Sioni sababu ya kuwazuia wahamiaji wanaopita

wakimataifa.

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
1,625
554
Kila kukicha serikali inawakamata wahamiaji wanaotoka Ethiopia somalia wakiwa wamefichwa kwenye magari.

Lengo lao kubwa kupita kwenda A.kusini wanapita kenya Tanzania wanapita Malawi na kuendelea.
la muhimu ni kuwadhibiti wasiishie hapa nchini au kuwakabidhi UN.
 
kila kukicha serikali inawakamata wahamiaji wanaotoka Ethiopia somalia wakiwa wamefichwa kwenye magari.
lengo lao kubwa kupita kwenda A.kusini wanapita kenya tanzania wanapita malawi na kuendelea.
la muhim ni kuwadhibiti wasiishie hapa nchini au kuwakabidhi UN
uko sahihi sana
 
Hiyo kweli kabisa,mbona nchi za ulaya haziwachukulii wakimbizi kama wahalifu?hapa tanzania hudhalilisha sana wakimbizi toka somalia,ethiopia,eritrea badala ya kuwasaidia kuokoa maisha yao.Pesa wanazolipa kwa vishoka wa kuwavusha ni nyingi sana, zingeweza ingia serikalini kama wangeruhusiwa kupita kwa passport kama wageni wengine
 
kila kukicha serikali inawakamata wahamiaji wanaotoka Ethiopia somalia wakiwa wamefichwa kwenye magari.
lengo lao kubwa kupita kwenda A.kusini wanapita kenya tanzania wanapita malawi na kuendelea.
la muhim ni kuwadhibiti wasiishie hapa nchini au kuwakabidhi UN
Hili wazo ni la msingi na la maana. Linafanyika tu kwa sababu hatuna viongozi wabunifu.

Watu wanateswa huko makwao na hata kuuawa mpaka wanaamua kukimbia kutafuta salama yao, bado tukiwapata humu nchini tunawarudisha kwao na hata kuwafunga. Wengine wakirudi kwao wanauawa, huu si ubinadamu.

Kwa nini serikali isitafute utaratibu wa kibinadamu wa kuwaruhusu wapite kuliko kuwazuia na kuwafanya wawe wanafia kwenye malori wanayofichwa kwa kukuosa hewa?
 
Nyee hamjua sheria za Kimataifa. Ndo maana hata Ulaya wamezuia maeneo mengi. Ingawa Kansela wa Ujerumani ndo anawasumbua tu. Wote wanarudishwa kwao.

Makambi mengi yako Uturuki kwa ajili yao na nchi hizi zinatoa huduma kule.

Ila kwa sababu ni wengi sana wengine wanatoroka kwa njia ya maji na ndo tunawaona wanaingia kwa sasa.
 
Ni vigumu sanna kuelewa au kujua madhara ya uhamiaji haramu. Akili yako bado inawaza siasa na pasipo kuangalia national security. Hii dhana ya uhamiaji kwako ni maji marefu mno ww jadili tu hoja za wasaka tonge wanafki wa bungen
 
Ni kweli hasa mkuu
sio wote wema ni haki ya uhamiaji kuhakikisha kuwa yeyote haingii nchini kinyume cha utaratibu.
hata wahamiaji haramu wenyewe wanajua ndio maana wanajificha kama wahalifu.
ukiruhusu wapiti holela hamna tija yeyote zaidi ya hatari kwa raia na nchi nzima kiujumla.
magaidi nao watakuja kwa njia hizo watafika sehemu wanavamia.
Na hamna nchi inayoruhusu watu wapite tu hata wewe umeweka fence then jitu linakatiza tu kwako eti short cut linaenda mtaa wa nyuma utakubali?
 
