Siri kuu ya kuuza Kigamboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri kuu ya kuuza Kigamboni

Discussion in 'Major Projects in Tanzania' started by BAK, Apr 18, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,818
  Trophy Points: 280
  Siri ya kuu ya kuuza Kigamboni

  Na Nyaronyo Kicheere

  MwanaHALISI~Maslahi ya Taifa Mbele

  WAKAZI WA wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam, wameshutumu serikali kwa kusema mpango wa kuwahamisha ili kupisha wawekezaji kutoka nje ni "wizi mtupu."

  Wamedai kuwa mradi wa Kigamboni ni wa kupatia fedha za CCM za kufanyia uchaguzi Oktoba 2010.

  Siyo siri tena kwamba wakazi wa Kigamboni watapewa "fidia," watahama au kuhamishwa ili kupisha wawekezaji kutoka nje ambao wanadaiwa watafanya Kigamboni kuwa eneo la kisasa.

  Uhamishaji utafanyika mwaka huu. Anayetajwa kuwa "dalali" wa Kigamboni ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Zephania Chiligati.

  Kwenye uwanja wa Swala, Kigamboni wananchi walimwambia Chiligati,"Huu ni wizi mtupu, sawa na EPA. Ninyi watu wa CCM mnatafuta fedha za kampeni za uchaguzi 2010."

  Wanajeshi wastaafu wamehoji, "Je, askari kastaafu, kapata malipo yake, anaambiwa aondoke kambini lakini nyie (Chiligati) mnamzuia kujenga nyumba eneo lake, sasa watoto wake wakalale wapi, apeleke wapi familia yake?" Chiligati alishindwa kujibu.

  Tayari Chiligati amewatangazia wakazi wa Kigamboni kuwa eneo hilo linahitaji "kuendelezwa" na ametaja sababu zifuatazo.

  Kwanza, ongezeko la watu jijini la asilimia saba kwa mwaka. Pili, Kigamboni kuwa sehemu ya jiji kwa mujibu wa sheria. Tatu, Kigamboni kuwa karibu na jiji na kuwa na mandhari nzuri ya kuvutia watalii.

  Taarifa zinasema tayari mnunuzi amepatikana lakini Chiligati hajawahi kumtaja. Kuna wanaosema mwekezaji ni Mwarabu wa Bahrein; wengine wanasema ni Waarabu wa Dubai; lakini wapo wanaodai eti ni rais mstaafu wa Marekani, George W. Bush.

  Naye Chiligati anasema tayari hatua ya "kuendeleza" Kigamboni imetangazwa kwenye gazeti la serikali ambako inaonyeshwa kuwa kutakuwa na mpango kabambe wa kuijenga upya.

  Katika mikutano yake ya Januari 16 (Chadibwa Beach), Machi 18 (Uwanja wa Swala- Tuangoma) na Machi 19, 2009 (Vijibweni) wilayani Temeke, Chiligati alirudia mara kadhaa kuwa madhumuni ya kuswaga wananchi nje ya Kigamboni ni kujenga mji uliopangika.

  Alisema serikali inataka mji wenye mifumo mizuri ya majengo; wenye huduma za jamii, wenye maeneo ya wazi, wenye maeneo ya uwekezaji na mji wenye mfumo wa kisasa wa mawasiliano.

  Chiligati aliwaambia wananchi kuwa mchakato wa utekelezaji utakuwa pamoja na kutoa tangazo la kusudio alilosema litatoka 24 Oktoba mwaka huu, kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mradi, kutafuta mtaalamu mbunifu wa mji na kuwatambua wakazi na miliki zao.

  Waziri alitaja jukumu jingine kuwa ni kutangazia wawekezaji, kulipa fidia na kuunda mamlaka ya usimamizi wa mradi.

  Alisema wananchi watakaokumbwa na upitishaji miundombinu watapewa viwanja maeneo ya makazi na kulipwa fidia; watakaoamua kuuza maeneo yao watalipwa fidia na wawekezaji na kupewa viwanja maeneo ya makazi; na watakaoamua kuwekeza wataingia ubia na wawekezaji hao.

  Tangazo la kusudio la mradi linalenga kutoa notisi na kuwapiga marufuku wananchi wa Kigamboni kuyaendeleza maeneo yao kwa kuwa watahamishwa.

  Hapa ndipo penye mvutano. Baadhi ya wananchi wanahoji itakuwaje wapigwe marufuku kuyaendeleza maeneo yao wakati ndiyo kwanza mchakato wa kutwaa Kigamboni unaanza na wenye ardhi hawajakubaliana?

  Wasiwasi wa wananchi unatokana na usiri uliotawala taarifa za "mradi wa Chiligati." Wizara ya Ardhi haikutoa taarifa yoyote hadi pale habari hizo zilipoandikwa na gazeti la kila siku la KuliKoni.

  Vilevile wadau ambao watapokonywa ardhi hawakuhusishwa tangu mwanzo, ikiwa ni pamoja na mbunge na diwani wao. Nayo halmashauri ya jiji iliwahi kukana kufahamu mradi huu.

