za mwili kama Magonjwa, njaa na kadhalika. Ila Adhabu za moyo ambazo ni za kihisia ni usaliti wa mapenzi. Ibrahimu mke wake alikoswa koswa na Mfalme almanusura alambwe lakini Mungu aliingilia kati. Wanaoifahamu hii stori wataungana nami. Huwezi ukala na mke wa Mtu wa Mungu ukasimamisha au ukabaki salama.

Kumbukumbu la torati 28:
30 Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake.

41 Utazaa wana na binti, lakini hawatakuwa wako wewe; kwa sababu watakwenda utumwani.

2. Kutokuoa Mwanamke Bikira
Jamani kuna watu humu wanadhani nimekuja kuwatukana au kukejeli. Hapana kwani kwanza hatufahamiana. Lengo ni kurudisha jamii ikae kwenye mstari. Bikra ni muhimu, nasisitiza Bikra ni muhimu sana. Mama unayesoma hapa. Mlinde mwanao kwa jina la mwenyezi Mungu naye atabaki salama.

Watu wana hangaika kutumia mitishamba ili wawaridhishe wanawake, ndugu zangu mwanamke hata ridhika kama hakuwa wako. Take from me. Haijalishi utamsugua kiasi gani lakini hiyo si muarobaini wa yeye kutokuonja vya nje.

Kijana ambaye haujaoa, shika sana maneno haya ni muhimu kwa maisha yako yote. Shika amri za Mungu na maagizo yake na Oa Bikra. Huwezi kujuta.
Hivyo jukumu la mwanamke ni kutunza bikra yake kwa vyovyote hata atakapoolewa na jukumu la mwanaume ni kushika amri za Mungu na kuoa Bikra.

Nakaribisha Hoja
 
Kutwa mapenzi!viwanda mtajenga saa ngapi?

Sent by Diaspora
 
Bikra labda uende kibaigwa kijijini ndani ndani huko ndo utapata bikra..

Ila ni kweli kuwa na mahusiano na demu ambaye umemtoa bikra wewe mwenyewe ina make sense,demu anakuwa anakufeel kinoma kama utamjali

Sent using Jamii Forums mobile app

Yaani mapenzi yanakuwa hot inatokea hadi kufa mnaweza msipishane hata mwaka.
Mwanamke uliyemtoa bikra ukimjali hata kama huna hela za magorofa na magari si rahisi kuchepuka. Lakini upande wa pili ni kucheza na shilingi chooni.

Embu sikia hii stori ya kweli kumhusu Dada yangu ambayo bila shaka anasadifu wanawake wengi duniani.
Ilikuwa ni harusi ya Dada yangu, Miaka mitano iliyopita. Dada alikuwa amerembwa akarembeka. Kila mmoja home alifurahi nikiwamo mimi. Yalikuwa ni mafanikio ya familia yetu kuona dada yetu akiingia katika ulimwengu wa ndoa. Siku ya Harusi iliwadia. nderemo na shamra shamra zilitawala. Wenye madera walikuwepo, suti haya, magauni ya gharama nao hawakuwa nyuma basi ilimradi harusi ifaane. Matarumbeta na ngoma ziliwafanya waalikwa kuiona siku ile hakuna nyingine ingefuata kumbe ni hisia tuu za furaha.

Tulikuwa ukumbini, maputo na vitu kama unyoya unyoya vilikuwa vikiranda randa mule ukumbini mwa kanisa. Dada yangu alikuwa kapendeza sana. Alivalishwa gauni jeupe kubwa ungedhani asingeweza kuliburuza. Muda mwingi alikuwa kajificha kwa aibu ndani ya shela. Wengi walitaka afunuliwe ili wamuone vizuri lakini wakumfunua alikuwa ni mmoja naam ndiye huyo shemeji yangu aliyekuwa anamuoa.

Muda wa kula viapo uliwadia, sikuamini nilichokiona. Nilimuona Dada akilia kwa hisia kali sana hali iliyompa tabu mshenga wake kumfuta kila mara machozi yake. Moyoni nilijiuliza badala dada afurahi anaolewa yeye analia, ni furaha gani kupitiliza hiyo.
Hatimaye ndoa ilifungwa na historia ikaandikwa.

Baada miezi kadhaa kupita nilienda kumtembelea Dada yangu. Nilipofika tulipiga soga za hapa na pale. Nyingi zilikuwa ni kukumbuka baadhi ya matukio ya harusi yake. Alinionyesha baadhi ya picha na mwisho aliweka CD ya harusi yake. Ndipo nikakumbuka kumuuliza kwa nini alilia siku ile kwa hisia kiasi kile. Hii ni Baada ya kuona kipande kikimuonyesha akilia kwa kwikwi.

Sio Mimi tuu hata wewe usingeamini jibu alilonipa. lilikuwa jibu lililopasua mishipa ya moyo wangu na kufanya mwili kufa ganzi. Aliniambia kuwa alilia kwa sababu hakuamini kama kweli Allen hatamuoa. Binafsi sikumjua huyo Allen zaidi ya Shemeji aliyefunga naye ndoa siku ile. Aliongeza kusema; kilichoniliza si furaha ya kuolewa bali hakuamini ni kweli Alleni mwanaume aliyempenda kwa dhati kuwa hatamuoa tena.

Binafsi nilishikwa na kigugumizi.

mkuu stori hii inahusu wadada wengi wanaoolewa. Wewe wakati unadhani mwanamke unayemuoa analia kwa furaha siku ukiwa kanisani. Kumbe mwenzako analia kutokuamini kuwa hivi ni kweli hatakuwa tena na Ex wake.
 
Back
Top Bottom