Jana 83 wamefungwa miaka mitatu kwa kuingia nchini bila ya kibali it wont be long kabla Ethiopia na Amnesty International kutuma barua zao kulikoni ndio mambo yanavyofanyika hivyo mi sijawaji kusikia nchi inayofunga wahamiaji haramu au kuwa detain bila ya wao kukataa kurudi kwa hiari walipotoka isnt that somewhere in internation charter; jaji kama huyu ndio anaweza kukupa life kisa kucheza ngoma na fisi kwa tuhuma za kutumia vibaya nyaraka za serikari.
 
kila kukicha serikali inawakamata wahamiaji wanaotoka Ethiopia somalia wakiwa wamefichwa kwenye magari.
lengo lao kubwa kupita kwenda A.kusini wanapita kenya tanzania wanapita malawi na kuendelea.
la muhim ni kuwadhibiti wasiishie hapa nchini au kuwakabidhi UN

Anayepita kwenda mfano Afrika Kusini PASSPORT YAKE lazima iwe imegongwa visa ya Afrika kusini hasa akitokea ethipopia na somalia.Unakuta wengine hata hawana.Unasemaje wanapita na hawahamii nchini kwako? Wako wasomali waliingia kupora mbugani Arusha wakiwa na zana za kivita ilibidi jeshi liiingilie kati.UJUE KUNA WAPITAJI NA WAHAMIAJI haramu ukimdaka anasema nilikuwa napita ukimwacha unakuta jambazi sugu limehamia nchini au gaidi linaendesha ugaidi.

Mpitaji anapita mipaka halali na njia halali akiwa na documents halali.Haramu utakuta mara amejificha kwenye mapipa,anapita njia za panya anasafiri kwa kujificha nk

Mtu utasemaje anapita hajapita hata mpakani kwako unamwona yuko ndani ya nchi yako si hatari hiyo
 
Jana 83 wamefungwa miaka mitatu kwa kuingia nchini bila ya kibali it wont be long kabla Ethiopia na Amnesty International kutuma barua zao kulikoni ndio mambo yanavyofanyika hivyi mi sijawaji kusikia nchi inayofunga wahamiaji haramu zaidi ya kuwarudisha walipotoka isnt that somewhere in internation charter

Kuna sheria za nchi husika kale nguruwe hadharani uarabuni ndipo utajua.Sheria za kimataifa zinaruhusu mtu kula chochote lakini sheria za nchi zinasema ole wako ule nguruwe utakiona cha mtema kuni.
 
Wakimbizi wanataabika kutafuta nusura. Kuwafunga ni ukatili busara ni kuwarejesha au kuwapa right of passage.
 
Kuna sheria za nchi husika kale nguruwe hadharani uarabuni ndipo utajua.Sheria za kimataifa zinaruhusu mtu kula chochote lakini sheria za nchi zinasema ole wako ule nguruwe utakiona cha mtema kuni.
Lazima utakuwa unasumbuliwa na 'bacterial vaginosis' ama una homa ya zika sio bure unajua misingi ya human rights na international charter directive kwenye treatment za watu kama hawa au unapayuka tu kwani Tanzania sio member state. Wakisema wanakimbia persecution huko walipotoka au hata economic migrants halafu wewe unawafunga kisa awana mwanasheria wa maana utasemaje, kuwafunga hao watu ni makosa huitaji mimi kukwambia ipe siku kadhaa utasikia kitakachotokea.
 
zipo hela za wahamiaji UN ila kwa nchi hizi wanaopita hawataki kutoa kwa A kusini wanawapa na ndio maana wanakimbilia huko.
dawa wakikamatwa ni kuwakabidhi UN ofisi zao zipo
 
Mkimbizi anatakiwa kujikabidhi ofisi za UNHCR ambazo ziko kuanzia nchini kwao nchi zote wanakopita ofisi hizo zipo.Pia kuna makambi ya wakimbizi kenya,tanzania,nk ilibidi waripoti huko kama wana genuine case.Huwezi kuingia nchi ya mtu enzi hizi za kupambana na ugaidi.Mtu kama hataki kwenda UNHCR anaenda kusumbua watu dawa yake ni nini?