  Wasiwasi unaongezwa na hatua ya Chiligati kuwa mtoa elimu badala ya mamlaka ya kusimamia mradi, ambayo hadi sasa haijaundwa, au viongozi walio karibu na wananchi.

  Kinachoshangaza wengi ni kwa nini serikali haikutoa elimu kabla ya kufikia maamuzi? Kwa hiyo, kinachoitwa elimu ya Chiligati kinachukuliwa kuwa uamuzi umefikiwa na sasa wajiandae kusambaa.

  Kuna taarifa kwamba mwekezaji hataonana na mwananchi mwenye ardhi bali waziri na wataalamu wake. Wataalamu ni pamoja na wale wanaotuhumiwa na wananchi kupora viwanja kumi au ishirini kila mmoja na kuwakosesha wananchi walioathirika kwa bomoabomoa ya Ubungo, Kurasini na maeneo mengine.

  Suala la ubia pia ni jambo lisilowezekana, kwa kuwa Kigamboni hakuna mwananchi mwenye mabilioni ya shilingi ya kuwekeza katika magorofa ya "kupamba mji."

  Hii si mara ya kwanza kwa Chiligati kufika Kigamboni na mradi wa kuuza ardhi ya wananchi. Iliwahi kutokea wakati Kitwana Kondo (KK) akiwa mbunge wa Kigamboni, huku Chiligati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

  Alipima eneo la Vijibweni bila fidia na KK akawaongoza wananchi kugomea ardhi yao kuchukuliwa bila fidia; badala yake viwanja hivyo viliuzwa na wenye ardhi.

  Kitongojini Vijibweni, mzee mmoja alipora kipaza sauti kabla ya mkutano kuanza na kuwatangazia wananchi waondoke katika mkutano huo kwa sababu Chiligati aliwadharau kwa kutofika siku aliyoadhidi na kwamba siku hiyo alipofika alikuwa amechelewa.

  Wengi waliondoka na Chiligati alibaki kuhutubia watu wachache, wengi wao wakiwa watoto.

  Kwa mikutano ya Kibada na Mjimwema, Chiligati aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Kihato ambaye alitofautiana na bosi wake kwa kudai kuwa wananchi watakubaliana na wawekezaji na siyo kuwakilishwa na serikali.

  Kihato alilazimika kutoa lugha ya matusi aliposhindwa kujibu swali la mtu mmoja anayeitwa Machano. Machano alisema, Wewe (Kihato) na wote waliokutuma ni wanafiki."

  Naye DC Kihato akajibu, "Shekh Machano ulienda jando gani wewe, la porini au la hospitali?" Wakazi wa Pwani wanaamini aliyekwenda jando la porini hufunzwa heshima na adabu.

  Alipofika Mjimwema Kihato alishindwa kujibu kwa nini ardhi ya mfanyabiashara wa asili ya kiasia, aliyetajwa kwa jina la Manji, ipatayo hekta 760, haikuingizwa kwenye mradi wa serikali wa kuiuza Kigamboni.

  Muuliza swali hakueleza ni Manji yupi. Mfanyabiashara Yusuf Manji aliwahi kuomba ubunge katika jimbo la Kigamboni.

  Kutokana na hali inavyokwenda, wananchi wa Kigamboni wamejipanga kupinga mradi huo mahakamani. Tayari wameanza vikao vya mkakati.

  Madai ya baadhi ya wananchi ambayo hayajaweza kuthibitishwa yanasema mradi wa Kigamboni ni wa kupatia fedha za CCM za kufanyia uchaguzi Oktoba 2010.

  Kumekuwa na madai kutoka kambi ya upinzani kwamba mwaka 2005, CCM ilitumia makada wake kuchota mabilioni ya shilingi kutoka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT).

  Ardhi ya Kigamboni ndiyo pekee katika jiji iliyosalia yenye thamani kubwa, iliyo karibu na jiji, inayouzika haraka na ambayo wakazi wake wengi ni walalahoi wasiojua mtu yeyote ikulu wa kuwasemea.

  Lakini, Kigamboni iliyo karibu na jiji, yenye pantoni kubwa ya kubeba magari 60 na abiria 2,000; inayojengewa daraja la njia sita pamoja na reli ya Vijibweni, haiwafai tena walalahoi. Je, wananchi wana ubavu wa kuzuia isichukuliwe?
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hao wanajeshi wastaafu nao ni wajinga kwa nini wajibizane na mjinga kama chili? Chukueni silaha mfanye kazi mtukomboe, najua baadhi yetu tutaumia lakini wengine watapona
   
 3. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ni haki yao wananchi wa Tanzania kupewa huduma safi ya kifisadi na Utawala wa CCM. Wananchi walitegemea nini kutoka ndani ya cham kilichpojaa mafisadi??

  Ukipanda Bangi utavuta bangi,siyo mchicha wala kisamvu, pia bangi hiyo hutaila utaivuta.

  Wananchi zidisheni msimamo wenu na mapenzi yenu kwa CCM, CCM imewatoa mbali na ina mpango wa kuwapeleka mbali mkafie huko.

  Shime wananchi wa kigamboni na kila kona ya nchi,ichagueni CCM kwa kipindi kingine cha miaka 5, ili izidi kuwapa huduma safi ya kifisadi.
   
