pedama
JF-Expert Member
- May 11, 2015
- 236
- 144
Habari wapendwa. Mwenzenu sipendi kukiri udhaifu. Sipendi kuhurumiwa, sipendi kueleza shida zangu kwa mtu. Ikitokea nikamweleza mtu matatizo huwa najutia Sana. sipendi kujishusha, sipendi mtu anione na tabu zangu au Shida yoyote inikute alafu anipe pole. Sipendi nionekane dhaifu, Hata nikiwa mjamzito sijipendi kwani watu huniweka kwenye spesho group. Mbaya zaidi hata wakati wa kujifungua huwa nanuna tu kuonesha kwamba ninamaumivu. Nikiwa nasex kidogo nachangamka kiasi. Sina rafiki wa kudumu kwani Sina la kumwambia.
Muda mwingi niko serious hadi nikijiangalia kwenye kioo najicheka. Nikiwa natembea mara nyingi watu huniuliza kwa nini nimenuna kiasi hiki, Nawajibu ndivyo nilivyo wanashangaa. Nikitoka kibaruani sitoki tena nyumbani. Mara chache nawatembelea majirani watatu kila mmoja dk10 kuwajulia hali. Sipendi wageni kwani mara nyingi wananipangulia ratiba ya muda(hasa wa kuwa jf) pesa na mara nyingi nakosa stori nao. Ninapopatwa na matatizo sipendi mtu aniambie pole maana kama nina hasira au huzuni nikipewa Pole najikuta nalia sana. Kwa hali kama hizi unahisi kunawatu nawakwaza? Kuna tatizo katika haya?
Ushauri wenu wapendwa.