Mkimbizi wa kiuchumi unaposema warudishwe kwa gharama ya kodi ya nani? Nchi haitengi bajeti kwa ajili ya kurudisha makwao wahamiaji haramu au magaidi wanaojitia wanapitia nchini kwako kwenda sehemu nyingine .Wakiwa hawana documents ni wajibu wa nchi husika iliyowadaka kuwashughulikia.Ukiwaachia wakaenda kufanya ugaidi nchi ya mwenzio hujatenda haki na jirani naye atawachia magaidi wapite bila documents waje kwako.

Mfano huyo anayejitia anapita bila documents ni gaidi anaenda lipua ubalozi wa marekani malawi wewe ukasema maadamu unapita pamoja na kuwa huna documents nenda tu akifika akalipua na wamarekani wakajua alipita kwako huo muziki si utakuwa mkubwa?

Mtu mwema na raia mwema hutumia nia njema kusafiri hata akitoroka lakini hujikabidhi kwa mamlaka husika

Tanzania tuna maelfu ya wakimbizi wala hawajafungwa wako makambini wanalishwa hao wanaoingia kinyemela na kwa kujificha ni wahalifu
 
zipo hela za wahamiaji UN ila kwa nchi hizi wanaopita hawataki kutoa kwa A kusini wanawapa na ndio maana wanakimbilia huko.
dawa wakikamatwa ni kuwakabidhi UN ofisi zao zipo

Hata nchini kwao wanakotoka ofisi za UN zipo wangeenda kujikabidhi huko huko kwao.Tanzania tuna sheria zetu sababu ukidakwa jela,faini kisha rudi kwenu kwa gharama zako au jela tena
 
Vita isikike tu, watu walikuwa na maisha yao, inawalazimu watafute njia zozote watoke maana wakibaki maisha ni magumu zaidi isitoshe unakuta mtu familia yote imesambaratishwa wazazi wameuwawa au kawapeleka kijijini na yeye anaamua kwenda kutafuta maisha awasaidie.

Ni vigumu kupata passport kwenye nchi ya vita kwani wengi hawakutarajia kusafiri hata siku moja. Kwa hiyo wengi wanaoondoka wanauza kama ni dhahabu au vitu vya thamani, wanakuwa na Cash hapo ndipo deal linatafutwa kwani kila sehemu wakienda hata Europe wanadhurumiwa hela zao zote.

Imagine mtu anahangaika na maisha kupita kote huku ameweka maisha yake hatarini kwa ajili ya watoto wake wapate rizki halafu na pocket money unamnyang'anya that's not fair au unamuuwa kabisa au kumfunga.

Hawa wqtu wanahitaji ukarimu wa hali ya juu kuangalia afya zao kuwapatia sehemu ndio maana UN iliundwa kwa sababu kama hizi.
Kuwafanya wahalifu ni dhambi itakayotutafuna na kuwarudisha kwao wanaweza kuuwawa tena
 
Mkimbizi anatakiwa kujikabidhi ofisi za UNHCR ambazo ziko kuanzia nchini kwao nchi zote wanakopita ofisi hizo zipo.Pia kuna makambi ya wakimbizi kenya,tanzania,nk ilibidi waripoti huko kama wana genuine case.Huwezi kuingia nchi ya mtu enzi hizi za kupambana na ugaidi.Mtu kama hataki kwenda UNHCR anaenda kusumbua watu dawa yake ni nini?

Mkimbizi wa kiuchumi unaposema warudishwe kwa gharama ya kodi ya nani? Nchi haitengi bajeti kwa ajili ya kurudisha makwao wahamiaji haramu au magaidi wanaojitia wanapitia nchini kwako kwenda sehemu nyingine .Wakiwa hawana documents ni wajibu wa nchi husika iliyowadaka kuwashughulikia.Ukiwaachia wakaenda kufanya ugaidi nchi ya mwenzio hujatenda haki na jirani naye atawachia magaidi wapite bila documents waje kwako.