 4. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #4
  Apr 19, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  madilu mie napanda bangi ila sivuti wala kula bange!
   
 5. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Chacha wa Mwita, mkuu, sasa kama hutumii unapanda sababu gani bangi? Unauza bangi? Na kama unauza bila kuonja utajuaje unauza bidhaa bora?
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  mimi nadhani kama sheria ya malipo ikiwa sahihi na kila mtu akipata haki staili sio mbaya kuendeleza eneo na kuwa la kisasa, tatizo ni haki itafuatwa?
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nina maslahi Kigamboni
  Ila kiukweliii ni kwamba
  Hivi sasa serikali inakuja na stories kwamba kutakuwa na negotiations za watakaopenda kuhama au kubaki au ubia na wawekezaji. Narudia tena hizo ni STORIES.
  Wanakuja na hadithi hizi kwa kuwa mwakani ni uchaguzi hivyo wanawaweka sawa watu waone kana kwamba kunamwanga wa matumaini. ila TRUE colors zitaonekana Day one baada ya uchaguzi ndipo asiye na meno ataazimwa ili ajumuike na wote ktk kulia na kusaga meno.
  Kwa nini wasijenge huo mji wa mfano MASAKI au hata ostabei, tusembe Mbezi beach. Kwa nini Kigamboni?? Kwa nini wanaharibu historia ya kule?? waacheni walalahoi wafaidike kuishi huru ktk nchi yao. KAJENGENI DODOMA nyie wavivu wa kufikiri na kupanga ebo!
  Chonde wanakibgamboni wenzangu msikubali kuuzwa na kupuuzwa.
  The year 2010 is here and INDOOR PLUMBING IS BIG....
   
 8. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hivi tofauti ya swali na statement ni nini? kwani binafsi sijaona swali alilouliza sheikh Machano, zaidi ya statement yenye kushutumu unafiki wa viongozi.
   
 9. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Wananchi wote kwa pamoja tuungane 2010 tufanye mabadiliko ya historia. Jana nilikuta kwenye Luninga taarifa inaishia ya wanakijiji huko Kilombero wanaondolewa about 95% ya eneo lao waliloishi kwa zaidi ya miaka 30 linapewa mwekezaji wa miwa. Hii ina maana ni kama kufuta kijiji hicho. Jamani kwa nini tunafanya Watanzania wazalendo wakimbizi ndani ya nchi yao?? Hii ndiyo kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania wakati mtanzania huyo anapokonywa ardhi yake yenye rutuba na rasilimali nyinginezo. Yaani inaniuma sana ninapoona kila kukicha kuna mzozo wa ardhi kati ya wazalendo na wawekezaji, haafu wakiifika viongozi huwa wanakuwa upande wa mwekezaji!!!! Yaani tunasalitiana sisi wenyewe?? Ule udugu na umoja umeshatoweka tangu tarehe 14/10/1999??? Tutafika wakati mitutu ya bunduki italia na ile amani kidogo iliyobaki tangu 14/10/1999 itatoweka?? Poor me, poor citizens, poor future generations of this country!!! Viongozi wetu wamekuwa vipofu, kufumbia macho maslahi ya wenye nchi. Je tutafika???
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wanakigamboni mnalia lia nini?
  Hao si mmewachagua wenyewe ili waweletee maisha bora hayo ndo maisha bora mliyo kuwa mnayataka na hao tayari wamesha plan kuchukua ardhi hiyo mtahamishwa juu juu.
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hii ndi yo bongo mkuu
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hii ndiyo aina ya VIONGOZI KUNTU wa CCM na serikali yake tulionao. inaitwa bongofleva leadership regime.
  ...inayojengewa daraja la KUFIKIRIKA la njia sita pamoja na reli ya Vijibweni.....
   
 13. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2009
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  WIZI MTUPU...............

  Huu ni uonevu wa hali ya juu, yaani tangu huyu Aucle Kikwete aingie madarakani mimi naona migogoro ya Ardhi imekuwa mingi kupitiliza... sijui ni nin hatma ya sisi walalahoi.
   
 14. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi hii jamani raisi wake yuko wapi? Wananchi wangapi watanyanyasika kwa kunyang'anywa haki yao hii? Mbona bora angewaachia basi wakenya na wengineo EAC waingie kumiliki ardhi ingekuwa transparent zaidi ya hili tunalolisikia? Ni kweli lakini? Mbona mie siamini amini kama unyama huu unaweza kuwatokea watanzania?? Tumeikosea nini serikali?

  Na bado kuna hekta 500,000 za mwarabu zinatakiwa, sijui ni mkoa upi utauzwa tena? Mbona tumeshakuwa wageni nchini mwetu?
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wakaazi wa Kigamboni wamechagua wenyewe fungu la kunyanyasika,hawana mtetezi kuanzia Bungeni hadi kwenye Wilaya wakileta za kuleta wataletewa mabuldoza ya kubomoa vijumba vyao na FFU wa kusimamia usalama wa zoezi la ubomoaji.
  Wakati wa uchaguzi utawasikia wananchi wanaimba kwa mbwembwe CCM ina wenyewe na wenyewe ndiyo sisi !!!!!!!!.
  Binafsi nafurahia sana kitakachowatokea wakaazi wa Kigamboni kwasababu wamekuwa wagumu wa kubaini CCM ya leo si ile aliyoiasisi Mwl Nyerere.CCM ya Mwl ilikuwa ni chama kwaajili ya wakulima na wafanyakazi hii ya sasa ni ya wafanyabiashara ambao wako katika siasa kwaajili ya maslahi yao.

