Hata mtoto mdogo anafahamu kuwa chopa inasafiri haraka kuliko landcruiser, kama unasema wale watu wanaomsimamisha barabarani sawa, lakini kama unazungumzia mikutano mingi ya kampeni, basi Lowassa kafanya mingi. Ubovu wa njia ya barabara ni kwamba huwezi kukiona kilichoko mbali na barabara, na huko mbali na barabara ndiko shida nyingi za wananchi ziliko. Watanzania wana tabia ya kutoa huduma nzuri kwa jamii zinazoishi kandokando ya barabara tu ambazo hawawezi kuwakilisha jamii zinazoishi mbali na barabara, huko ndiko ambako nyuma za manyasi, ukosefu wa huduma za barabara, shule, maduka, zahanati, masoko na usafiri vinapatikana. Usafiri wa ndege unakupa picha nzuri ya umaskini kuliko usafiri wa barabara.