Siri nzito ya 'muccob's" hii hapa.

Siri nzito ya 'muccob's" hii hapa.

mm si mwanafunzi wa hapo ..
Ni mjasriamali nilifanya tafiti hiyo kujihakikishia ukweli wa hoja ziibukazo juu ya sifa nzuri ya chuo hicho.
Naweza kumshauri ndugu yangu kujiunga na chuo hicho sasa baada ya kujihakikishia mm binafsi.

Hebu tuwekee huo utafiti hapa kwani inawezekana akili zako ni zilezile
 
Muanzisha uzi kweli umechimba vya kutosha miye nimesoma pale shahada yangu ya kwanza na naomba ni sadiki yote uliyoyasema ni sahihi na cha kuongezea tu mitihani ya kozi ya ugavi na ununuzi pamoja uhasibu na usimamizi wa fedha inapitia bodi husika hivyo kuongeza ubora wa mitihani, vile vile mbinu nzuri za ufundishaji zinazotumiwa na wahadhiri za kutoa mazoezi ya kutosha, kuwapo kwa presentation nyingi na umakini katika usahihishaji wa mitihani.
Ambapo wahitimu hupata GPA kulingana na uwezo tofauti na vyuo vingine ndo vimechangia sana product zinatoka Muccobs kuuzika sana sokoni
 
Kuna jamaa kamaliza hapo toka 2009 kozi ya procurement,ila mpaka leo hajawahi kuitwa hata kwenye interview.
 
mbona hukuandika ukweli kuwa hao ma lecturer wamesoma chuo gani??? pili hukusema chuo hiki ndo kinaongoza kuchukua wanafunzi waliofeli zaidi?? mf.div 3 na 4??? chuo gani SENIOR LECTURER anaitwa MR??????? kina Maprofesa wangapi?? hiki chuo ni sifuri tuu kama kilivyo UDOM!!!
 
Acha promo mkuu kwanz mm cji ng'o kusoma hapo napiga CBE hapa
poa man endelea kila mtu na choice ila mwishoni ndo huwa tofauti inapojitokeza pale unapotoka kwenye dreams na kuingia dunia ya labours!
 
Hata Mzumbe ni 50 acha sifa za kijinga wewe chuo chenyewe wanaosoma 70% hawana boom sababu ya div III na IV 20% div II na 10% div I.
mbona hatukutaja chuo chako unaumia hivyo? unaweza kututajia nasi tuweze kukicheck ili nasi tuone how much you worth?
kingine acha matusi, msela nini?
 
NYIE WATOTO MTAKUWA LINI JAMANI??? kila siku nasema msiangalie chuo angalia hiyo elimu uliyopata inakusaidia nini katika maisha yako? je imekidhi mahitaji yako?
 
Sioni kama kuna ulazima wa kuanza kubishana kuhusu vyuo au aina ya intake ya chuo.

Mleta mada ameitoa kwa mfumo wa prom ambapo amezungumzia ubora wa chuo chao katika kutoa elim na wahitim.

So unapo argue ilikuwa ni vema kuzungumzia ubora wao kazini na elim inayo tolewa chuoni hapo.


Baadhi ya watu mnasema intake yao ni mbovu kwa kuchukua III and IV, inaweza ikawa fact but its not strong, kwa sababu, mtu mbovu nnakwambia hawezi maliza semester 6 zote (unless kuwe na carry) bila disco.

Halafu kila stage ya elimu kwa hapa Tz inajitegemea, yaani ukipata one form four si lazima upate one form six, kuna watu walipata one form four, six wakapata zero/III.


Aina ya intake its not an issue, jaribuni kuangalia ubora wa elimu wanayo itoa chuoni na uwajibikaji wao wakiwa kazini.
 
mbona hatukutaja chuo chako unaumia hivyo? unaweza kututajia nasi tuweze kukicheck ili nasi tuone how much you worth?
kingine acha matusi, msela nini?

Acha uoga tusi gani lipo hapo. Kwani uongo mbona lipo wazi Muccobs wanachukua div 3 na 4 na bahati mbaya 1st na 2nd Degree sijachukua Mzumbe.
 