  Watanzania haya mambo yatakayowapata wakaazi wa Kigamboni kwa uzoefu wangu tutayatazama kwamba si mambo yanayotuhusu.Tanzania kila mmoja anabeba msalaba wake hakuna kusaidiana kwa hali na mali kuwatetea ndugu zetu wa Kigamboni.
   
 16. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2009
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160

  Kibogoyo: Miradi Ya Wizara Ya Ardhi Inachochea Umaskini
  20th April 2009 @ 21:45, Imeandikwa na KJ Na 4
  TANZANIA ni miongoni mwa nchi zinazokumbana na mabadiliko ya kasi ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Mabadiliko haya yanapelekea kuwepo kwa mabadiliko ya siasa na sera za kiuchumi ili kuendana na mfumo wa uchumi wa dunia kama vile sera za ushindani wa soko, ulegezaji masharti ya biashara, utandawazi na mengineyo.

  Mabadiliko haya yameibua uwekezaji mkubwa wa ndani na kutoja nje, hivyo wananchi kujikuta wakitakiwa kuhama kupisha miradi mbali mali ya maendeleo na ile ya kiuwekezaji. Kwa kuzingatia athari za muda mrefu za kijamii na kiuchumi azipatazo mtu anayehamishwa kutoka kwenye ardhi na makazi yake; Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitunga Sheria za Ardhi Namba 4 & 5 za mwaka 1999.
  Kwa kiwango kikubwa, ikiwa watendaji watazingatia sheria kikamilifu, Watanzania wanaweza kutumia ardhi waliyo nayo kujikwamua kutoka kweye lindi la umaskini.

  Lakini, kushuka kwa maadili ya kitaifa, kushamiri kwa vitendo vya rushwa na tamaa za baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kujilimbikizia ardhi na mali, vinawafanya baadhi ya Watanzania wenzetu waliokabidhiwa hatamu za kutekeleza miradi ya kuwalipa wananchi fidia wanapotakiwa kuhama kugeuka kuwa kikwazo kwa malengo na shabaha za sheria za ardhi kutimia.

  Moja ya mbinu wanayotumia watendaji hawa wanapoanza kutekeleza miradi ya kuchukua ardhi za wananchi ni kuwadanganya na kuwapotosha juu ya kile kinachotekelezwa katika ardhi hiyo ili wasiweze kudai fidia stahiki.
  Mathalani, katika utekelezaji wa mradi wa kituo cha Luguruni, watendaji waliwapotosha wananchi kuwa ardhi hiyo inachukuliwa kwa ajili ya kujenga makao makuu ya wilaya mpya ya Ubungo.
  Hivyo, wananchi walikubali haraka haraka kuondoka kwa kuwa ilonekana ni mradi wa Kiserikali.

  Kumbe, ukweli ni kwamba kilikuwa kinajengwa kituo cha kibiashara cha kwanza na cha aina yake katika Tanzania. Wananchi waliokuwa katika ardhi hii walikuwa na haki ardhi yao kurasimishwa ili waweze kuwekeza katika miradi na biashara zinazokusudiwa badala ya kuondolewa kinyama kama ilivyofanyika.
  Katika mradi wa upimaji viwanja Kwembe, watendaji waliwapotosha wananchi kuwa mradi huo ni wa kuwawekea barabara na miundo mbinu tu; kumbe mradi huo unatwaa ardhi kwa ajili ya upimaji viwanja vya kuuza.

  Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999 inayotawala ardhi zilizoko mijini kifungu 56 kinaelekeza utaratibu wa kurasimisha maslahi ya wananchi katika ardhi. Kifungu kinataka utaratibu huu utumike katika ardhi yote iliyoko ndani ya mipaka ya halmashauri za miji ikiwemo Manispaa. Kifungu cha 57 (e) kinataka utaratibu nitakaoeleza hapa chini uzingatiwe kikamilifu katika ardhi yote ambayo inakusudiwa au imekwishatamkwa kuwa ni kwa ajili ya kupangwa upya chini ya Sheria ya upangaji miji (The Town and Country Planning Ordinance).

  Mwaka 1985 vijiji vyote katika Jiji la Dar es Salaam vilifutwa na hivyo mkoa mzima kutamkwa kwa upangwaji upya. Hivyo kifungu cha hapo kinahusika katika ardhi katika Manispaa zote tatu za Dar Es Salaam. Kifungu cha 58 kinamtaka Waziri wa Ardhi kutangaza eneo kuwa ni eneo la MPANGO WA URASIMISHAJI MASLAHI YA WANANCHI KATIKA ARDHI ama kwa kuombwa Halmashauri ya Mji husika au azimio la mkutano mkuu wa Mtaa au Kijiji. Hivyo, watendaji wa Wizara ya Ardhi kwa kuendekeza maslahi binafsi wanaacha kwa makusudi kuwapatia wananchi elimu ya kuingiza maeneo yao katika mpango huo na badala yake wanawapoka ardhi zao kinyemela.

