carmel
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,836
- 262
Recently kumezuka tabia ya kuhalalisha sana kutoka na waume za watu au wake za watu. Tena bila aibu majigambo ya hao wagombea wenza ni kama, aah, yule anajuta kuoana na yule mwanamke/mwanaume, au hampendi basi tu kwa kuwa ni ndoa. au kwa mkewe/mumewe haridhishwi, au anaishi nae tu kwa ajili ya watoto, na mengine mengi mwaweza kuongeza. Lakini cha kunishangaza mie ni kwamba, inakuwaje mume wa mtu anakuja na kukwambia simpendi mke wangu ila wewe, na binti unaamini kabisa wakati kumuacha mkewe hamuachi ila anafanya kwa kificho? the same kwa wanawake wanaocheat kwa kisingizio simpendi mume wangu wakati unaishi nae kila siku. Mi nadhani ifike mahali tuukubali ukweli kwamba mke/mume wa mtu ndie the first one no matter what, hata ukiwa unatoka naye ujue ana familia na ukweli ulio wazi ni kwamba kwa nyumba ndogo anachofata ni 20% na 80% ziko kwa nyumba kubwa. Na mara zote ni wachache sana wanaokubali kuacha 80% na kufata 20%. So ukiwa unatoka na mume au mke wa tu ujijue we ni mshka pembe so no need to boost. au kwa ufupi kipoozeo. Tafakari na chukua hatua.