Hivi, haiwezekani kuandika vizuri kwa herufi ndogo na kubwa ili kuyapa uvutivu wa kusoma mawazo yako. Bila shaka haya ni matokeo ya kuvushwa madarasa. Kuandika kwa herufi kubwa na ndogo katika sentensi si ni masomo ya darasa la pili....!

Sikuyasoma mawazo yako sababu hayavutii.

HABARI WANA JAMVI.


TUMEKUA TUKISIKIA WADAU MBALIMBALI WAKISEMA KUA AJIRA NYINGI HUPEWA WATU WANAOTOKA KWENYE CHUO CHA USHIRIKA KILICHOPO MOSHI 'MOSHI UNIVERSITY COLLEGE OF COOPERATIVE AND BUSINESS STUDIES' YAANI MUCCOB'S,AMBACHO NI CHUO KISHIRIKI CHA 'SUA' YAANI 'SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE'[AMBACHO CHUO HICHO 'MUCCOBS' HIVI SASA KIPO KWENYE MCHAKATO WA KUA CHUO KIKUU KAMILI YAANI KISIWE TENA CONSTITUENT COLLEGE OF SUA] .WATU WANADAI KUA AJIRA NYINGI HUPENDELEWA WADAU WALIOMALIZA KUTOKA CHUO HICHO NA ZAIDI KWENYE TAASISI ZA BIASHARA PIA ZA MAENDELEO YA KIJAMII KAMA NGO'S,WENGI WANASEMA HII INATOKANA NA HISTORIA YA WAFANYAKAZI WENGI KWENYE TAASISI MBALIMBALI KUA NA UMAKINI NA WELEDI WAKIWA KAZINI . (GOOD REPUTATION).MIMI BINAFSI NIMEKUTANA NA WATU WENGI SANA WAKIDAI KUA CHUO HICHO KINATOA WAHITIMU WAZURI NA WALIOIVA.KUNA HABARI PIA ISEMAYO, KAZI ZILIZOTANGAZWA NA TRA WENGI WATATOKA USHIRIKA.( HUMU JF PIA IMEWEKWA).

NIMECHUNGUZA NI KWANINI CHUO HICHI KINAJIZOLEA SIFA HIZO, NA NIMEGUNDUA KUA 'GOOD REPUTATION' INATOKANA NA SABABU ZIFUATAZO;

1. WELEDI WA WALIMU {LECTURERS}
KATIKA TAFITI ZANGU, NIMEGUDUA KUA WALIMU WANAOFUNDISHA KWENYE CHUO HICHO WENGI WAO WAKIWA NI MAPROFESA NA MADAKTARI, WANA SIFA ZIFUATAZO, I).WAMEBOBEA KWNEYE KAZI HIYO YA UFUNDISHAJI (EXPERIENCE) II).NI WENYE WELEDI (DESCPLINE).NA III).WAMEJITOA KWENYE KAZI HIYO.NIMEGUNDUA HILO KUTOKANA IV).VITU WANAVYOVIFUNDISHA VINGI NI VITU AMBAVYO WENGI WAO WANAKUTANA NAVYO NA KUVIFANYAKAZI KATIAKA MAISHA YAO YA KILA SIKU IKIWA WENGI WAO HUTUMIKA KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA SERIKALI, PIA KATIKA KUTENGENEZA SERA NA SHERIA MBALIMBALI JUU YA MASWALA YA USHIRIKA,VIWANDA NA BIASHARA,NA HIVYO KUA NA HIVYO KUWAWIA RAHISI NA HALISI ZAIDI KWA KILE WANACHOKIFUNDISHANA.NA PIA TAFITI WANAZOZIFANYA {RESEARCH] ZIMEKUA ZIKISAIDIA KATIKA KUTATUA MASWALA MBALIMBALI KATIKA UCHUMI.ZAIDI NIMESHUHUDIA JINSI WALIMU WANAVYOHUDHURIA VIPINDI BILA KUKOSA TENA KWA MUDA MUAFAKA ,NAMNA YA UFUNDISHAJI,NA PIA UHUSIANO MZURI ULIOPO KATI YA WALIMU NA WANAFUNZI.