  Kwa mujibu wa kifungu hiki, wananchi wa maeneo ya Kigamboni, Pugu Kajiungeni, Mji Mwema, Bunju na Kongowe ambako Wizara ya Ardhi inakusudia kupeleka miradi ya kinyonyaji ya vituo vya kibiashara kama hiki cha Luguruni wanatakiwa kukaa katika mikutano yao ya Mitaa na kupendekeza maeneo hayo yatangazwe kuwa maeneo ya MPANGO WA URASIMISHAJI MASLAHI YA WANANCHI KATIKA ARDHI. Hivyo wawe huru kuchagua ama kulipwa fidia au kuwekeza wenyewe katika miradi inayopendekezwa.

  Porojo zinazotolewa sasa hivi na viongozi wa Wizara ya Ardhi kuhusu wanachi walioko katika maeneo hayo ni za kisiasa na si za kweli kwa kuwa hata waathirika wa Luguruni awali waliahidiwa kuwa ni 5% tu watakaohamishwa wale watakaoangukiwa na barabara, miundo mbinu na ofisi za kiserikali. Matokeo yake wananchi wote 259 walihamishwa kinyemela kama tutakavyoona hapa chini.

  Hivyo, wananchi wa maeneo hayo wanatakiwa kutokuamini kauli hizo na badala yake wachukue hatua haraka za kuingiza maeneo katika mipango ya urasimishaji. Vile vile, wananchi wa maeneo mengine ambako ipo miradi ya upimaji viwanja kama vile Mabwe Pande, Goba, na kwingineko Tanzania, pia wanatakiwa kufuata utaratibu huo ili maslahi yao katika ardhi yarasimishwe badala ya watu kulipwa fidia hafifu na kunyang’anywa ardhi yako kiholela.

  Sera ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi ilitolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Mwaka 2004. Katika suala la Ardhi ibara 4.9.2 Sera hiyo inatamka bayana kuwa “Serikali itatumia ardhi kama njia ya kuwawezesha wananchi wake kushiriki kikamilifu kiuchumi.

  Lengo ni kusaidia wananchi watumie ardhi waliyo nayo ama kwa kujipatia hisa katika shughuli za uwekezaji huo au pato lenye kuwanufaisha kushiriki kikamilifu katika shughuli zingine za kiuchumi”. Mkakati wa utekelezaji wa tamko hilo ibara ya 4.9.3.(ii), “Kutoa ardhi kwa wawekezaji wakubwa kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi. Pale ambapo itabidi Wananchi wahamishwe ili kuwapisha wawekezaji wakubwa. Serikali itawasidia utaalamu wa kuingia katika makubaliano muafaka na wawekezaji kwa nia ya kuwanufaisha”.

  Ukisoma Sera hiyo na Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999 utabaini ni kwa kiwango gani zimeweka bayana haki za wananchi na kulinda maslahi yao katika ardhi waliyo nayo. Ila nimeshindwa kuelewa ni kwanini lundo kubwa la Wabunge na Madiwani wa CCM katika Manispaa tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, Halmashauri za Miji na Vijiji nchi nzima hawazitumii Sera na sheria hizi kulinda maslahi ya wananchi katika ardhi na wanawaruhusu watendaji wa Wizara ya Ardhi, Halmashauri za Miji na Wilaya kuwapoka wananchi ardhi zao kifisadi.

  Ninaamini, kuwa moja ya kazi za mbunge, diwani na kiongozi wa Serikali za vijiji na Mitaa ni kusoma sheria ndio maana wanapatiwa mishahara na posho ili waweze kusoma sheria za kuzitumia kulinda hali na maslahi ya wananchi wanaowaongoza. Kitendo cha wabunge, madiwani na viongozi wa vijiji na mitaa kushindwa kutumia sheria kulinda haki na maslahi ya wananchi ni usaliti na kutokuwajibika.

  Katika hili wananchi pia wanastahili lawama kubwa kwa kuwanyanyapaa wapinzani kila wanapoomba kuchaguliwa katika nafasi za ubunge, udiwani, na uongozi wa vijiji na mitaa. Kwa kuzingatia mfumo Chukua Chako Mapema na ufisadi uliojikita ndani ya CCM ni kazi bure wananchi kuendelea kulundika wabunge, madiwani na viongozi wa vijiji na mitaa kutoka CCM kwa kuwa hudhibitiwa kila wanapotaka kukosoa utendaji wa Serikali yao.

  Hivyo, huamua kukaa kimya. Bado tunakumbuka jinsi Mama Anna Kilango na baadhi ya wabunge CCM waliokuwa mstari wa mbele kuikosoa Serikali bungeni wanavyokemewa na kupigwa vijembe ndani ya vikao vya CCM bungeni na hata nje kwa kusema ukweli.

  Kutokana na mfumo huo wa kulindana ndani ya CCM wabunge wasema ukweli wamekuwa wakiwatumia wenzao wa upinzani ambao ni wachache kuzungumzia mambo yenye maslahi kwa taifa. Je, ikiwa Watanzania wangekuwa wameweka nusu kwa nusu pale bungeni ninaamini hata huu ufisadi usingelikuwepo kabisa.