Mfano huyo anayejitia anapita bila documents ni gaidi anaenda lipua ubalozi wa marekani malawi wewe ukasema maadamu unapita pamoja na kuwa huna documents nenda tu akifika akalipua na wamarekani wakajua alipita kwako huo muziki si utakuwa mkubwa?

Mtu mwema na raia mwema hutumia nia njema kusafiri hata akitoroka lakini hujikabidhi kwa mamlaka husika

Tanzania tuna maelfu ya wakimbizi wala hawajafungwa wako makambini wanalishwa hao wanaoingia kinyemela na kwa kujificha ni wahalifu
Subiri tuipe siku kadhaa tuone mwisho wake hili sio swala la mimi hila najua kuna watu wakisikia haya the likes of amnesty international, human rights watch, etc watakwambia zaidi kama ni sahihi kuwafunga wahamiaji haramu tena waliokuwa na malengo ya kwenda kwingine.
 
Nilifikiri kuwafunga jela ni kujiongezea gharama serikalini na kuzidi kukuza tatizo la msongamano kwenye magereza yetu. Nadhani njia bora ingekuwa kuwasiliana na nchi husika warejeshwe walikotoka. Jela iwe ni kwa wanaowasafirisha na wanaogoma kurudi kwao bila sababu za msingi.

Nilishawahi kumuuliza jamaa mmoja pale Uhamiaji HQ kuhusu suala hilo akanijibu kwa mkato "mradi wa wakubwa huo usiulizeulize". Sijui kama nguvu ya aina hiyo hutumika kwa wale wanaozamia kabisa ndani ya nchi.
 
Subiri tuipe siku kadhaa tuone mwisho wake hili sio swala la mimi hila najua kuna watu wakisikia haya the likes of amnesty international, human rights watch, etc watakwambia zaidi kama ni sahihi kuwafunga wahamiaji haramu tena waliokuwa na malengo ya kwenda kwingine.

Waambie hao human rights watch watoe nauli za kuwarudisha makwao au wawachukue wao wae wanawatunza na kuwagharimia.Na ni vizuri waanzie kuwatunza nchini kwao huko watokako.Ukimshika mkimbizi haramu unamweka wapi kama huna nauli ya kumrudisha kwao? Jela ndio sehemu ya kumuweka hadi siku nauli itakapopatikana.Huwezi kumweka kwenye maeneo ya watu sababu humjui kama ni jambazi sugu au chinja chinja au akskari mwasi anayetoroka vita nchini kwao.
 
Nadhani njia bora ingekuwa kuwasiliana na nchi husika warejeshwe walikotoka..
Kuna tatizo hapo.Uchukulie wewe ni mtanzania huna passport umedakwa Afrika ya kusini.Afrika ya kusini wanawasiliana na Tanzania kuwa kuna mtu wako mhamiaji haramu huku hana documents tumemdaka.Tanzania haiwezi kusema sawa.Tunatuma nauli umlete!! Wanamjuaje kuwa ni mtanzania wakati hana makaratasi? unamjua kwa kuongea kiswahili? Kiswahili nchi nyngi zinaongea.Kuhakiki huyo mtu kama ni raia wako au la kwaweza chukua muda mrefu mno na nchi nyingi huwa hata hazihangaiki Wanakausha kuwa utajua mwenyewe utafanyaje na huyo mtu wako.Unakuta serikali iliyomshika iko desparate inampreleka jela na inamrudisha mpaka alikoingilia na kumwambia ole wako tukuone tena.

Wanaopata usaidizi ni wale ambao ndugu zao huenda wizara za mambo ya nje kuomba msaada warudi hutoa nauli husika nk Ndugu wakikauka watu huozea jela.Wako watanzania wameozea jela
 
Back
Top Bottom