Siri ya furaha ni uhuru na siri ya uhuru ni ujasiri...uhuru hupiganiwa, usipopiganiwa hufa.

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,266
23,199
  • Je hivi vitu viwili, uhuru na haki, vinaweza kutenganishwa kimoja kikawepo bila kingine?
  • Je, katika demokrasia, uhuru wa kujieleza unawezekana bila kuwa na haki ya kusikilizwa?
  • Je haki za msingi za binadamu zinawezekana kudumishwa bila uhuru ndani ya taifa?
  • Je woga wa uhuru kwa viongozi wetu unasababishwa na hofu ya kuwajibika?
  • Je maendeleo yanawezekana bila uhuru kuachwa kuota mzizi ndani ya jamii?
Ndugudugu zangu msomaji wa JF hayo ni baadhi ya maswali ninayojiuliza kila nikiamka, je wewe una maoni gani? Nachokoza tu mjadala, karibuni.
 
Wapiganaji wa uhuru wa kweli wameshaenda. Afrika imebaki na viongozi wasiojiamini,wanaotaka kupendwa kwa kulazimisha,wababe kwa nje waadhaifu kwa ndani,wanaotaka kila sifa iwe juu yake,wanaopenda kutajwa na viongozi wa chini yao hata kwenye mkutano wa kijiji,wanaofikiri wanafanya wanachofanya kwa ajili ya kuwatetea watu wanyonge,wakaidi na wabishi,wasio na chembe ya huruma mbele ya wanaoita maskini na wapambanaji na wanyonyaji wakubwa kwa kile kile kinachoitwa sheria na kunyoosha kinachosababishwa na ukomo wa uwezo wao wa kiubunifu na kiakili katika kuendeleza ustawi wa jamii wanazoziongoza
 
..je uongozi wenye chuki na ukatili unaweza kuchochea maendeleo ktk jamii?
Ukishajawa na chuki na ukatili, neno uhuru haliko kwenye msamiati wako na kwa msingi huo huo utawala wa sheria na haki lazima uuweke kando. Jamii inayomsifia kiongozi mwenye chuki na mkatili, ni jamiii isiyoelimika na iliyopofushwa na woga na hivyo kudumisha maisha ya kinafiki na kizandiki. Hata hivyo ni swala la muda tu itajikuta ikionja machungu ya kiongozi huyo kwani maisha ya kinafiki hayadumu na njia pekee ya kujihami na kadhia hiyo ni kupambana na uongozi huo bila woga na bila kuchoka.
 
Kuwa Mwanachama wa CCM ni silaha tosha kwa Rais katili na mwenye visasi na chuki.

Uoga ndani ya CCM unapelekea Rais Katili kuendelea kunenepa na kujiweka kwenye nafasi ya kudumu milele. Pole sana kwa wanaccm kwa sasa mko ICU vinginevyo jitoeni hapo si pema.
 
Mwaka wa 2 sasa ni chuki na visasi halafu majukwaani tunaimba UHURU NA UMOJA,
UHURU usiozingatia haki ya kuishi? Uhuru usiozingatia haki ya kupata habari? UHURU usiozingatia haki ya kusikilizwa? Ati umoja, na kwa neno UMOJA basi mwingine aombewe ili afanye kazi yake vizuri ya kuminya UHURU wa wanaomuombea, duuuuh! Umoja gani huu usiojali msaada kwa madhira waliopata waathirika wa tetemeko? Umoja usiojua kama kuna watu wanakufa kwa njaa? Haya mazingaombwe ni Tanzania tu halaf tunasubiri Mungu atende muujiza mwingine wakati kipomdi cha JK tulisubiri Mungu atende muujiza, haya katenda sasa,
 
Back
Top Bottom