  Kutokana na wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji na mitaa kushindwa kutumia sheria nzuri zilzizopo kulinda maslahi ya wananchi katika ardhi, Watanzania wanatakiwa kufuata nyayo za hayati Mwalimu Nyerere aliyetangaza hadharani kumuunga mkono na kisha kumpigia kura mgombe wa NCCR Ndg Paul Ndobo kwa ajili ya Ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mwaka 1995 na kumuacha mgombea wa CCM aliyekuwa na tuhuma za kufilisi ushirika.

  Ikiwa hayati Mwalimu Nyerere muasisi wa TANU na baadaye CCM aliweza kutambua umuhimu wa kuweka maslahi ya nchi mbele kabla ya maslahi ya chama chake cha CCM kwa kuchagua kiongozi bora na sio bora kiongozi kwa kuwa katoka CCM.
  Mwaka 2009 na 2010 Watanzania wanatakiwa kuamka na kutumia vyema haki zetu za kikatiba kuchagua timu ya viongozi ambao watakwenda kuweka maslahi ya taifa mbele na sio maslahi ya vyama na binafsi Bungeni, katika Mabaraza ya Madiwani na katika Serikali za Mitaa. Itaendelea.

  Mwandishi wa makala hii ni mwanaharakatai wa masuala ya ardhi, anaitwa Ndg Chrizant Kibogoyo. Aliwasaidia sana waathrika wa mradi wa Luguruni kudai haki yao, na sasa yuko bega bega na wakazi wa Kwembe kuhakikisha kuwa unyonyaji unaoendeshwa na watumishi wa Wizara ya Ardhi unakomeshwa ili ardhi waliyo nayo wananchi itumike kuwaendeleza kiuchumi.

  Anapatikana kwa simu 0787-
  125599/0719-126575 au chrizant.k@gmail.com

  Kwanza Jamii,
  Box 2414,
  Iringa,
  Tanzania,
  Email: kwanzajamii@gmail.com,
  Tel: 255 754 678 252
   
 17. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2009
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Wanajamii fualieni hiyo makal kwenye gazeti jipya la **** ENDELEVU KWANZA kila Jumanne ili kubaini uporaji wa ardhi unaoendelea na namn ya kujinusuru ardhi yako isporwe.
   
 18. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huyo mwekazaji awajengee watu nyumba sehemu ambayo watahamishiwa ,au serikali iwajengee nyumba ndivyo haswa inavyofanywa ,hesabuni nyumba za kigamboni halafu jengeni idadi ya nyumba hizo tena muongezee na kaeneo kwa kila nyumbakwa ajili ya kupaki gari na kasehemu ka kulima mchicha na mboga mboga na kajisehemu kadogo cha kuweka ng'ombe mmoja wa maziwa na kajibanda ka kuku.

  Nimeonyeshwa sehemu fulani katika nchi za kiarabu nilipokwenda kununua magari ya biashara ,nikaambiwa hizi nyumba hapa zinajengwa na zikisha malizwa wale watu wa mtaa ule ambao umepakana na bahari watapewa nyumba hizi na kitita cha feza juu ,ili uondoa manunguniko ,halafu zimejengwa bora kuliko zile wanazoishi na nasikia wameshahamishwa na ile sehemu imeshapigwa grader na kusimamishwa mahoteli ya bei mbaya ,sasa serikali isionee raia zake kwa kuwafanya kuwalipa feza na kuwapa kiwanja ,maana ikiwa watamlipa mtu kiwanja na kitita cha kujengea nyumba kwa nini serikali isitumie hivyo viwanja na feza kuwajengea wananchi nyumba na kitakachobakia itakuwa kihama nyumba naamini hakuna atakae lalamika.
   
 19. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2009
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Fikra Endelevu Kwanza la Jumanne Aprili 21-27, 2009

  Kibogoyo: Miradi Ya Wizara Ya Ardhi Inachochea Umaskini
  20th April 2009 @ 21:45, Imeandikwa na KJ Na 4

  TANZANIA ni miongoni mwa nchi zinazokumbana na mabadiliko ya kasi ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Mabadiliko haya yanapelekea kuwepo kwa mabadiliko ya siasa na sera za kiuchumi ili kuendana na mfumo wa uchumi wa dunia kama vile sera za ushindani wa soko, ulegezaji masharti ya biashara, utandawazi na mengineyo.

  Mabadiliko haya yameibua uwekezaji mkubwa wa ndani na kutoja nje, hivyo wananchi kujikuta wakitakiwa kuhama kupisha miradi mbali mali ya maendeleo na ile ya kiuwekezaji. Kwa kuzingatia athari za muda mrefu za kijamii na kiuchumi azipatazo mtu anayehamishwa kutoka kwenye ardhi na makazi yake; Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitunga Sheria za Ardhi Namba 4 & 5 za mwaka 1999.
  Kwa kiwango kikubwa, ikiwa watendaji watazingatia sheria kikamilifu, Watanzania wanaweza kutumia ardhi waliyo nayo kujikwamua kutoka kweye lindi la umaskini.