2. PROGRAM ZINAZOTOLEWA.{(UBUNIFU}
INGAWA KUNA PROGRAM ZILIZO ZOELEKA KUTOLEWA KWENYE VYUO VINGINE KAMA, PROCUREMENT,ACCOUNT AND FINANCE PAMOJA NA HUMAN RESOURCE MANAGEMENT , ILA PALE ZINATOLEWA KWA NAMNA YA KITOFAUTI KABISA. HUTOFAUTIANA NA VYUO VINGINE KUTOKANA NA IDADI YA COURSE ZILIZOPO KWENYE PROGRAM HUSIKA, PAMOJA NA MATERIAL YANAYOTUMIKA HUA YAPO KWENYE MUDA SAHIHI,

UBUNIFU
;
UBUNIFU MKUBWA UMEJIONYESHA KWENYE KUTENGENEZA PROGRAM ZA MASOMO ZINAZOENDANA NA MABADILIKO YA KIUCHUMI DUNIANI,UBUNIFU HUO UMEONEKANA KWENYE PROGRAM ZIFUATAZO;

a)'MICRO-FINANCE AND ENTERPRISE DEVELOPMENT'{DEGREE LEVEL}
PROGRAMU HII INAHUSIKA NA MAMBO YA TAASISI NDOGONDOGO ZA KIFEDHA PAMOJA NA UJASIRIAMALI.KAMA ILIVYO SASA , JAMII INAJIKWAMUA KWNYE UMASIKINI KUPITIA TAASISI HIZI NDOGONDGO ZA KIFEDHA(SACCOS) KWA KUJIPATIA MIKOPO YENYE UNAFUU, DUNIA PIA IMEJIKITA KWNYE UJASIRIAMALI NA KUONA NDIO NAMNA PEKEE YA KUDIDMIZA UMASIKINI.PROGRAM HIYO HAIKUISHIA TU HAPO BALI INA WIGO MPANA KATI YA COURSE TAKRIBANI 52 ILIYOJIBEBEA NDANI YAKE KUNA COURSE ZA MAMBO YA BANK,FINANCE,BUSSINES LAW NA NYINGINE NYINGI , COURSE AMABAZO ZINAMPA FURSA MHITIMU KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALI MBALI KATIKA JAMII INAYOMZUNGUKA.PROGRAM HII HUMFANYA MHITIMU KUA WA KISASA NA KUENDANA NA MABADILIKO YA DUNIA KATIKA SWALA ZIMA LA KUJIKWAMUA KIUCHUMI NA KUONDOKANA NA UMASIKINI.

PROGRAM TAJWA HAPO JUU KWA SASA NI KAMA 'LULU' NA NI GUMZO MIDOMONI MWA WATU NA TAASISI MBALIMBALI.

b) 'COMMUNITY ECONOMIC DEVELOPMENT"{DEGREE LEVEL}


SEHEMU MBALIMBALI PROGRAM HII IMEKUA INAJULIKANA KAMA 'COMMUNITY DEVELOPMENT' LAKINI KWA UMAKINI NA UFANISI WA HALI YA JUU,WANAZUONI WA MUCCOBS WALIGUNDUA KUA MABADILIKO NA MAENDELEO YA JAMII YANAENDA SAMBAMBA NA MABADILIKO YA KIUCHUMI, HIVYO BASI WAKAONA KUNA HAJA NA UMUHIMU WA KUWEPO KWA PROGRAM HII ILIKUONYESHA NI KWA JINSI GANI UKUWAJI WA UCHUMI UNALETA MABADILIKO CHANYA KATIKA UKUAJI NA MAENDELEO YA KIJAMII . PROGRAM HII INATOA MAFUNZO JUU YA MAHUSIANO YALIPO KATI YA JAMII PAMOJA NA UCHUMI.

PROGRAM TAJWA HAPO JUU ZOTE CHIMBUKO LAKE NI CHUONI HAPO.


