Siri hujenga au hubomoa mahusiano?

Siri hujenga au hubomoa mahusiano?

unapokuwa kwenye mapenzi na ukawa muwazi sana kwenye ishu zako wengine wanaichukulia for granted na kuona umekufa umeoza. ni kuwa muwazi huko huko kwaweza vunja mahusiano yako as yaweza tumika kama silaha ya kukuchapa. kwangu mimi siri ni muhimu. Wakati mwingine siri hujenga mahusiano.

Unataka kusema nini mrembo? Una mambo yako ambayo mtu wa karibu katika maisha hayajui? Je, kwa bahati mbaya akijua, si ndo balaa linaanza!
 
Unataka kusema nini mrembo? Una mambo yako ambayo mtu wa karibu katika maisha hayajui? Je, kwa bahati mbaya akijua, si ndo balaa linaanza!

Akiuliza hasa kama ana clue flani nitamwambia ila si mimi kuanza kumueleza,
 
Siri ktk mahusiano yaweza kujenga na kubomoa pia. Mwanzo wa mahusiano ni vizuri kuelezana yote yaliyo ya muhimu na hasa yale ambayo mwenzako akija jua yataleta mtafaruku ktk mahusiano yenu . Kwa mfano je una watoto/mtoto, kipato chako ukipenda kusema, mipango ya ndoa haya yote hayapaswi kua siri. Kuna mambo kama siku hizi vijana kuingiliwa kinyume na maumbile hii hapana si vizuri kusema uliwahi fanyiwa unyama wa namna hii, abortion kwa mdada nayo itegemee na uwezo wa mkaka atalichukuliaje hili lkn ni bora akajua toka mwanzo kama uliwahi fanya abortion.

So kwa nionavyo mimi uwazi ndio mpango mzima iwapo mmeamua kuishi pamoja.
 
kwanini iwe siri? Pia siri ni siri endapo ni ya mtu mmoja! Back to topic :Sometmes siri huimarisha endapo tu siri hiyo itakuwa na madhara kwa mwenza na endapo tu kama haijafahamika!! pia hubomoa mahusiano endapo tu siri hiyo itajulikana kwa mwenza na kama ilikuwa yafaa kufahamishwa hapo kabla.
 
Akiuliza hasa kama ana clue flani nitamwambia ila si mimi kuanza kumueleza,

Kweli tuna mtazamo tofauti katika hili!
.. napenda kuwa muwazi na pia, mtu wangu awe muwazi... maisha ya kuishi hide n play siyafagilii sana.
 
Kweli tuna mtazamo tofauti katika hili!
.. napenda kuwa muwazi na pia, mtu wangu awe muwazi... maisha ya kuishi hide n play siyafagilii sana.

uwazi ukizidi ni madhara, jibu ulichoulizwa ila si kupresent usichoulizwa........nimeishi maisha hayo nimeona madhara yake esp kwa watu walio mbulula
 
kwa upande wangu mm inategemea na aina ya siri, mfano unakuta kwenu kuna matatizo fulani, si vizuri kumwambia mwenza wako ,maana anaweza kukushusha thamani kutokana na ndugu zako( mf labda kaka yako ni mdokozi) bahati mbaya mkazaa mtoto mdokozi, mwanaume ataanza kukutukana na kusema mtoto karithi kwa wajomba zake. lakini ukiweka siri mnakuwa mnashirikiana kutatua tatizo .AU uns historia mbaya ya kuwa na wanaume /wanawake wengi kabla hujakutana naye, hapo kwa kweli si vizuri kumhadithia mwenza wako maana utamfanya asiwe na imani na wewe tena , na inaweza kumpelekea hata mkaachana, akija kujua unamwambia yalikuwa mambo ya ujana na sasa nimebadilika na nakuheshimi mke/mume wangu.
SIRI YA PESA kwa kweli hili linatokana na jinsi mnavyoishi hapo home, kwa upande wangu mimi huwa sisemi kipato chote nipatacho kwa sababu unaweza kuta ndugu yangu ana shida, huwa sipendi kwenda kumuomba mume wangu huwa matatizo ya upande wangu hasa ndugu zangu natatua mwenyewe, nahisi kama kashfa akijua kuwa dada yangu ananiomba pesa, au home kunatakiwa pesa za matumizi, hiyo huwa nacover mwenye kimya kimya, kiasi heshima ya home inabaki pale pale.
 