  Lakini, kushuka kwa maadili ya kitaifa, kushamiri kwa vitendo vya rushwa na tamaa za baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kujilimbikizia ardhi na mali, vinawafanya baadhi ya Watanzania wenzetu waliokabidhiwa hatamu za kutekeleza miradi ya kuwalipa wananchi fidia wanapotakiwa kuhama kugeuka kuwa kikwazo kwa malengo na shabaha za sheria za ardhi kutimia.

  Moja ya mbinu wanayotumia watendaji hawa wanapoanza kutekeleza miradi ya kuchukua ardhi za wananchi ni kuwadanganya na kuwapotosha juu ya kile kinachotekelezwa katika ardhi hiyo ili wasiweze kudai fidia stahiki.
  Mathalani, katika utekelezaji wa mradi wa kituo cha Luguruni, watendaji waliwapotosha wananchi kuwa ardhi hiyo inachukuliwa kwa ajili ya kujenga makao makuu ya wilaya mpya ya Ubungo.
  Hivyo, wananchi walikubali haraka haraka kuondoka kwa kuwa ilonekana ni mradi wa Kiserikali.

  Kumbe, ukweli ni kwamba kilikuwa kinajengwa kituo cha kibiashara cha kwanza na cha aina yake katika Tanzania. Wananchi waliokuwa katika ardhi hii walikuwa na haki ardhi yao kurasimishwa ili waweze kuwekeza katika miradi na biashara zinazokusudiwa badala ya kuondolewa kinyama kama ilivyofanyika.
  Katika mradi wa upimaji viwanja Kwembe, watendaji waliwapotosha wananchi kuwa mradi huo ni wa kuwawekea barabara na miundo mbinu tu; kumbe mradi huo unatwaa ardhi kwa ajili ya upimaji viwanja vya kuuza.

  Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999 inayotawala ardhi zilizoko mijini kifungu 56 kinaelekeza utaratibu wa kurasimisha maslahi ya wananchi katika ardhi. Kifungu kinataka utaratibu huu utumike katika ardhi yote iliyoko ndani ya mipaka ya halmashauri za miji ikiwemo Manispaa. Kifungu cha 57 (e) kinataka utaratibu nitakaoeleza hapa chini uzingatiwe kikamilifu katika ardhi yote ambayo inakusudiwa au imekwishatamkwa kuwa ni kwa ajili ya kupangwa upya chini ya Sheria ya upangaji miji (The Town and Country Planning Ordinance).

  Mwaka 1985 vijiji vyote katika Jiji la Dar es Salaam vilifutwa na hivyo mkoa mzima kutamkwa kwa upangwaji upya. Hivyo kifungu cha hapo kinahusika katika ardhi katika Manispaa zote tatu za Dar Es Salaam. Kifungu cha 58 kinamtaka Waziri wa Ardhi kutangaza eneo kuwa ni eneo la MPANGO WA URASIMISHAJI MASLAHI YA WANANCHI KATIKA ARDHI ama kwa kuombwa Halmashauri ya Mji husika au azimio la mkutano mkuu wa Mtaa au Kijiji. Hivyo, watendaji wa Wizara ya Ardhi kwa kuendekeza maslahi binafsi wanaacha kwa makusudi kuwapatia wananchi elimu ya kuingiza maeneo yao katika mpango huo na badala yake wanawapoka ardhi zao kinyemela.

  Kwa mujibu wa kifungu hiki, wananchi wa maeneo ya Kigamboni, Pugu Kajiungeni, Mji Mwema, Bunju na Kongowe ambako Wizara ya Ardhi inakusudia kupeleka miradi ya kinyonyaji ya vituo vya kibiashara kama hiki cha Luguruni wanatakiwa kukaa katika mikutano yao ya Mitaa na kupendekeza maeneo hayo yatangazwe kuwa maeneo ya MPANGO WA URASIMISHAJI MASLAHI YA WANANCHI KATIKA ARDHI. Hivyo wawe huru kuchagua ama kulipwa fidia au kuwekeza wenyewe katika miradi inayopendekezwa.

  Porojo zinazotolewa sasa hivi na viongozi wa Wizara ya Ardhi kuhusu wanachi walioko katika maeneo hayo ni za kisiasa na si za kweli kwa kuwa hata waathirika wa Luguruni awali waliahidiwa kuwa ni 5% tu watakaohamishwa wale watakaoangukiwa na barabara, miundo mbinu na ofisi za kiserikali. Matokeo yake wananchi wote 259 walihamishwa kinyemela kama tutakavyoona hapa chini.

  Hivyo, wananchi wa maeneo hayo wanatakiwa kutokuamini kauli hizo na badala yake wachukue hatua haraka za kuingiza maeneo katika mipango ya urasimishaji. Vile vile, wananchi wa maeneo mengine ambako ipo miradi ya upimaji viwanja kama vile Mabwe Pande, Goba, na kwingineko Tanzania, pia wanatakiwa kufuata utaratibu huo ili maslahi yao katika ardhi yarasimishwe badala ya watu kulipwa fidia hafifu na kunyang’anywa ardhi yako kiholela.