3.TIME TABLE.
RATIBA NYINGI ZA MASOMO NILIZO ZIONA CHUONI PALE ,ZIPO TOFAUTI KABISA NA RATIBA NILIZIZIONA KWNYE VYUO VINGINE. IKIWA NI PAMOJA IDADI YA MASOMO YANAYOFUNDISHWA KWA SIKU PAMOJA NA MUDA WA KILA SOMO KUFUNDISHWA. MASOMO MENGI CHUONI HAPO HUFUNDISHWA KWA MUDA USIOPUNGUA MASAA MAWILI NA RATIBA ZOTE HUANZA KUANZA 8:00am NA KUMALIZIKA 7;30pm. PIA WAMEZINGATIA UWEPO WA KUTOSHA WA SEMINER HOURS. HII INAMPA MWANAFUNZI FURSA YA KUJUA MAMBO MENGI.PIA WALIMU WAMEKUA MAKINI KATIKA KUZINGATIA MUDA,MUDA KIPINDI KINAPASWA KUANZA HUNAANZA NA MDA KINAPASWA KUISHA HUISHA KWA MUDA MUAFAKA. KWA HILI HATA WW UTAWEZA KULISHUHUDIA, CHA KUFANYA FIKA ENEO HILO NA UONE MDA WANAINGIA NA MUDA WANATOKA CHUO NA JINSI WALIMU NA WANAFUNZI WANAVYOPISHANA KUKIMBIA KWNYE VIPINDI.

4.UTUNGWAJI NA USIMAMIZI WA MITIHANI PAMOJA NA WASTANI WA UFAULU..

WASTANI WA UFAULU NI KUANZIA WASTANI WA ..... NA KUENDELEA. MGAWANYIKO UKIWA KAMA IFUATAVYO

ASSIAMENT + QUIZ+PRESENTATION+CLASS TEST {COURSE WORK} 40%
FINAL EXAM 60%


TOTAL 100%


KWA MGAWANYIKO HUO HAUMPI NAFASI MWANAFUNZI KUBEBWA NA COURSE WORK' NA KWA MAANA HIYO ATABAKI KUA NA KIBARUA KIKUBWA CHA KUFANYA VIZURI KWENYE ALAMA 60% ZA MTIHANI WA MWISHO NA LAZIMA ITAMGHARIMU KUSOMA KWA BIDII KUFIKISHA KIWANGO CHA UFAULU.
UTUNGWAJI WA MITIHANI NI WA KIWANGO CHA JUU ,USIMAMIZI WAKATI WA MITIHANI NDIO HATARI KABISAA/USIMAMIZI NI WA KIWANGO CHA JUU.


5. ADABU WALIYONAYO WANAFUNZI.

UKITOFAUTISHA NA VYUO VINGINE TENA UKIZINGATIA IDADI KUBWA YA WANAFUNZI WENGI WA VYUO NI VIJINA, VYUO VINGI WANAFUNZI WAMEKUA WAKIKOSA HESHIMA KWA KUJIINGIZA KWENYE STAREHE MBALIMBALI NA KUWAFANYA WASAHAU KILICHOWAPELEKA,ILA KWENYE CHUO HICHI , WENGI WAO WANAJIHESHIMU NA KUJUA NI NN HASA KILICHOWAPELEKA.WAHUDHURIAJI WAZURI KWENYE VIPINDI NA PIA WANAKUA NA JITIHADA KATI KUSOMA,WAKIZINGATIA ZAIDI KUSOMA KWENYE MAKUNDI.WENGI HUJIONA KAMA WAMETUA MZIGO MZITO PALE IFIKAPO MWISHO WA SEMISTER.
NILIJARIBU KUJIULIZA NI KWANINI WANAFUNZI HAWA WAPO HIVI,NA NILJIULIZA YAFUATAYO,

1.SABABU ZA KIMKOA, MJI WA MOSHI NI MJI TULIVU , MJI WA KIBIASHARA, NA WATU WENGI WAPO BIZY KUTAFUTA HELA KULIKO KUFANYA STAREHE. NI MJI AMBAO HAUNA STAREHE KAMA MJI WA DAR-ES-SALAAM.

2. LABDA ,NI JINSI RATIBA INAVYOWABANA NA KUWAFANYA WASHINDWE KUJIINGIZA KATIKA MASWALA YASIYO NAA MAADILI.

NA MENGINE MENGI AMBAYO NILIJIULIZA ,ILA NILIISHIA KUJUA TUU ..PALE NDIPO ADABU INAFUATA MKONDO WAKE NA TENA ZAIDI UKIWA UNAFANANISHA NA VYUO VINGINE .