"Kuna siri mf. Za maisha ya nyuma yasiyopendeza,mmoja anayaficha kwa mwenzake"
siri za maisha ya nyuma hazitakiwi kiuwa siri, mambo ya nyuma yana-belong 2 the past, na kila mtu ana past yake. kama una mtoto, ulishawahi kuolewa hiyo haitakuwa kuwa siri hizo ni facts khs wewe maana zilibadilili pia status zako mfn from single 2 married 2 widow. frm binti 2 a mother/ single mother. so hizo sio siri wa si vitu vya kuficha

"Siri za wapenzi wa siri",
kama bado una wapenzi wa siri wkt una mwenzio uwezekano wa kuingia kwenye migogoro na hatimae kuvunja uchumba/ ndoa ni mkubwa. ila kama unaye lazima iwe siri otherwise hakukaliki

"Siri ya furaha na huzuni katika maisha ya chumbani n.k"
hii ni siri kubwa sana ya kufichwa, yanayojiri room kwetu ni ya kwetu sie wenyewe tu, either tunafurahishana au tunahuzunishana. mwenzako hata kama ana kilema/ udhaifu/ anakupa starehe kubwa sana ambayo hujawahi kuipata kwingine lazima umfichie siri maana hata yeye anatakiwa kufanya hivyo kwako wewe. hata mkiachana siri kama hizo hazifai kumwambia mtu. kuzitoa ni kudharauliana, kutoheshimiana na kuonyesha level ndogo ya maturity.
 
Mkuu Himidini kwa upande wangu naona siri huweza kuvunja mahusiano na hii ni kwa sababu watu wanapoamua kuwa pamoja kama wapenzi wanamaanisha kuwa watakuwa wawazi kwa kila jambo na ndio maana pindi wawili wakifunga ndoa hawawi miili miwiwli tena bali mwili mmoja,sasa je utaufichaje mwili wako jambo?

kuficha siri baina ya watu waili huweza kuvunja uhusiano kwani kuna usemi usemao dunia haina siri kwa hiyo ukimficha mwenza wako siri na akaisikia kwa mtu mwingine,inaweza kuleta madhara kadhaa:

1.kujihisi hufai(kwa nini hakunieleza jambo hili na kuwaeleza wengine,ina maana anaona sina maana au?)

2.kupunguza hisia za upendo juu ya mtu alificha siri kwa kuamini kuwa mtu huyo hakuthamini haoni umuhimu wako.

3.kupoteza hali ya uaminifu baina ya wawili wapendanao.

kwa hiyo nadhani ndani ya mahusiano hakupaswai na siri zozote.
 
Last edited by a moderator:
Siri hizi jaman....achen ziwepo....mm binafsi zimenivusha meng hata sehem ingine nikijifanya mshamba kumbe Nguli....
 
kuna mambo mengine huwezi fanya siri hata kidogo. ila kuwe na mipaka ya kushare taarifa zako na mwenzi wako.
 
Mkuu kuna siri nyingine ni vizuri zikawekwa wazi kama tu wawili hao wanataka kujenga uhusiano wa kudumu:
1. Inawezekana mmoja wao katika safari ya mahusiano alipata mtoto na ambaye labda anaishi na bibi/babu yake. Hapo ni vizuri siri ikawa hadharani, maana inapofichwa na mmojawapo ipo siku itakapofichuka sijui kama ushusiano utaendelea kuw ana afya kama awali.

2. Ni vizuri kila mmoja akawajua ndugu wa mwenzi wake wote kadiri iwezekanavyo, hata kama inatokea ndugu mmoja wapo ana mapungufu. Wapo watu wanaficha kuwatambulisha kwa wapenzi wao ndugu zao weney ulemavu au magonjwa ya kuambukiza. Sio vizuri itambulike kuwa dunia haina siri ipo siku akijua anaweza jenga taswira fulani ambayo siyo nzuri kwa mwenza. Nk

Vile vile kuna siri ambazo si vizuri zikatolewa hadhari au kwa mpenzi wako mpya.
1. Kama uliwahi kubakwa kwa mtindo wa mtungo (kwa wasichana)
2. Kama uliwahi kupata pesa kwa njia isiyo halali halafu ukaachana na njia hiyo, nk.
 
nimependa maelezo yako..........Nakumiss sana.....
 
mimi naona siri zinaweza kujenga au kubomoa kutokana na uelewa na mipango ya mtu anayelengwa. Mfano, mtu mwingine anapenda kuambiwa wakati mwingine hapendi
 
Utata mtupu!
Siri kuhusu watoto, pesa haijengi kabisa.
Wanaume wengine hawana vifua ukimpa kidogo tu yaliyojiri enzi hizo wanapaniki! ya nini masumbufu! Lakini ni vizuri pia ajue kuwa anaweza kufundishwa vilevile, asijifanye anayajua mambo saana!
 
Back
Top Bottom