  Sera ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi ilitolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Mwaka 2004. Katika suala la Ardhi ibara 4.9.2 Sera hiyo inatamka bayana kuwa “Serikali itatumia ardhi kama njia ya kuwawezesha wananchi wake kushiriki kikamilifu kiuchumi.

  Lengo ni kusaidia wananchi watumie ardhi waliyo nayo ama kwa kujipatia hisa katika shughuli za uwekezaji huo au pato lenye kuwanufaisha kushiriki kikamilifu katika shughuli zingine za kiuchumi”. Mkakati wa utekelezaji wa tamko hilo ibara ya 4.9.3.(ii), “Kutoa ardhi kwa wawekezaji wakubwa kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi. Pale ambapo itabidi Wananchi wahamishwe ili kuwapisha wawekezaji wakubwa. Serikali itawasidia utaalamu wa kuingia katika makubaliano muafaka na wawekezaji kwa nia ya kuwanufaisha”.

  Ukisoma Sera hiyo na Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999 utabaini ni kwa kiwango gani zimeweka bayana haki za wananchi na kulinda maslahi yao katika ardhi waliyo nayo. Ila nimeshindwa kuelewa ni kwanini lundo kubwa la Wabunge na Madiwani wa CCM katika Manispaa tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, Halmashauri za Miji na Vijiji nchi nzima hawazitumii Sera na sheria hizi kulinda maslahi ya wananchi katika ardhi na wanawaruhusu watendaji wa Wizara ya Ardhi, Halmashauri za Miji na Wilaya kuwapoka wananchi ardhi zao kifisadi.

  Ninaamini, kuwa moja ya kazi za mbunge, diwani na kiongozi wa Serikali za vijiji na Mitaa ni kusoma sheria ndio maana wanapatiwa mishahara na posho ili waweze kusoma sheria za kuzitumia kulinda hali na maslahi ya wananchi wanaowaongoza. Kitendo cha wabunge, madiwani na viongozi wa vijiji na mitaa kushindwa kutumia sheria kulinda haki na maslahi ya wananchi ni usaliti na kutokuwajibika.

  Katika hili wananchi pia wanastahili lawama kubwa kwa kuwanyanyapaa wapinzani kila wanapoomba kuchaguliwa katika nafasi za ubunge, udiwani, na uongozi wa vijiji na mitaa. Kwa kuzingatia mfumo Chukua Chako Mapema na ufisadi uliojikita ndani ya CCM ni kazi bure wananchi kuendelea kulundika wabunge, madiwani na viongozi wa vijiji na mitaa kutoka CCM kwa kuwa hudhibitiwa kila wanapotaka kukosoa utendaji wa Serikali yao.

  Hivyo, huamua kukaa kimya. Bado tunakumbuka jinsi Mama Anna Kilango na baadhi ya wabunge CCM waliokuwa mstari wa mbele kuikosoa Serikali bungeni wanavyokemewa na kupigwa vijembe ndani ya vikao vya CCM bungeni na hata nje kwa kusema ukweli.

  Kutokana na mfumo huo wa kulindana ndani ya CCM wabunge wasema ukweli wamekuwa wakiwatumia wenzao wa upinzani ambao ni wachache kuzungumzia mambo yenye maslahi kwa taifa. Je, ikiwa Watanzania wangekuwa wameweka nusu kwa nusu pale bungeni ninaamini hata huu ufisadi usingelikuwepo kabisa.

  Kutokana na wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji na mitaa kushindwa kutumia sheria nzuri zilzizopo kulinda maslahi ya wananchi katika ardhi, Watanzania wanatakiwa kufuata nyayo za hayati Mwalimu Nyerere aliyetangaza hadharani kumuunga mkono na kisha kumpigia kura mgombe wa NCCR Ndg Paul Ndobo kwa ajili ya Ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mwaka 1995 na kumuacha mgombea wa CCM aliyekuwa na tuhuma za kufilisi ushirika.

  Ikiwa hayati Mwalimu Nyerere muasisi wa TANU na baadaye CCM aliweza kutambua umuhimu wa kuweka maslahi ya nchi mbele kabla ya maslahi ya chama chake cha CCM kwa kuchagua kiongozi bora na sio bora kiongozi kwa kuwa katoka CCM.
  Mwaka 2009 na 2010 Watanzania wanatakiwa kuamka na kutumia vyema haki zetu za kikatiba kuchagua timu ya viongozi ambao watakwenda kuweka maslahi ya taifa mbele na sio maslahi ya vyama na binafsi Bungeni, katika Mabaraza ya Madiwani na katika Serikali za Mitaa. Itaendelea.

  Mwandishi wa makala hii ni mwanaharakatai wa masuala ya ardhi, anaitwa Ndg Chrizant Kibogoyo. Aliwasaidia sana waathrika wa mradi wa Luguruni kudai haki yao, na sasa yuko bega bega na wakazi wa Kwembe kuhakikisha kuwa unyonyaji unaoendeshwa na watumishi wa Wizara ya Ardhi unakomeshwa ili ardhi waliyo nayo wananchi itumike kuwaendeleza kiuchumi. Itaendelea

  Anapatikana kwa simu 0787-
  125599/0719-126575 au chrizant.k@gmail.com
   
Loading...