HIZO NI KATI TU YA SABABU CHACHE NILIZOWEZA KUZIONA BAADADA YA KUFANYA TAFITI NDOGO KWENYE CHUO CHA 'MUCCOBS' ,NAJUA ZITAKUWEPO SABABU NYINGINE KAMA VILE , MAZINGIRA MAZURI, MANEJIMENTI NZURI NA NYINGINE NYINGI TU ZINAZOKIFANYA CHUO CHA USHIRKA MOSHI KUA ASALI KICHWANI,MIDOMONI NA KWENYE TASISI MBALIMBALI.
HIVYO BASI MSIBAKI KUUMIZA VICHWA NA KUSEMA 'WHY MUCCoB'S' HIZO NDIZO SABABU , VYUO VINGINE YAPASA KUIGA .

BIG UP {MUCCoB'S}
 
Sioni kama kuna ulazima wa kuanza kubishana kuhusu vyuo au aina ya intake ya chuo.

Mleta mada ameitoa kwa mfumo wa prom ambapo amezungumzia ubora wa chuo chao katika kutoa elim na wahitim.

So unapo argue ilikuwa ni vema kuzungumzia ubora wao kazini na elim inayo tolewa chuoni hapo.


Baadhi ya watu mnasema intake yao ni mbovu kwa kuchukua III and IV, inaweza ikawa fact but its not strong, kwa sababu, mtu mbovu nnakwambia hawezi maliza semester 6 zote (unless kuwe na carry) bila disco.

Halafu kila stage ya elimu kwa hapa Tz inajitegemea, yaani ukipata one form four si lazima upate one form six, kuna watu walipata one form four, six wakapata zero/III.


Aina ya intake its not an issue, jaribuni kuangalia ubora wa elimu wanayo itoa chuoni na uwajibikaji wao wakiwa kazini.

Wewe ushawahi ona wapi Tz hii kuna mtu mwenye div 4 form six aliyechaguliwa kujiunga chuo kikuu kwaajili ya degree program??????
 
Acha uoga tusi gani lipo hapo. Kwani uongo mbona lipo wazi Muccobs wanachukua div 3 na 4 na bahati mbaya 1st na 2nd Degree sijachukua Mzumbe.
Hao wa 3 na 4 wanaenda kusomea level gani au unapayuka tu?

Na hapo kwenye red umemaanisha nn? embu andika vizuri ueleweke, maana haueleweki umezisomea Mzumbe ama na kama sio umechukulia wapi?

Na degree mbili inamaana hukuwa na uhakika na degree hiyo ya kwanza kukutoa? au ya pili ni ya nyuki? maana siku hizi mtu anakuambia ana degree mbili kumbe moja ni ya ufugaji wa nyuki ambayo buyer wa labour ni Tanapa peke yake au ajinunue mwenyewe.
 
hivi we umeona suala la ratiba kuanzia saa 8:00asubh hadi 7:30jion ndo usirias wenyewe kweli? mbona kuna vyuo ratiba inaanza saa 7:00asubuh hadi 8:00usiku, hebu uliza UDSM ratiba inaanza saa ngapi na kuisha saa ngapi...na kama ni hao maprofesa na madokta UDSM ndo wamejaa tele....otherwise sema tu kwamba unapiga promo..,
 
Hao wa 3 na 4 wanaenda kusomea level gani au unapayuka tu?

Na hapo kwenye red umemaanisha nn? embu andika vizuri ueleweke, maana haueleweki umezisomea Mzumbe ama na kama sio umechukulia wapi?

Na degree mbili inamaana hukuwa na uhakika na degree hiyo ya kwanza kukutoa? au ya pili ni ya nyuki? maana siku hizi mtu anakuambia ana degree mbili kumbe moja ni ya ufugaji wa nyuki ambayo buyer wa labour ni Tanapa peke yake au ajinunue mwenyewe.

Wewe kama ulipata 3 ukaenda Muccobs usituletee hasira zako hapa hata ukikataa ila ukweli unaujua moyoni kuwa mlio soma Muccobs mlifeli form six na ndio maana wengi wenu hamna vigezo vya kupata mkopo yani chuo chenu aliyejitahidi sana basi ana div II ya 12 na mnamuona kipanga kweli, sina haja ya kurudia rudia comment ukisoma thread yote utaona majibu yangu sio kukurupuka tu na hasira zako.
 
Back
Top Bottom